< 1 Timotheo 6 >
1 Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
Let as many servants as are under the yoke count their own masters worthy of all honor, that the name of God and [his] doctrine may not be blasphemed.
2 Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao ni waaminio, ambao ni wapenzi wao. Fundisha mambo haya na uwahimize kuyafuata.
And they that have believing masters, let them not despise [them], because they are brethren; but rather do [them] service, because they are faithful and beloved, partakers of the benefit. These things teach and exhort.
3 Ikiwa mtu yeyote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Yesu Kristo na yale ya utauwa,
If any man teacheth otherwise, and consenteth not to wholesome words, [even] the words of our Lord Jesus Christ, and the doctrine which is according to godliness,
4 huyo amejivuna wala hajui kitu chochote. Yeye amejaa tamaa ya mabishano na ugomvi kuhusu maneno ambavyo matokeo yake ni wivu na mapigano, maneno ya ukorofi, shuku mbaya,
He is proud, knowing nothing, but doting about questions and strifes of words, from which cometh envy, strife, railings, evil surmisings,
5 na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.
Perverse disputings of men of corrupt minds, and destitute of the truth, supposing gain to be godliness: from such withdraw thyself.
6 Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
But godliness with contentment is great gain.
7 Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu.
For we brought nothing into [this] world, [and it is] certain we can carry nothing out.
8 Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo.
And having food and raiment, with these let us be content.
9 Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka huanguka kwenye majaribu, na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi.
But they that will be rich, fall into temptation, and a snare, and [into] many foolish and hurtful lusts, which drown men in destruction and perdition.
10 Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.
For the love of money is the root of all evil: which while some have coveted, they have erred from the faith, and pierced themselves through with many sorrows.
11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.
But thou, O man of God, flee from these things; and follow after righteousness, godliness, faith, love, patience, meekness.
12 Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi. (aiōnios )
Fight the good fight of faith, lay hold on eternal life, to which thou art also called, and hast professed a good profession before many witnesses. (aiōnios )
13 Nakuagiza mbele za Mungu avipaye vitu vyote uhai, na mbele za Kristo Yesu ambaye alipokuwa anashuhudia mbele ya Pontio Pilato alikiri ukiri mzuri,
I give thee charge in the sight of God, who maketh alive all things, and [before] Christ Jesus, who before Pontius Pilate testified a good confession;
14 uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,
That thou keep [this] commandment without spot, unrebukable, until the appearing of our Lord Jesus Christ:
15 ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe: yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana,
Which in his times he will show [who is] the blessed and only Potentate, the King of kings, and Lord of lords;
16 yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen. (aiōnios )
Who only hath immortality, dwelling in the light which no man can approach; whom no man hath seen, nor can see: to whom [be] honor and power everlasting. Amen. (aiōnios )
17 Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie. (aiōn )
Charge them that are rich in this world, that they be not high-minded, nor trust in uncertain riches, but in the living God, who giveth us richly all things to enjoy; (aiōn )
18 Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali zao na wengine.
That they do good, that they be rich in good works, ready to distribute, willing to communicate;
19 Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.
Laying up in store for themselves a good foundation against the time to come, that they may lay hold on eternal life.
20 Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
O Timothy, keep that which is committed to thy trust, avoiding profane [and] vain babblings, and oppositions of science falsely so called;
21 ambayo wengine kwa kujidai kuwa nayo wameiacha imani. Neema iwe nanyi. Amen.
Which some professing, have erred concerning the faith. Grace [be] with thee. Amen.