< 1 Timotheo 6 >

1 Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.
As many as are under the yoke of slavery should consider their own owners to be worthy of full respect, so that God's name and doctrine not be slandered.
2 Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao ni waaminio, ambao ni wapenzi wao. Fundisha mambo haya na uwahimize kuyafuata.
Those who have owners who are believers must not disregard them because they are brothers; instead they must serve them even better, because those receiving the good service are believers and beloved. Teach and exhort these things.
3 Ikiwa mtu yeyote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Yesu Kristo na yale ya utauwa,
If anyone teaches differently and does not consent to sound words, the words of our Lord Jesus Christ, and to the doctrine that accords with godliness,
4 huyo amejivuna wala hajui kitu chochote. Yeye amejaa tamaa ya mabishano na ugomvi kuhusu maneno ambavyo matokeo yake ni wivu na mapigano, maneno ya ukorofi, shuku mbaya,
he is conceited and understands nothing. Rather he is obsessed with controversies and hair-splitting word battles, from which come envy, strife, slanderings, evil suspicions,
5 na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.
constant wranglings of men with corrupted minds and destitute of the Truth, who suppose that godliness is a means to financial gain. Keep away from such people.
6 Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
Now godliness with contentment is great gain.
7 Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu.
We brought nothing into the world and it is certain that neither can we take anything out.
8 Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo.
So having food and clothing we will be content with that.
9 Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka huanguka kwenye majaribu, na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi.
But those who want to get rich fall into temptation and a snare and into many foolish and harmful desires, that plunge people into ruin and loss;
10 Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.
because the love of money is a root of all kinds of evil; in their greediness some have been led away from the faith and have impaled themselves on many distresses.
11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.
But you, O man of God, flee these things; rather pursue righteousness, godliness, faith, love, endurance, gentleness.
12 Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi. (aiōnios g166)
Fight the good fight of faith; take hold of the eternal life into which you were called—indeed, you confessed the good confession in the presence of many witnesses. (aiōnios g166)
13 Nakuagiza mbele za Mungu avipaye vitu vyote uhai, na mbele za Kristo Yesu ambaye alipokuwa anashuhudia mbele ya Pontio Pilato alikiri ukiri mzuri,
In the presence of the God who gives life to all things, and of Christ Jesus who testified the good confession before Pontius Pilate, I charge you
14 uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,
to keep this commandment without spot, blameless until the appearing of our Lord Jesus Christ,
15 ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe: yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana,
which He will manifest at the proper time—He who is the blessed and only Sovereign, the King of kings and the Lord of lords;
16 yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen. (aiōnios g166)
who alone has immortality, residing in unapproachable light; whom no man has seen or can see; to whom be honor and eternal power. Amen. (aiōnios g166)
17 Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie. (aiōn g165)
Command those who are rich in this present world not to be haughty, nor to rely upon the uncertainty of riches but on the living God, who richly provides us with everything to enjoy; (aiōn g165)
18 Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali zao na wengine.
they are to do good, to be rich in good works, to be generous sharers
19 Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.
—storing up for themselves a good foundation against the time to come, so that they may lay hold on the eternal life.
20 Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
O Timothy, guard the deposit! Turn away from the godless, empty chatter and inconsistencies of what is falsely called ‘science’
21 ambayo wengine kwa kujidai kuwa nayo wameiacha imani. Neema iwe nanyi. Amen.
—by professing it some have erred concerning the Faith. The Grace be with you. Amen.

< 1 Timotheo 6 >