< 1 Wathesalonike 1 >

1 Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo: Neema iwe kwenu na amani.
Paul, and Sylvanus, and Timothy, to the congregation of the Thessalonians, which is in God the Father, and in the Lord Jesus Christ: Favor to you, and peace from God our Father, and from our Lord Jesus Christ.
2 Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima.
We give thanks to God at all times for you all, making mention of you in our prayers;
3 Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Yesu Kristo.
incessantly remembering your work of faith, and labor of love, and patience of hope in our Lord Jesus Christ, in the sight of God, even our Father;
4 Ndugu zetu mpendwao na Mungu, kwa kuwa tunajua kwamba Mungu amewachagua,
knowing, brethren, beloved of God, your election:
5 kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu.
for our gospel came not to you in word only, but also with power, and with the Holy Spirit, and with much assurance: as you know what sort of men we were among you.
6 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu.
And you became imitators of us, and of the Lord, having embraced the word in much affliction, with joy of the Holy Spirit.
7 Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya.
So that you become patterns to all who believe, in Macedonia and Achaia.
8 Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake.
Besides, from you the word of the Lord has resounded, not only in Macedonia and Achaia; but also in every place your faith in God is spread abroad, so that we have no need to speak anything.
9 Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli
For they themselves publish concerning us, what sort of entrance we had to you, and how you turned to God from idols, to serve the living and true God;
10 na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.
and to wait for his Son from heaven, whom he has raised from the dead, even Jesus, who delivers us from the wrath which is to come.

< 1 Wathesalonike 1 >