< 1 Samweli 8 >
1 Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli.
撒母耳年紀老邁,就立他兒子作以色列的士師。
2 Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba.
長子名叫約珥,次子名叫亞比亞;他們在別是巴作士師。
3 Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.
他兒子不行他的道,貪圖財利,收受賄賂,屈枉正直。
4 Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama.
以色列的長老都聚集,來到拉瑪見撒母耳,
5 Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.”
對他說:「你年紀老邁了,你兒子不行你的道。現在求你為我們立一個王治理我們,像列國一樣。」
6 Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba Bwana.
撒母耳不喜悅他們說「立一個王治理我們」,他就禱告耶和華。
7 Naye Bwana akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanakuambia. Si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao.
耶和華對撒母耳說:「百姓向你說的一切話,你只管依從;因為他們不是厭棄你,乃是厭棄我,不要我作他們的王。
8 Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe.
自從我領他們出埃及到如今,他們常常離棄我,事奉別神。現在他們向你所行的,是照他們素來所行的。
9 Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.”
故此你要依從他們的話,只是當警戒他們,告訴他們將來那王怎樣管轄他們。」
10 Samweli akawaambia wale watu waliokuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya Bwana.
撒母耳將耶和華的話都傳給求他立王的百姓,說:
11 Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.
「管轄你們的王必這樣行:他必派你們的兒子為他趕車、跟馬,奔走在車前;
12 Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake.
又派他們作千夫長、五十夫長,為他耕種田地,收割莊稼,打造軍器和車上的器械;
13 Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji.
必取你們的女兒為他製造香膏,做飯烤餅;
14 Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake.
也必取你們最好的田地、葡萄園、橄欖園賜給他的臣僕。
15 Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake.
你們的糧食和葡萄園所出的,他必取十分之一給他的太監和臣僕;
16 Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike, na ngʼombe wenu walio wazuri sana na punda kwa matumizi yake mwenyewe.
又必取你們的僕人婢女,健壯的少年人和你們的驢,供他的差役。
17 Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake.
你們的羊群他必取十分之一,你們也必作他的僕人。
18 Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye Bwana hatawajibu.”
那時你們必因所選的王哀求耶和華,耶和華卻不應允你們。」
19 Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala.
百姓竟不肯聽撒母耳的話,說:「不然!我們定要一個王治理我們,
20 Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.”
使我們像列國一樣,有王治理我們,統領我們,為我們爭戰。」
21 Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za Bwana.
撒母耳聽見百姓這一切話,就將這話陳明在耶和華面前。
22 Bwana akamjibu, “Wasikilize na uwape mfalme.” Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, “Kila mmoja arudi mjini kwake.”
耶和華對撒母耳說:「你只管依從他們的話,為他們立王。」撒母耳對以色列人說:「你們各歸各城去吧!」