< 1 Samweli 5 >

1 Baada ya Wafilisti kuteka Sanduku la Mungu, walilichukua kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi.
And the Philistines took the ark of God, and brought it from Eben-ezer to Ashdod.
2 Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni.
When the Philistines took the ark of God, they brought it into the house of Dagon, and set it by Dagon.
3 Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
And when they of Ashdod arose early on the morrow, behold, Dagon [had] fallen upon his face to the earth before the ark of the LORD. And they took Dagon, and set him in his place again.
4 Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
And when they arose early on the morrow morning, behold, Dagon had fallen upon his face to the ground before the ark of the LORD: and the head of Dagon and both the palms of his hands [were] cut off upon the threshhold; only [the stump of] Dagon was left to him.
5 Ndiyo sababu mpaka leo makuhani wa Dagoni wala wengine waingiao katika hekalu la Dagoni huko Ashdodi hawakanyagi kizingiti.
Therefore neither the priests of Dagon, nor any that come into Dagon's house, tread on the threshhold of Dagon in Ashdod to this day.
6 Mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.
But the hand of the LORD was heavy upon them of Ashdod, and he destroyed them, and smote them with emerods, [even] Ashdod, and its borders.
7 Watu wa Ashdodi walipoona kile kilichokuwa kikitokea, wakasema, “Sanduku la Mungu wa Israeli kamwe lisikae hapa pamoja na sisi, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya Dagoni mungu wetu.”
And when the men of Ashdod saw that [it was] so, they said, The ark of the God of Israel shall not abide with us: for his hand is severe upon us, and upon Dagon our god.
8 Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kuwauliza, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Mungu wa Israeli?” Wakajibu, “Sanduku la Mungu wa Israeli na liende Gathi.” Basi wakalihamisha Sanduku la Mungu wa Israeli.
They sent therefore, and gathered all the lords of the Philistines to them, and said, What shall we do with the ark of the God of Israel? And they answered, Let the ark of the God of Israel be carried about to Gath. And they carried the ark of the God of Israel [thither].
9 Lakini baada ya kulihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi ya huo mji wa Gathi, akiuweka katika fadhaa kuu. Mungu akawatesa watu wa huo mji, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.
And it was [so], that after they had carried it thither, the hand of the LORD was against the city with a very great destruction: and he smote the men of the city both small and great, and they had emerods in their secret parts.
10 Basi wakapeleka Sanduku la Mungu Ekroni. Wakati Sanduku la Mungu lilipokuwa linaingia Ekroni, watu wa Ekroni walilia wakisema “Wamelileta Sanduku la Mungu wa Israeli kwetu ili kutuua sisi na watu wetu.”
Therefore they sent the ark of God to Ekron. And it came to pass as the ark of God came to Ekron, that the Ekronites cried out, saying, They have brought about the ark of the God of Israel to us, to slay us and our people.
11 Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kusema, “Liondoeni Sanduku la Mungu wa Israeli na lirudishwe mahali pake, la sivyo litatuua sisi na watu wetu.” Kwa kuwa kifo kilikuwa kimeujaza mji hofu; kwani mkono wa Mungu ulikuwa mzito sana juu yake.
So they sent and convened all the lords of the Philistines, and said, Send away the ark of the God of Israel, and let it go again to its own place, that it slay us not, and our people: for there was a deadly destruction throughout all the city; the hand of God was very heavy there.
12 Wale ambao hawakufa walipatwa na majipu, na kilio cha mji kilikwenda juu hadi mbinguni.
And the men that died not, were smitten with the emerods: and the cry of the city went up to heaven.

< 1 Samweli 5 >