< 1 Petro 5 >
1 Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa:
Therefore, I exhort the elders among you, as a fellow elder, and a witness of the sufferings of Meshikha, and who will also share in the glory that will be revealed.
2 lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika.
Shepherd the flock of God which is among you, exercising the oversight, not under compulsion, but voluntarily, as God wants; not for dishonest gain, but willingly;
3 Msijifanye mabwana juu ya wale walio chini ya uangalizi wenu, bali kuweni vielelezo kwa hilo kundi.
neither as lording it over those entrusted to you, but making yourselves examples to the flock.
4 Naye Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu isiyoharibika.
When the chief Shepherd is revealed, you will receive the crown of glory that does not fade away.
5 Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Likewise, you younger ones, be subject to the elder. Yes, all of you clothe yourselves with humility, towards one another; for God resists the proud, but gives grace to the humble.
6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.
Humble yourselves therefore under the mighty hand of God, that he may exalt you in due time;
7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.
casting all your worries on him, because he cares for you.
8 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza.
Be sober and self-controlled. Be watchful. Your adversary the devil, walks around like a roaring lion, seeking whom he may devour.
9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.
Withstand him steadfast in your faith, knowing that your brothers who are in the world are undergoing the same sufferings.
10 Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha. (aiōnios )
And the God of all grace, who called you to his eternal glory in Meshikha, after you have suffered a little while, will himself restore, confirm, strengthen and establish you. (aiōnios )
11 Uweza una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
To him be the power forever. Amen. (aiōn )
12 Kwa msaada wa Silvano, ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
Through Silvanus, our faithful brother, as I consider him, I have written to you briefly, exhorting, and testifying that this is the true grace of God. Stand firm in it.
13 Kanisa lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu.
She who is in Babylon, chosen together with you, greets you; and so does Markos, my son.
14 Salimianeni kwa busu la upendo. Amani iwe nanyi nyote mlio katika Kristo.
Greet one another with a kiss of love. Peace be to you all who are in Meshikha.