< 1 Petro 5 >

1 Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa:
我想鼓励你们中的长老们。我也是一名长老,是基督受难的见证人,那即将到来的荣耀将有我的一份。
2 lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika.
看好上帝赐予你、让你照顾的羊群,不是因为你被迫这样做,而是因为高兴,因为上帝希望你这样做。你要心甘情愿地这样做,而不是想从中获利。
3 Msijifanye mabwana juu ya wale walio chini ya uangalizi wenu, bali kuweni vielelezo kwa hilo kundi.
不要狂妄自大,凌驾于被你照顾之人之上,而是要成为羊群的榜样。
4 Naye Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu isiyoharibika.
当牧长显现之时,你将获得永不衰败的荣耀冠冕。
5 Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
年轻人,按照长老的吩咐去做。事实上,你们所有人都应该谦卑地为彼此服务,因为“上帝反对骄傲之人,偏爱谦卑之人。”
6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.
在上帝强大的手面前要谦卑,这样他就会在适当的时候把你举起来。
7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.
把你所有的忧愁都交给他,因为他在乎你。
8 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza.
要负责任,保持警惕。魔鬼是你的敌人,像咆哮的狮子一样四处游荡,寻找可以吞噬之人。
9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.
要坚定地反对他,相信上帝。记住,世界各地其他和你一样的信徒,也正在经历类似的问题。
10 Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha. (aiōnios g166)
你受苦一小段时间之后,那所有恩典的上帝,那曾召唤你、让你与基督一样走进其永恒荣耀的上帝,就会亲自将你恢复,支持你,给你力量,并给你一个坚实的基础。 (aiōnios g166)
11 Uweza una yeye milele na milele. Amen. (aiōn g165)
愿力量永永远远属于他!阿门。 (aiōn g165)
12 Kwa msaada wa Silvano, ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
我是在西尔瓦努斯的帮助下,将这封信寄给你们,他是我值得信赖的兄弟。通过我所写的这些文字,我想鼓励你们并见证这是上帝真正的恩典。要坚定地站在上帝的恩典中!
13 Kanisa lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu.
在 “巴比伦”这里的信徒,和你一起被选中,向你问候,就像我的儿子马克一样。还有我的儿子马克也问候你们。
14 Salimianeni kwa busu la upendo. Amani iwe nanyi nyote mlio katika Kristo.
以爱的吻互相问候。愿你们所有与基督同在之人都能够平安。

< 1 Petro 5 >