< 1 Petro 1 >

1 Petro, mtume wa Yesu Kristo: Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia.
Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wageni wa utawanyiko, kwa wateule, katika Ponto yote, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia,
2 Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utiifu kwa Yesu Kristo na kunyunyiziwa damu yake: Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi.
kutokana na ufahamu wa Mungu, Baba, kwa kutakaswa na Roho Mtakatifu, kwa utiifu wa Yesu Kristo, na kwa kunyunyuziwa damu yake. Neema iwe kwenu, na amani yenu iongezeke.
3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake kuu ametuzaa sisi mara ya pili katika tumaini lenye uzima kupitia kwa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu,
Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na abarikiwe. Katika ukuu wa rehema yake, alitupa kuzaliwa upya kwa ujasiri wa urithi kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka katika wafu,
4 ili tuupate urithi usioharibika, usio na uchafu, ule usionyauka: uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,
kwa urithi usioangamia, hautakua na uchafu wala kupungua. Umehihifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu.
5 ninyi ambao mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani, hadi uje ule wokovu ulio tayari kufunuliwa nyakati za mwisho.
Kwa uwezo wa Mungu mnalindwa kupitia imani kwa wokovu ambao upo tayari kufunuliwa katika nyakati za mwisho.
6 Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi.
Furahini katika hili, ingawaje sasa ni lazima kwenu kujisikia huzuni katika majaribu ya aina mbalimbali.
7 Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa.
Hii, ni kwa sababu imani yenu iweze kujaribiwa, imani ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ambayo inapotea katika moto ambao hujaribu imani yenu. Hii hutokea ili imani yenu ipate kuzaa sifa, utukufu, na heshima katika ufunuo wa Yesu Kristo.
8 Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka.
Hamjamuona yeye, lakini mnampenda. Hamumuoni sasa, lakini mnaamini katika yeye na mna furaha isiyoweza kuelezeka kwa furaha ambayo imejawa na utukufu.
9 Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.
Sasa mnapokea wenyewe matokeo ya imani yenu, wokovu wa nafsi zenu.
10 Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa,
Manabii walitafuta na kuuliza kwa umakini kuhusu wokovu huu, kuhusu neema ambayo ingekuwa yenu.
11 wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.
Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata.
12 Walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali waliwahudumia ninyi, waliponena kuhusu mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya.
Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.
13 Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Yesu Kristo atakapodhihirishwa.
Kwa hiyo fungeni viuno vya akili zenu. Muwe watulivu katika fikra zenu. Muwe na ujasiri mkamilifu katika neema ambayo italetwa kwenu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo.
14 Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga.
Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu.
15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.
Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.
16 Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
Kwa kuwa imeandkwa, “Iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu.”
17 Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.
Na kama mkiita “Baba” yule ahukumuye kwa haki kulingana na kazi ya kila mtu, tumia muda wa safari yako katika unyenyekevu.
18 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu,
Mnafahamu kwamba haikuwa kwa fedha au dhahabu - vitu vinavyoharibika- ambavyo mmekombolewa kutoka kwenye tabia zenu za ujinga ambazo mlijifunza kutoka kwa baba zenu.
19 bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.
Lakini mmekombolewa kwa damu ya heshima ya Kristo, kama ya kondoo asiye na hila wala doa.
20 Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.
Kristo alichaguliwa kabla ya misingi ya dunia, lakini sasa siku hizi za mwisho, amefunuliwa kwenu.
21 Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.
Mnamwamini Mungu kupitia yeye, ambaye Mungu alimfufua toka kwa wafu na ambaye alimpa utukufu ili kwamba imani yenu na ujasiri uwe katika Mungu.
22 Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Mmefanya nafsi zenu kuwa safi kwa utii wa ile kweli, kwa dhumuni la pendo la kidugu lililo na unyofu, hivyo pendaneni kwa bidii toka moyoni.
23 Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. (aiōn g165)
Mmekwisha zaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, lakini kutoka katika mbegu isiyoharibika, kupitia uzima na neno la Mungu lililosalia. (aiōn g165)
24 Maana, “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni; majani hunyauka na maua huanguka,
Kwa maana “miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
25 lakini neno la Bwana ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu. (aiōn g165)
lakini neno la Bwana hubakia milele.” Huu ni ujumbe ambao ulitangazwa kama injili kwenu. (aiōn g165)

< 1 Petro 1 >