< 1 Wafalme 5 >

1 Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Solomoni ametiwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Solomoni, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi.
Hiramu mfalme wa Tiro aliwatuma watumishi wake kwa Sulemani kwa kuwa alisikia kuwa walikuwa wamemtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alimpenda Daudi.
2 Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:
Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, akisema,
3 “Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wake, hadi Bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake.
“Unajua kuwa Daudi baba yangu hakujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake kwa sababu ya vile vita vilivyomzunguka, kwa kuwa wakati wa uhai wake BWANA alikuwa akiweka maadui wake chini ya nyayo za miguu yake.
4 Lakini sasa Bwana Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa.
Lakini sasa BWANA amenipa mimi pumziko toka pande zote. Hakuna maadui wala majanga.
5 Kwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Daudi, wakati aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’
Kwa hiyo ninakusudia kujenga hekalu kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyosema kwa Daudi baba yangu, akisema, 'Mwanao ambaye nitamweka kwenye kiti chako cha enzi mahali pako, ndiye atakayenijengea hekalu kwa jina langu.'
6 “Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitawalipa watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.”
Kwa hiyo sasa amuru wakate mierezi kutoka Lebanoni kwa ajili yangu. Watumishi wangu wataungana na watumishi wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watumishi wako ili kwamba upate malipo mazuri kwa kila kitu utakchokubali kukifanya. Kwa kuwa unajua kuwa hakuna mtu mioingoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni.”
7 Hiramu aliposikia ujumbe wa Solomoni, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”
Hiramu aliposikia maneno ya Sulemani, akafurahi sana akasema, “BWANA na abarikiwe leo, ambaye amempa Daudi mwana wa hekiima juu ya kundi hili kubwa.”
8 Hiramu akatuma neno kwa Solomoni: “Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari.
Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, “Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji.
9 Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.”
Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu.”
10 Kwa njia hii Hiramu akampa Solomoni miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji,
Kwa hiyo Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo alihitaji.
11 naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,000 za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000. Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka.
Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano kwa ajili ya chakula cha watumishi wake na kori ishirii za mafuta safi. Sulemani akavitoa hivi kwa Hiramu mwaka baad ya mwaka.
12 Bwana akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba.
BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyokuwa amemwahidi. Kulikuwa na amani kati ya Hiramu na Sulemani na wote wawili wakafanya agano.
13 Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote.
Mfalme Sulemani akaandaa wafanya kazi kutoka Israeli yote. Idadi ya watenda kazi walioandaliwa ilikuwa wanaume elfu thelathini.
14 Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu 10,000 kwa mwezi, hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja na miezi miwili nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa.
Aliwatuma kwenda Lebanoni, aliwatuma kwa zamu ya watu elfu kumi kila mwezi. Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani. Adoniramu ndiye aliyekuwa msimamizi wa watenda kazi.
15 Solomoni alikuwa na wachukuzi wa mizigo 70,000 na wachonga mawe 80,000 huko vilimani,
Sulemani alikuwa na watu elfu sabini waliokuwa wabeba mizigo na watu elfu themanini wa kukata mawe milimani,
16 pamoja na wasimamizi 3,300 ambao walisimamia kazi hiyo na kuwaongoza wafanyakazi.
zaidi ya hao, walikuwepo maakida 3, 300 ambao pia waliokuwa wakiisimamia hiyo kazi.
17 Kwa amri ya mfalme walitoa kwenye machimbo ya mawe, mawe makubwa, yaliyo bora kwa kujengea msingi wa nyumba yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu.
Kwa amri ya mfalme walileta mawe makubwa ya thamani kwa ajili ya kulaza kwenye msingi wa hekalu.
18 Mafundi wa Solomoni, wa Hiramu na watu wa Gebali walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.
Kwa hiyo wajenzi wa Sulemani na wajenzi wa Hiramu na Wagebaliti walifanya kazi ya kukata na kuandaa mbao kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.

< 1 Wafalme 5 >