< 1 Wafalme 4 >

1 Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote.
Mfalme Sulemani alikuwa mfalme wa Israeli.
2 Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;
Hawa ndio waliokuwa wakuu wake: Azaria mwana wa Sadoki alikuwa kuhani.
3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;
Elihorefu na Ahiya mwana wa Shisha, walikuwa makatibu. Yehoshafati mwana wa Ahilui alikuwa mwandishi.
4 Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani;
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa jeshi. Sadoki na Abiatahari walikuwa makuhani.
5 Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;
Azaria mwana wa Natahani ndiye aliyekuwa juu ya hawa maakida. Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani na rafiki wa mfalme.
6 Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.
Ahishari alikuwa mkuu wa nyumba. Adoniramu mwana wa Abda alikuwa mkuu wa watenda kazi.
7 Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.
Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli yote, ambao walitoa chakula kwa mfalme na watu wake wote. Kila mtu alikuwa na zamu ya kuhudumia kwa mwezi mmoja katka mwaka.
8 Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;
Majina yao yalikuwa ndiyo haya: Beni Huri, Kutoka milima ya Efraimu;
9 Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;
Beni Dekeri wa Makazi, Shaalibimu, Bethi Shemeshi, na Elonbethi Hanaan;
10 Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);
Beni Hesed, wa Arubothi (kutoka kwake alipatikana Sokohi na nchi yote ya Hefa);
11 Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);
Ben Abinadabu, wa wilaya yote ya Dori (alikuwa na Tafathi binti wa mfalme ambaye alikuwa mke wake);
12 Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;
Baana mwana wa Ahiludi, wa Taanaki na Megido, na Beth Shani iliyo upande mwingine wa Zarethani chini ya Yezreel, Kutoak Bethi Shani mpaka Abeli Mehola iliyo upande mwingine wa Jokimeamu;
13 Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);
Ben Geberi, ya Ramothi Gileadi (kutoka kwake tunapata miji ya Yairi mwana wa Manase, ambayo iko Gileadi, na mkoa wa Arigobu ulikuwa wake, ambao uko Bashani, miji sitini yenye maboma na yenye nguzo za malango ya shaba);
14 Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;
Ahinadabu mwana wa Ido, wa Mahanaimu;
15 Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);
Ahimaazi, wa Naftali (ambaye pia alimwoa Basimathi binti wa Sulemani kuwa mke wake);
16 Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;
Baana mwana wa Hushai, ya Asherina Bealothi;
17 Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;
Yehoshafati mwana wa Paruha, kwa Isakari;
18 Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;
Shimei mwana wa Ela, wa Benjamini;
19 Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.
na Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, ambayo ni nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na Ogi mfalme wa Bashani, na yeye ndiye akida pekee aliyekuwa katika nchi hiyo.
20 Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.
Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa baharini. Nao walikuwa wakila na kunywa na kufurahi.
21 Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.
Suleimani alitawala utawala wote kutoka mtoni hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri. Wote walileta kodi na walimtumikia Sulemani katika siku za maisha yake yote.
22 Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida.
Mahitaji ya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano,
23 Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana.
makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.
24 Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote.
Kwa kuwa utawala wake ulikuwa zaidi ya nchi yote upande huu wa mto, kutoka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa mto, naye alikuwa na amani pande zote.
25 Wakati wa maisha ya Solomoni Yuda na Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba, wakaishi salama kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake.
Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini y a mzabibu wake na chini ya mtini wake, kutoka Dani mpaka Beerisheba, siku zote za Sulemani.
26 Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 ya magari ya vita, na farasi 12,000.
Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa ajili ya magari yake, na wapanda farasi elfu kumi na mbili.
27 Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua.
Na maakida walileta chakula kwa Sulemani na kwa wale walioketi kwenye meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake. Walihakikisha hakuna kinachopungua.
28 Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.
Na pia walileta kwenye eneo husika shayiri na majani kwa ajili ya wale farasi wa magari na kwa wale farasi wa mbio kila mmoja alileta kadri alivyoweza.
29 Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari.
Mungu alimpa Sulemani hekima kubwa, ufahamu, na upana wa uelewa kama mchanga wa baharini.
30 Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri.
Hekima ya Sulemani ilizidi hekima ya watu wote wa mashariki na hekima yote ya Misri.
31 Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka.
Alikuwa na hekima kuliko wanaume wote - kuliko Ethani Muezrahi, Hemani, Kaliko, na Darda, wana wa Maholi - na habari zake zikaenea hadi kwenye mataifa yote yaliyomzunguka.
32 Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005.
Aliongea mithali elfu tatu na idadi ya nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.
33 Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki.
Aliifafanua mimea, kuanzia mierezi iliyoko Lebanoni hadi Hisopo imeao ukutani. Aliwafafanua wanyama, ndege, vitu vitambaavyo na samaki. Watu walikuja kutoka mataifa yote kuisikia hekima ya Sulemani.
34 Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.
Watu walikuja kutoka falme zote za duniani waliosikia juu ya hekima yake.

< 1 Wafalme 4 >