< 1 Wafalme 2 >

1 Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Solomoni agizo.
Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema,
2 Akasema, “Mimi ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jionyeshe kuwa mwanaume,
“Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amari zake,
3 shika lile Bwana Mungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote uendako,
maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwamngalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,
4 ili kwamba Bwana aweze kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako wakiangalia sana wanavyoishi, na kama wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli.’
na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, 'kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.
5 “Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake.
Wewe pia wajua kile Yoabu mwana wa Seruya alichonifanyia, na kile alichowafnyia majemedari wa majeshi y a Israeli, kwa Abina mwana wa Neri, na kwa Amasa mwana wa Yetheri, ambaye alimwua. Alimwaga damu vitani wakati wa amani na kuiweka ile damu kwenye mshipi uliokuwa kiunoni mwake na kwenye vile viatu miguuni mwake.
6 Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani. (Sheol h7585)
Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani. (Sheol h7585)
7 “Lakini uwaonyeshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.
Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.
8 “Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa Gera, Mbenyamini kutoka Bahurimu, ambaye alinilaani kwa laana kali siku niliyokwenda Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani, nilimwapia kwa Bwana: ‘Sitakuua kwa upanga!’
Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,'
9 Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.” (Sheol h7585)
Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu. Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini.” (Sheol h7585)
10 Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi.
Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
11 Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
12 Kwa hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana.
Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
13 Basi Adoniya, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Solomoni. Bathsheba akamuuliza, “Je, umekuja kwa amani?” Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.”
Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, “Je, unakuja kwa amani?” Naye akajiibu. “kwa amani.”
14 Kisha akaongeza, “Ninalo jambo la kukuambia.” Akajibu, “Waweza kulisema.”
Kisha akasema, “Nina jambo la kukuambia.” Naye akajibu, “Sema.”
15 Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Bwana.
Adoniya amesema, “Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.
16 Sasa ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.” Bathsheba akasema, “Waweza kuliomba.”
Sasa nina ombi moja kwako. Usinikatalie.”Bathisheba akamwambia, “Sema.”
17 Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Solomoni, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”
Naye akamwambia, “Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu.”
18 Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.”
Bathisheba akamwambia, “Vyema sana, nitamwambia mfalme”
19 Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adoniya, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono wake wa kuume.
Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme.
20 Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo ombi moja dogo la kukuomba; usinikatalie.” Mfalme akajibu, “Omba, mama yangu; sitakukatalia.”
Ndipo alipomwambia, “Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie.” Mfalme, akamjibu, “Mama omba kwa kuwa sitakukatalia.”
21 Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adoniya.”
Naya akamwambia, “Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake.”
22 Mfalme Solomoni akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya!”
Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini unamwombea Adoniya huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? - au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?”
23 Mfalme Solomoni akaapa kwa Bwana, akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila huruma, ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili!
Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, “Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adoniya hajayasema haya kinyume na maisha yake.
24 Basi sasa, hakika kama Bwana aishivyo, yeye ambaye ameniimarisha salama kwenye kiti cha ufalme cha Daudi baba yangu, naye amenipa ufalme wa kudumu kama alivyoahidi, Adoniya atauawa leo!”
Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo.”
25 Hivyo Mfalme Solomoni akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akampiga Adoniya akafa.
Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.
26 Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la Bwana Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.”
Kisha akamwambia Abiathari kuhani, “Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. unastahili kufa, lakini sitakua sasa hivi, kwa sababu ulilbeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata tabu.”
27 Hivyo Solomoni akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Bwana, akilitimiza neno la Bwana alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.
Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.
28 Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa amefanya shauri baya na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la Bwana na kushika pembe za madhabahu.
Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adoniya, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu.
29 Mfalme Solomoni akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la Bwana naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Solomoni akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!”
Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda, ukamwue.”
30 Ndipo Benaya akaingia kwenye hema la Bwana na kumwambia Yoabu, “Mfalme anasema, ‘Toka nje!’” Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.” Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo Yoabu alivyonijibu.”
Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, “Mfalme anasema utoke hemani.” Yoabu akamjibu, “Hapana, Nitafia hapa,” Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, “Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu,”
31 Kisha mfalme akamwamuru Benaya, “Fanya kama asemavyo. Muue na kumzika, ili uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu aliyoimwaga.
Naye mfalme akamwambia, “Kafanye kama alivyosema. Muue na ukamzike, ili kwamba uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu.
32 Bwana atamlipiza kwa ajili ya damu aliyoimwaga, kwa sababu pasipo Daudi baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda, walikuwa watu wazuri na wanyofu kuliko yeye.
BWANA na amrudishie damu yake kichwani kwake, kwa sababu aliwaua wanaume wawili wasio na hatia na wema kuliko yeye na akawaua kwa upanga, Abineri mwana wa Neri, Jemedari wa Jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Jetheri, jemedari wa jeshi la Yuda, bila baba yangu Daudi kujua.
33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Bwana milele.”
Kwa hiyo damu yao na imrudie Yoabu kichwani pake na kwenye vichwa vya uzao wake milele na milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, na nyumba yake, na kwenye kiti chake cha enzi, kuwe na amani ya kudumu kutoka kwa BWANA.”
34 Basi Benaya mwana wa Yehoyada akakwea, akampiga na kumuua Yoabu, naye akazikwa katika nchi yake mwenyewe katika jangwa.
Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani.
35 Mfalme akamweka Benaya mwana wa Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari.
Mfalme akamwinua Benaya mwana wa Yehoyada kuwa juu ya jeshi badala yake, na akamweka Sadoki kuhani kwenye nafasi ya Abiatahari.
36 Kisha mfalme akatuma ujumbe kwa Shimei na kumwambia, “Ujijengee nyumba huko Yerusalemu uishi huko, lakini usiende mahali pengine popote.
Kisha Mfalme akatuma watu kumwita Shimei, na akamwambia, “Kajijengee nyumba kwa ajili yako kule Yerusalemu na ushi huko, na usitoke nje ya Huo mji na kwenda mahali pengine.
37 Siku utakayoondoka kuvuka Bonde la Kidroni, uwe na hakika utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.”
Kwa kuwa siku utakayoenda mahali pengine, na kupita bonde la Kidroni, ujue kwa hakika kuwa utakufa. Damu yako itakuwa juu ya kichwa chako.”
38 Shimei akamjibu mfalme, “Ulilolisema ni jema. Mtumishi wako atatenda kama bwana wangu mfalme alivyosema.” Naye Shimei akakaa Yerusalemu kwa muda mrefu.
Kwa hiyo Shimei akamwambia mfalme, “Unachosema ni chema. Kama vike mfalme bwana wangu alivyosema, ndivyo ambavyo mtumishi wako atakavyofanya.” Kwa hiyo Shimei akaishi Yerusalemu kwa miaka mingi.
39 Lakini baada ya miaka mitatu, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi, naye Shimei akaambiwa, “Watumwa wako wako Gathi.”
Lakiini mwishoni mwa mwaka wa tatu, watumishi wawili wa Shimei wakakimbilia kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Kwa hiyo wakamwambia Shimei, wakisema, “Tazama, watumishi wako wameenda Gathi,”
40 Kwa ajili ya hili, Shimei akatandika punda wake, akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumwa wake. Basi Shimei akaondoka na kuwarudisha watumwa wake kutoka Gathi.
Kisha Shimei akainuka, akapanda punda wake akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumishi wake. Akaenda na akawaleta watumishi wake toka Gathi.
41 Solomoni alipoambiwa kuwa Shimei ametoka Yerusalemu na kwenda Gathi na amekwisha kurudi,
Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi na amerudi,
42 mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Bwana na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’
mfalme akatuma wito kwa Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapisha kwa BWANA na kushuhudia kwako, nikisema, 'Tambua kuwa siku utakayotoka kwenda nje na kwenda mahali popote, hakika utakufa'? Na ukaniambia kuwa unachosema ni chema.'
43 Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Bwana na kutii amri niliyokupa?”
Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako kwa BWANA na amri niliyokupa?”
44 Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako makosa uliyomtendea baba yangu Daudi. Sasa Bwana atakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda.
Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako maovu yote uliyofanya kwa baba yangu Daudi. Kwa hiyo BWANA atakurudishia maovu yako kichwani pako.
45 Lakini Mfalme Solomoni atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha Daudi kitakuwa imara mbele za Bwana milele.”
Lakini Sulemani atabarikiwa na enzi ya Daudi itaimarika mbele ya BWANA milele.”
46 Kisha mfalme akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akatoka nje, akampiga Shimei na kumuua. Sasa ufalme ukawa umeimarika kikamilifu mikononi mwa Solomoni.
Kwa hiyo mfalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada kwenda kumwua Shimei. Kwa hiyo ule utawala ulikuwa mwema kwa mkono wa Sulemain.

< 1 Wafalme 2 >