< 1 Wafalme 15 >

1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda,
La dix-huitième année du roi Jéroboam, fils de Nébat, Abijam commença à régner sur Juda.
2 naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
Il régna trois ans à Jérusalem. Sa mère s'appelait Maaca, et était fille d'Abishalom.
3 Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.
Il marcha dans tous les péchés que son père avait commis avant lui; et son cœur ne fut point intègre envers l'Éternel son Dieu, comme le cœur de David, son père.
4 Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara.
Mais, pour l'amour de David, l'Éternel son Dieu lui donna une lampe dans Jérusalem, suscitant son fils après lui et laissant subsister Jérusalem;
5 Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.
Parce que David avait fait ce qui est droit devant l'Éternel, et que, pendant toute sa vie, il ne s'était point détourné de tout ce qu'il lui avait commandé, excepté dans l'affaire d'Urie, le Héthien.
6 Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.
Et il y avait eu guerre entre Roboam et Jéroboam, tout le temps de leur vie.
7 Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
Le reste des actions d'Abijam et tout ce qu'il fit, cela n'est-il pas écrit au livre des Chroniques des rois de Juda? Il y eut aussi guerre entre Abijam et Jéroboam.
8 Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake.
Et Abijam s'endormit avec ses pères, et on l'ensevelit dans la cité de David; et Asa, son fils, régna à sa place.
9 Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda,
La vingtième année de Jéroboam, roi d'Israël, Asa commença à régner sur Juda;
10 naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
Et il régna quarante et un ans à Jérusalem. Sa mère s'appelait Maaca, et elle était fille d'Abishalom.
11 Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa Bwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake.
Et Asa fit ce qui est droit aux yeux de l'Éternel, comme David, son père.
12 Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.
Il chassa du pays les prostitués, et il ôta toutes les idoles que ses pères avaient faites.
13 Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye wadhifa wake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
Et même il destitua de son rang sa mère, Maaca, qui avait fait une idole pour Ashéra. Et Asa abattit son idole et la brûla au torrent de Cédron.
14 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote.
Les hauts lieux ne furent point ôtés; néanmoins, le cœur d'Asa fut intègre envers l'Éternel tout le long de ses jours,
15 Akaleta ndani ya Hekalu la Bwana fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.
Et il remit dans la maison de l'Éternel les choses qui avaient été consacrées par son père, avec ce qu'il lui avait aussi consacré, l'argent, l'or et les ustensiles.
16 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.
Or il y eut guerre entre Asa et Baesha, roi d'Israël, tout le temps de leur vie.
17 Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Et Baesha, roi d'Israël, monta contre Juda, et il bâtit Rama, afin de ne laisser sortir ni entrer aucun homme pour Asa, roi de Juda.
18 Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu la Bwana na za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu, aliyekuwa akitawala Dameski.
Alors Asa prit tout l'argent et l'or demeuré dans les trésors de l'Éternel et les trésors de la maison royale, et les remit à ses serviteurs; et le roi Asa les envoya vers Ben-Hadad, fils de Tabrimon, fils de Hezjon, roi de Syrie, qui habitait à Damas, pour lui dire:
19 “Akasema na pawepo mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”
Il y a alliance entre moi et toi, comme entre mon père et ton père; voici je t'envoie un présent en argent et en or; va, romps ton alliance avec Baesha, roi d'Israël, afin qu'il se retire de moi.
20 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali.
Et Ben-Hadad écouta le roi Asa, et il envoya les capitaines de ses armées contre les villes d'Israël; et il frappa Ijjon, Dan, Abel-Beth-Maaca et tout Kinnéroth, avec tout le pays de Nephthali.
21 Wakati Baasha aliposikia hili, akaacha kuijenga Rama na akaenda kuishi Tirsa.
Et aussitôt que Baesha l'eut appris, il cessa de bâtir Rama; et il resta à Thirtsa.
22 Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.
Alors le roi Asa fit publier par tout Juda, que tous, sans exempter personne, eussent à emporter les pierres et le bois de Rama, que Baesha faisait bâtir; et le roi Asa en bâtit Guéba de Benjamin, et Mitspa.
23 Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.
Quant à tout le reste des actions d'Asa et tous ses exploits, et tout ce qu'il fit, et les villes qu'il bâtit, cela n'est-il pas écrit au livre des Chroniques des rois de Juda? Seulement, au temps de sa vieillesse, il fut malade des pieds.
24 Kisha Asa akalala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake.
Et Asa s'endormit avec ses pères, et il fut enseveli avec eux dans la cité de David, son père; et Josaphat, son fils, régna à sa place.
25 Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili.
Nadab, fils de Jéroboam, avait commencé à régner sur Israël la seconde année d'Asa, roi de Juda, et il régna deux ans sur Israël.
26 Akafanya maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.
Il fit ce qui est mal aux yeux de l'Éternel; et il marcha dans la voie de son père et dans le péché par lequel il avait fait pécher Israël.
27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira.
Et Baesha, fils d'Achija, de la maison d'Issacar, conspira contre lui, et le frappa à Guibbéthon qui est aux Philistins, lorsque Nadab et tout Israël assiégeaient Guibbéthon.
28 Baasha akamuua Nadabu katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Baesha le fit donc mourir, la troisième année d'Asa, roi de Juda; et il régna à sa place.
29 Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu yeyote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la Bwana lililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,
Et dès qu'il fut roi, il frappa toute la maison de Jéroboam; et il ne laissa à Jéroboam aucune âme vivante qu'il n'exterminât, selon la parole que l'Éternel avait prononcée par son serviteur Achija, de Silo,
30 kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli.
A cause des péchés que Jéroboam avait commis et fait commettre à Israël, en provoquant l'Éternel, le Dieu d'Israël.
31 Kwa matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyofanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
Le reste des actions de Nadab, et tout ce qu'il fit, cela n'est-il pas écrit au livre des Chroniques des rois d'Israël?
32 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao.
Or, il y eut guerre entre Asa et Baesha, roi d'Israël, tout le temps de leur vie.
33 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirsa, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne.
La troisième année d'Asa, roi de Juda, Baesha, fils d'Achija, commença à régner sur tout Israël, à Thirtsa; il régna vingt-quatre ans.
34 Akatenda maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.
Il fit ce qui est mal aux yeux de l'Éternel; et il marcha dans la voie de Jéroboam et dans le péché par lequel il avait fait pécher Israël.

< 1 Wafalme 15 >