< 1 Wakorintho 2 >
1 Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu.
When I came to you, brothers, I did not come with eloquence of speech or wisdom as I proclaimed hidden truths about God.
2 Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa.
For I decided to know nothing when I was among you except Jesus Christ, and him crucified.
3 Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana.
And I was with you in weakness, and in fear, and in much trembling.
4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho
And my message and my proclamation were not with persuasive words of wisdom. Instead, they were with the demonstration of the Spirit and of power,
5 ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.
so that your faith might not be in the wisdom of humans, but in the power of God.
6 Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. (aiōn )
Now we do speak wisdom among the mature, but not the wisdom of this world, or of the rulers of this age, who are passing away. (aiōn )
7 Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. (aiōn )
Instead, we speak God's wisdom in hidden truth, the hidden wisdom that God predestined before the ages for our glory. (aiōn )
8 Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu. (aiōn )
None of the rulers of this age understood it, for if they had understood it, they would not have crucified the Lord of glory. (aiōn )
9 Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna jicho limepata kuona, wala sikio limepata kusikia, wala hayakuingia moyoni wowote, yale Mungu amewaandalia wale wampendao”:
But as it is written, “Things that no eye has seen, no ear has heard, no mind has imagined, the things that God has prepared for those who love him.”
10 Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu.
These are the things that God has revealed to us through the Spirit. For the Spirit searches everything, even the deep things of God.
11 Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
For who knows a person's thoughts except the spirit of the person in him? So also, no one knows the deep things of God except the Spirit of God.
12 Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure.
But we did not receive the spirit of the world, but the Spirit who is from God, so that we might know the things freely given to us by God.
13 Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa maneno ya kiroho.
We speak about these things in words that man's wisdom cannot teach, but which the Spirit teaches us. The Spirit interprets spiritual words with spiritual wisdom.
14 Mtu ambaye hana Roho hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni.
The unspiritual person does not receive the things that belong to the Spirit of God, for they are foolishness to him. He cannot know them because they are spiritually discerned.
15 Mtu wa kiroho hubainisha mambo yote, lakini yeye mwenyewe habainishwi na mtu yeyote.
The one who is spiritual judges all things, but he is not subject to the judgment of others.
16 “Kwa maana ni nani aliyefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumfundisha?” Lakini sisi tunayo mawazo ya Kristo.
“For who can know the mind of the Lord, that he can instruct him?” But we have the mind of Christ.