< 1 Wakorintho 11 >

1 Igeni mfano wangu, kama ninavyouiga mfano wa Kristo.
Mwilondai nene, kutya nene kanikamfuata Kristu.
2 Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa.
Henu ni kabhafifu kwa ndabha ya fhela kamkani khomboka mghakamuili mayhopolelu kutya kumuletai kwa muenga.
3 Napenda mfahamu kwamba kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu.
Basi nilonda mmanyai ya kuwa Kristu ndo kichwa kya kila mwanagosi, ni muene mwanagosi ndo kichwa cha bhanadala, ni ya kuya K'yara ndo mutu wa Kristu.
4 Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
Khila mwanagosi yais'oma au yaipisya unabii ikayelai afuniki mutu wa muene akakiaibisha mutu wa muene.
5 Naye kila mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake, kwani ni sawa na yeye aliyenyoa nywele.
Kakiyele kila mwanadala yais'oma au kupisya unabii hali mutu wa muene kikayelai wazi akakiaibisha mutu wa muene. Kwa mana so sawasawa ni kutya kaakasibhu.
6 Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
Ikayelai kutya mwandala alafunikalepi mutu wa muene, na adumulibhwai njuili sya muene siyelai sifupi. Mana ukayela soni mwanadala kudumula njuili sya muene au kukasibhwa, basi afunikai mutu wa muene.
7 Haimpasi mwanaume kufunika kichwa chake kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume.
Kwani ikampasalepi mwanagosi kufunika mutu wa muene, kwa ndabha muene ndo mfuano ni utukufu wa k'yara. Kakiyele mwanadala ndo utukufu wa mwanagosi.
8 Kwa maana mwanaume hakutoka kwa mwanamke, bali mwanamke alitoka kwa mwanaume.
Mana mwanagosi atokene hee ni mwanadala. Bali mwanadala atokhene ni mwanagosi.
9 Wala mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume.
Wala mwanagosi abhombibhu hee kwajia ya mwanadala. Bali mwanadala abhombibhu kwajia ya mwanagosi.
10 Kwa sababu hii na kwa sababu ya malaika, inampasa mwanamke awe na ishara ya mamlaka juu yake.
Eye ndo ndabha mwanadala ipasibhwa kuya ni ishala ya mamlaka juu ya mutu wa muene, kwa ndabha ya malaika.
11 Lakini katika Bwana, mwanamke hajitegemei pasipo mwanaume na mwanaume hajitegemei pasipo mwanamke.
Hata efu, kup'etela Bwana, mwana ndala ayehe muene pasipo mwanangosi, au mwanangosi pasipo mwanadala.
12 Kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanaume, vivyo hivyo mwanaume huzaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vyatoka kwa Mungu.
Mana kutya kabhele mwanadala ahomili kwa mwanagosi, khela khela umwanagosi ahomili kwa mwanadala. Ni fhenu fyoa fihomela kwa K'yara.
13 Hukumuni ninyi wenyewe: Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu bila kufunika kichwa chake?
Mjihukumuayi mwayhomo: Ko! ndosahihi mwanadala an's'omai K'yara hali mutu wa muene ukayelai wazi?
14 Je, maumbile ya asili hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu?
Ko hata asili ya yumuene ikabhafundisya lepi ya ndabha mwanagosi akayela ni njuili sitali ndo soni kwa muene?
15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu ili kumfunika.
Ko asili ikabhafundisya lepi ya ndabha mwanadala akayela ni njuili sitali ndo utukufu kwa muene? Mana apelibhu sela njuili sitali kutya nghobho sya muene.
16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Kakiyele ikayela munu yuyuoa yhola ilondaa kubishana juu ya ele, tete tuyehee ni namna yhenge, wala makanisa gha K'yara.
17 Basi katika maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu, kwa sababu mkutanikapo si kwa ajili ya faida bali kwa hasara.
Kup'etela maagizo ghaghifuatila, nene nikabhasifuhee. Mana pamwikusanyika, si kwa faida bali kwa hasala.
18 Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo.
Mana kuanza, ni p'eleka ya kuya pamwikusanika mu kanisa, kuyenimigawanyiko kati ya yhomo, ni kwa sehemu niamini.
19 Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili kuonyesha ni nani anayekubaliwa na Mungu.
Kwa mana lazima iyelai misuguano kati ya yhomo, ili ndabha bhala bhakubalili bhamanyinikai kwayhomo.
20 Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula,
Kwa mana pamwibhonenela, kamwila so kyakulya kya Bwana.
21 kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa.
Pamwilya, kila mmonga ilya kyakulya kya muene yumuene kabula ya bhamana bhalili lepi. hata ni oyho ayehe ni njala, ni oyho agalili.
22 Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha!
Ko iyelepi nyumba yakulelela au kunywelela? Ko mkaliza ku kanisa la K'yara ni kubhafezehesha yabhadulili fhenu? Nijobha kiki kwa muenga? Nibhasifilai? Nilabhasifila lepi kup'etela ele!
23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate,
Mana nayhopholili kuhomela kwa Bwana khela kanibhapelili muenga ya kuwa Bwana Yesu, pakilu bhola paasalitibhu, atolili n'kate.
24 naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”
Baada wa kuushukulu, audumuili ni kujobha, “Obho ndo mbhele wanene, wauyele kajia ya yhomo. Mkhetainaa kwa kunikhombhoka nene.”
25 Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
Na ni naa kabhele atolili kikhombi baada ya kulya, ni kujobha, “Kikhombi ekhe ndo agano lipya kup'etela muasi wa yhoni. Mkhetai na mala nyingi kila pamwinywa kwa kunikhombhoka nene.”
26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo.
Kwakila muda pamwilya n'kate obho ni kunywelela kikombi, mkaitangasya umauti wa Bwana mpaka paihidai.
27 Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana.
Kwa elu, kila yailayi n'kate au kukinywelela kikhombi ekhu kya Bwana kakibelili kuya, alaya ajipelili hatia y mbhele ni muasi wa Bwana.
28 Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe.
Munu akajihojilepi yumwene hosi, ni kabhele alyai n'kate, ni kukinywelela kikhombi.
29 Kwa maana mtu yeyote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, hula na kunywa hukumu juu yake mwenyewe.
Mana yailya ni kunywa bila kupambanula mbhele, ilya ni kunywa hukumu ya muene yumuene.
30 Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa.
Eye ndo ndabha bhanu bhingi kati yayhomo ni bhagonjwa ni bhazaifu, ni baazi yhinu bhafuile.
31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa.
Kakiyele tukachunguzimai tabhene tulahukumibhwa hee.
32 Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
Ila patihukumlibhwa ni Bwana, tikhelebhukila ili tusihidi kuhukumlibhwa pamonga ni dunia.
33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane.
Kwa elu, kaka ni dada bhayangu pamwibhonanila mbhuesyai kulya, mlendanai.
34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.
Munu akayelai ni alyai kunyumba kwa muene, ili ndabha pamwibhonana pamonga isiyi kihukumu. Ni kuhusu mambo ghamana ghamwayandiki, nilabhajobhela pamwihidai.

< 1 Wakorintho 11 >