< 1 Nyakati 8 >
1 Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara,
2 Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
Noha, na Rafa.
3 Wana wa Bela walikuwa: Adari, Gera, Abihudi,
Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi,
4 Abishua, Naamani, Ahoa,
Abishau, Naamani, Ahoa,
5 Gera, Shefufani na Huramu.
Gera, Shefufani, na Huramu.
6 Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati:
7 Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi.
8 Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.
Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara.
9 Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu,
kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu,
10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.
Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao.
11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu.
12 Wana wa Elpaali walikuwa: Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka),
Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi ( ambao walijenga Ono na Lod pamoja na vijiji vilivyozunguka.)
13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya koo walizoishi Aijalon, Ambao waliwaondoa wakazi wa Gati.
14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi,
Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Jeremothi,
15 Zebadia, Aradi, Ederi,
Zebadia, Aradi, Eda,
16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
Mikaeli, Ishipa, na Joha.
17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,
Elipaa alikuwa na wana hawa: Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba,
18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
Ishimerai, Izilia, na Yobabu.
Shimei alikuwa na wana hawa: Yokimu, Zikri, Zabdi,
20 Elienai, Silethai, Elieli,
Elienai, Zilletai, Elieli,
21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
Adaia, Beraia, na Shimrati.
22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,
Shashaki alikuwa na wana hawa: Ishipani, Eba, Elieli,
23 Abdoni, Zikri, Hanani,
Abdoni, Zikri, Hanani,
24 Hanania, Elamu, Anthothiya,
Hanania, Elamu, Antotoja,
26 Shamsherai, Sheharia, Athalia,
Yerohamu alikuwa na wana hawa: Shamsherai, Sheharia, Atli,
27 Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
Yaareshia, Elija, na Zikri.
28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
Hawa walikuwa vichwa vya koo na viongozi walioishi Yerusalemu.
29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka.
Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni.
30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
Uzao wake wa kwanza alikuwa Abdoni, akafatia Zuri, Kishi, Baali, Nadab,
32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.
33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
34 Yonathani akamzaa: Merib-Baali, naye Merib-Baali akamzaa Mika.
Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika.
35 Wana wa Mika walikuwa: Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi.
36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.
Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao: Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.
Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli.
39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa: Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti.
Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu.
40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150. Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.