< 1 Nyakati 7 >

1 Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
以萨迦的儿子是陀拉、普瓦、雅述、伸 ,共四人。
2 Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
陀拉的儿子是乌西、利法雅、耶勒、雅买、易伯散、示母利,都是陀拉的族长,是大能的勇士。到大卫年间,他们的人数共有二万二千六百名。
3 Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.
乌西的儿子是伊斯拉希;伊斯拉希的儿子是米迦勒、俄巴底亚、约珥、伊示雅,共五人,都是族长。
4 Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
他们所率领的,按着宗族出战的军队,共有三万六千人,因为他们的妻和子众多。
5 Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.
他们的族弟兄在以萨迦各族中都是大能的勇士,按着家谱计算共有八万七千人。
6 Wana watatu wa Benyamini walikuwa: Bela, Bekeri na Yediaeli.
便雅悯的儿子是比拉、比结、耶叠,共三人。
7 Wana wa Bela walikuwa: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.
比拉的儿子是以斯本、乌西、乌薛、耶利摩、以利,共五人,都是族长,是大能的勇士。按着家谱计算,他们的子孙共有二万二千零三十四人。
8 Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.
比结的儿子是细米拉、约阿施、以利以谢、以利约乃、暗利、耶利摩、亚比雅、亚拿突、亚拉篾。这都是比结的儿子。
9 Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.
他们都是族长,是大能的勇士。按着家谱计算,他们的子孙共有二万零二百人。
10 Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.
耶叠的儿子是比勒罕;比勒罕的儿子是耶乌施、便雅悯、以忽、基拿拿、细坦、他施、亚希沙哈。
11 Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
这都是耶叠的儿子,都是族长,是大能的勇士;他们的子孙能上阵打仗的,共有一万七千二百人。
12 Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
还有以珥的儿子书品、户品,并亚黑的儿子户伸。
13 Wana wa Naftali walikuwa: Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.
拿弗他利的儿子是雅薛、沽尼、耶色、沙龙。这都是辟拉的子孙。
14 Wana wa Manase walikuwa: Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi.
玛拿西的儿子亚斯列是他妾亚兰人所生的,又生了基列之父玛吉。
15 Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
玛吉娶的妻是户品、书品的妹子,名叫玛迦。玛拿西的次子名叫西罗非哈;西罗非哈但有几个女儿。
16 Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
玛吉的妻玛迦生了一个儿子,起名叫毗利施。毗利施的兄弟名叫示利施;示利施的儿子是乌兰和利金。
17 Mwana wa Ulamu alikuwa: Bedani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
乌兰的儿子是比但。这都是基列的子孙。基列是玛吉的儿子,玛吉是玛拿西的儿子。
18 Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.
基列的妹子哈摩利吉生了伊施荷、亚比以谢、玛拉。(
19 Wana wa Shemida walikuwa: Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.
示米大的儿子是亚现、示剑、利克希、阿尼安。)
20 Wana wa Efraimu walikuwa: Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi,
以法莲的儿子是书提拉;书提拉的儿子是比列;比列的儿子是他哈;他哈的儿子是以拉大;以拉大的儿子是他哈;
21 Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao.
他哈的儿子是撒拔;撒拔的儿子是书提拉。以法莲又生以谢、以列;这二人因为下去夺取迦特人的牲畜,被本地的迦特人杀了。
22 Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji.
他们的父亲以法莲为他们悲哀了多日,他的弟兄都来安慰他。
23 Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.
以法莲与妻同房,他妻就怀孕生了一子,以法莲因为家里遭祸,就给这儿子起名叫比利亚。
24 Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.
他的女儿名叫舍伊拉,就是建筑上伯·和 、下伯·和 与乌羡·舍伊拉的。
25 Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
比利阿的儿子是利法和利悉。利悉的儿子是他拉;他拉的儿子是他罕;
26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama,
他罕的儿子是拉但;拉但的儿子是亚米忽;亚米忽的儿子是以利沙玛;
27 Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.
以利沙玛的儿子是嫩;嫩的儿子是约书亚。
28 Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake.
以法莲人的地业和住处是伯特利与其村庄;东边拿兰,西边基色与其村庄;示剑与其村庄,直到迦萨与其村庄;
29 Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.
还有靠近玛拿西人的境界,伯·善与其村庄;他纳与其村庄;米吉多与其村庄;多珥与其村庄。以色列儿子约瑟的子孙住在这些地方。
30 Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
亚设的儿子是音拿、亦施瓦、亦施韦、比利亚,还有他们的妹子西 拉。
31 Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
比利亚的儿子是希别、玛结;玛结是比撒威的父亲。
32 Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
希别生雅弗勒、朔默、何坦,和他们的妹子书雅。
33 Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
雅弗勒的儿子是巴萨、宾哈、亚施法。这都是雅弗勒的儿子。
34 Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
朔默的儿子是亚希、罗迦、耶户巴、亚兰。
35 Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
朔默兄弟希连的儿子是琐法、音那、示利斯、亚抹。
36 Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,
琐法的儿子是书亚、哈尼弗、书阿勒、比利、音拉、
37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.
比悉、河得、珊玛、施沙、益兰、比拉。
38 Wana wa Yetheri walikuwa: Yefune, Pispa na Ara.
益帖的儿子是耶孚尼、毗斯巴、亚拉。
39 Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia.
乌拉的儿子是亚拉、汉尼业、利写。
40 Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.
这都是亚设的子孙,都是族长,是精壮大能的勇士,也是首领中的头目,按着家谱计算,他们的子孙能出战的共有二万六千人。

< 1 Nyakati 7 >