< 1 Nyakati 4 >

1 Wana wa Yuda walikuwa: Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.
בני יהודה פרץ חצרון וכרמי וחור ושובל׃
2 Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.
וראיה בן שובל הוליד את יחת ויחת הליד את אחומי ואת להד אלה משפחות הצרעתי׃
3 Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi.
ואלה אבי עיטם יזרעאל וישמא וידבש ושם אחותם הצללפוני׃
4 Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.
ופנואל אבי גדר ועזר אבי חושה אלה בני חור בכור אפרתה אבי בית לחם׃
5 Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
ולאשחור אבי תקוע היו שתי נשים חלאה ונערה׃
6 Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.
ותלד לו נערה את אחזם ואת חפר ואת תימני ואת האחשתרי אלה בני נערה׃
7 Wana wa Hela walikuwa: Serethi, Sohari, Ethnani,
ובני חלאה צרת יצחר ואתנן׃
8 na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.
וקוץ הוליד את ענוב ואת הצבבה ומשפחות אחרחל בן הרום׃
9 Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.”
ויהי יעבץ נכבד מאחיו ואמו קראה שמו יעבץ לאמר כי ילדתי בעצב׃
10 Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
ויקרא יעבץ לאלהי ישראל לאמר אם ברך תברכני והרבית את גבולי והיתה ידך עמי ועשית מרעה לבלתי עצבי ויבא אלהים את אשר שאל׃
11 Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni.
וכלוב אחי שוחה הוליד את מחיר הוא אבי אשתון׃
12 Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.
ואשתון הוליד את בית רפא ואת פסח ואת תחנה אבי עיר נחש אלה אנשי רכה׃
13 Wana wa Kenazi walikuwa: Othnieli na Seraya. Wana wa Othnieli walikuwa: Hathathi na Meonathai.
ובני קנז עתניאל ושריה ובני עתניאל חתת׃
14 Meonathai akamzaa Ofra. Seraya akamzaa Yoabu, baba wa Ge-Harashimu. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.
ומעונתי הוליד את עפרה ושריה הוליד את יואב אבי גיא חרשים כי חרשים היו׃
15 Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu: Iru, Ela na Naamu. Naye mwana wa Ela alikuwa: Kenazi.
ובני כלב בן יפנה עירו אלה ונעם ובני אלה וקנז׃
16 Wana wa Yahaleleli walikuwa: Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.
ובני יהללאל זיף וזיפה תיריא ואשראל׃
17 Wana wa Ezra walikuwa: Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa.
ובן עזרה יתר ומרד ועפר וילון ותהר את מרים ואת שמי ואת ישבח אבי אשתמע׃
18 Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.
ואשתו היהדיה ילדה את ירד אבי גדור ואת חבר אבי שוכו ואת יקותיאל אבי זנוח ואלה בני בתיה בת פרעה אשר לקח מרד׃
19 Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa: baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.
ובני אשת הודיה אחות נחם אבי קעילה הגרמי ואשתמע המעכתי׃
20 Wana wa Shimoni walikuwa: Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni. Wazao wa Ishi walikuwa: Zohethi na Ben-Zohethi.
ובני שימון אמנון ורנה בן חנן ותולון ובני ישעי זוחת ובן זוחת׃
21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa: Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea,
בני שלה בן יהודה ער אבי לכה ולעדה אבי מרשה ומשפחות בית עבדת הבץ לבית אשבע׃
22 Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.)
ויוקים ואנשי כזבא ויואש ושרף אשר בעלו למואב וישבי לחם והדברים עתיקים׃
23 Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.
המה היוצרים וישבי נטעים וגדרה עם המלך במלאכתו ישבו שם׃
24 Wazao wa Simeoni walikuwa: Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.
בני שמעון נמואל וימין יריב זרח שאול׃
25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.
שלם בנו מבשם בנו משמע בנו׃
26 Wazao wa Mishma walikuwa: Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.
ובני משמע חמואל בנו זכור בנו שמעי בנו׃
27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.
ולשמעי בנים ששה עשר ובנות שש ולאחיו אין בנים רבים וכל משפחתם לא הרבו עד בני יהודה׃
28 Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali,
וישבו בבאר שבע ומולדה וחצר שועל׃
29 Bilha, Esemu, Toladi,
ובבלהה ובעצם ובתולד׃
30 Bethueli, Horma, Siklagi,
ובבתואל ובחרמה ובציקלג׃
31 Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi.
ובבית מרכבות ובחצר סוסים ובבית בראי ובשערים אלה עריהם עד מלך דויד׃
32 Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano:
וחצריהם עיטם ועין רמון ותכן ועשן ערים חמש׃
33 pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.
וכל חצריהם אשר סביבות הערים האלה עד בעל זאת מושבתם והתיחשם להם׃
34 Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,
ומשובב וימלך ויושה בן אמציה׃
35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.
ויואל ויהוא בן יושביה בן שריה בן עשיאל׃
36 Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,
ואליועיני ויעקבה וישוחיה ועשיה ועדיאל וישימאל ובניה׃
37 Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.
וזיזא בן שפעי בן אלון בן ידיה בן שמרי בן שמעיה׃
38 Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana,
אלה הבאים בשמות נשיאים במשפחותם ובית אבותיהם פרצו לרוב׃
39 wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao.
וילכו למבוא גדר עד למזרח הגיא לבקש מרעה לצאנם׃
40 Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.
וימצאו מרעה שמן וטוב והארץ רחבת ידים ושקטת ושלוה כי מן חם הישבים שם לפנים׃
41 Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao.
ויבאו אלה הכתובים בשמות בימי יחזקיהו מלך יהודה ויכו את אהליהם ואת המעינים אשר נמצאו שמה ויחרימם עד היום הזה וישבו תחתיהם כי מרעה לצאנם שם׃
42 Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri.
ומהם מן בני שמעון הלכו להר שעיר אנשים חמש מאות ופלטיה ונעריה ורפיה ועזיאל בני ישעי בראשם׃
43 Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.
ויכו את שארית הפלטה לעמלק וישבו שם עד היום הזה׃

< 1 Nyakati 4 >