< 1 Nyakati 3 >

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
ואלה היו בני דויד אשר נולד לו בחברון הבכור אמנן לאחינעם היזרעאלית שני דניאל לאביגיל הכרמלית׃
2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
השלשי לאבשלום בן מעכה בת תלמי מלך גשור הרביעי אדניה בן חגית׃
3 wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
החמישי שפטיה לאביטל הששי יתרעם לעגלה אשתו׃
4 Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,
ששה נולד לו בחברון וימלך שם שבע שנים וששה חדשים ושלשים ושלוש שנה מלך בירושלם׃
5 nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni.
ואלה נולדו לו בירושלים שמעא ושובב ונתן ושלמה ארבעה לבת שוע בת עמיאל׃
6 Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti,
ויבחר ואלישמע ואליפלט׃
7 Noga, Nefegi, Yafia,
ונגה ונפג ויפיע׃
8 Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.
ואלישמע ואלידע ואליפלט תשעה׃
9 Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.
כל בני דויד מלבד בני פילגשים ותמר אחותם׃
10 Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu, mwanawe huyo alikuwa Abiya, mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati, mwanawe huyo alikuwa Asa,
ובן שלמה רחבעם אביה בנו אסא בנו יהושפט בנו׃
11 mwanawe huyo alikuwa Yehoramu, mwanawe huyo alikuwa Ahazia, mwanawe huyo alikuwa Yoashi,
יורם בנו אחזיהו בנו יואש בנו׃
12 mwanawe huyo alikuwa Amazia, mwanawe huyo alikuwa Azaria, mwanawe huyo alikuwa Yothamu,
אמציהו בנו עזריה בנו יותם בנו׃
13 mwanawe huyo alikuwa Ahazi, mwanawe huyo alikuwa Hezekia, mwanawe huyo alikuwa Manase,
אחז בנו חזקיהו בנו מנשה בנו׃
14 mwanawe huyo alikuwa Amoni na mwanawe huyo alikuwa Yosia.
אמון בנו יאשיהו בנו׃
15 Wana wa Yosia walikuwa: Yohanani mzaliwa wake wa kwanza, Yehoyakimu mwanawe wa pili, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
ובני יאשיהו הבכור יוחנן השני יהויקים השלשי צדקיהו הרביעי שלום׃
16 Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni: Yekonia mwanawe, na Sedekia.
ובני יהויקים יכניה בנו צדקיה בנו׃
17 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka: Shealtieli mwanawe,
ובני יכניה אסר שאלתיאל בנו׃
18 Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
ומלכירם ופדיה ושנאצר יקמיה הושמע ונדביה׃
19 Wana wa Pedaya walikuwa: Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa: Meshulamu na Hanania. Shelomithi alikuwa dada yao.
ובני פדיה זרבבל ושמעי ובן זרבבל משלם וחנניה ושלמית אחותם׃
20 Pia walikuwepo wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.
וחשבה ואהל וברכיה וחסדיה יושב חסד חמש׃
21 Wazao wa Hanania walikuwa: Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
ובן חנניה פלטיה וישעיה בני רפיה בני ארנן בני עבדיה בני שכניה׃
22 Wazao wa Shekania: Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.
ובני שכניה שמעיה ובני שמעיה חטוש ויגאל ובריח ונעריה ושפט ששה׃
23 Wana wa Nearia walikuwa: Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.
ובן נעריה אליועיני וחזקיה ועזריקם שלשה׃
24 Wana wa Elioenai walikuwa: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.
ובני אליועיני הודיוהו ואלישיב ופליה ועקוב ויוחנן ודליה וענני שבעה׃

< 1 Nyakati 3 >