< 1 Nyakati 27 >
1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.
Hii ni orodha ya familia za viongozi wa Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, pamoja na maafisa wa jeshi walio mtumikia mfalme kwa namna tofauti. Kila kikosi cha jeshi kilitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima. Kila kikosi kilikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
2 Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake.
Kwa mwezi wa kwanza wa kikosi alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
3 Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
Alikuwa miongoni mwa uzao wa Perezi na mhusika wa maafisa wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
4 Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Juu ya kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, wa ukoo wa uliotoka kwa Ahoa. Mikilothi alikuwa wa pili kwa cheo. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
5 Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000.
Mkuu wa jeshi wa mwezi wa tatu alikuwa Benaia mwana wa Yehoiada, kuhani na kiongozi. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
6 Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.
Huyu ni Benaia aliye kuwa kiongozi wa wale thelathini na juu ya wale thelathini. Amizabadi mwanae alikuwa katika kikosi chake.
7 Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu. Zebadia mwanae akawa mkuu baada yake. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
8 Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa tano alikuwa Shamihuthi, mzao wa Izra. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
9 Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa sita alikuwa Ira mwana wa Ikeshi, kutoka Tekoa. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
10 Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
11 Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa nane alikuwa Sibekai Mhushathi, kutoka ukoo ulitoka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
12 Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa tisa alikuwa Abi Ezeri Manathothi, kutoka kwa kabila la Benjamini. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
13 Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai kutoka mji wa Netofa, kutoka ukoo ulio toka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
14 Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaia kutoka mji wa Pirathoni, kutoka kabila la Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
15 Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Mkuu kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Helidai kutoka mji wa Netopafa, kutoka ukoo uliotoka kwa Othinieli. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
16 Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa: Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri; kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;
Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli: Kwa kabila la Rubeni, Eliezeri mwana wa Zikri alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Simeoni, Shefatia mwana wa Maka alikuwa kiongozi.
17 kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli; kwa Aroni: Sadoki;
Kwa kabila la Lawi, Hashinia mwana wa Kemueli alikuwa kiongozi, na Zadoki aliongoza uzao wa Aruni.
18 kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi; kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;
Kwa kabila la Yuda, Elihu, mmoja wa kaka zake Daudi, alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Isakari, Omri mwana wa Mikaeli alikuwa kiongozi.
19 kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia; kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;
Kwa kabila la Zebuluni, Ishimaia mwana wa Obadia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Naftali, Yeremothi mwana wa Azirieli alikuwa kiongozi.
20 kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia; kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;
Kwa kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaia alikuwa kiongozi.
21 kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria; kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;
Kwa nusu kabila la Manase lililo Gileadi, Ido mwana wa Zekaria alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Benjamini, Yaasieli mwana wa Abneri alikuwa kiongozi.
22 kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.
Kwa kabila la Dani, Azareli mwana wa Yerohamu alikuwa kiongozi. Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.
23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.
Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.
24 Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.
Yoabu mwana wa Zeruia alianza kuhesabu wanaume, lakini hakumaliza. Gadhabu iliangukia Israeli kwa hili. Hii idadi haikuandikwa kwenye nyakati za mfalme Daudi.
25 Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme. Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.
Azimavethi mwana wa Adieli alikuwa mhusika wa hazina za mfalme. Yonathani mwana wa Uzia alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini, na kwenye minara iliyo imarishwa.
26 Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.
Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi.
27 Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu. Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.
Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi kutoka Shefamu alikuwa juu ya mizabibu na mhifadhi wa mvinyo.
28 Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi. Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.
Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi.
29 Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni. Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.
Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai.
30 Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia. Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.
Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.
31 Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi. Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.
Hawa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
32 Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.
Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri, sababu alikuwa na busara na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakimoni aliwajali watoto wa mfalme.
33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme. Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme.
Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme, na Hushai kutoka watu wa Waariki alikuwa mshauri wake wa siri.
34 Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari. Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.
Nafasi ya Ahithofeli ilichukuliwa na Yehoiada mwana wa Benaia, na Abiathari. Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi la mfalme.