< 1 Nyakati 25 >

1 Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:
David and some of the temple officials (OR, army commanders) chose some of the descendants of Asaph, Heman, and Jeduthun to be in charge of proclaiming God’s messages, and to play harps and lyres and cymbals. This is a list of the men whom they chose for that work:
2 Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa: Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.
From the sons of Asaph they chose Zaccur, Joseph, Nethaniah, and Aserelah. Asaph supervised them. And the king appointed Asaph to proclaim God’s messages.
3 Wana wa Yeduthuni walikuwa sita: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.
From the sons of Jeduthun they chose six men: Gedaliah, Zeri, Jeshaiah, Shimei, Hashabiah, and Mattithiah. Jeduthun supervised them and also proclaimed God’s messages, playing his harp while he thanked and praised Yahweh.
4 Wana wa Hemani walikuwa: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.
From the sons of Heman, who was one of the king’s prophets, they chose Bukkiah, Mattaniah, Uzziel, Shubael, Jerimoth, Hananiah, Hanani, Eliathah, Giddalti, Romamti-Ezer, Joshbekashah, Mallothi, Hothir, and Mahazioth.
5 Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.
God promised to cause Heman to be strong, so altogether, God have him 14 sons and three daughters.
6 Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.
All those men were supervised by their fathers while they played music in the temple of Yahweh. They played cymbals, lyres, and harps. And their fathers—Asaph, Jeduthun and Heman—were supervised by the king.
7 Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288.
Those men and their relatives were all trained and skilled for playing musical instruments in the temple. That was their work for Yahweh. Including their relatives, there were 288 of them.
8 Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.
All of them, including ones who were young and those who were old, cast lots to determine what work they would do.
9 Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12
From the family of Asaph, the first ones selected were Joseph and 12 of his sons and relatives.
10 Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Gedaliah and 12 of his sons and relatives were selected.
11 ya nne ikamwangukia Isri, // wanawe na jamaa zake, 12
Next, Zaccur and 12 of his sons and relatives were selected.
12 ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Nethaniah and 12 of his sons and relatives were selected.
13 ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Bukkiah and 12 of his sons and relatives were selected.
14 ya saba ikamwangukia Yesarela, // wanawe na jamaa zake, 12
Next, Jesarelah and 12 of his sons and relatives were selected.
15 ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Jeshaiah and 12 of his sons and relatives were selected.
16 ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Mattaniah and 12 of his sons and relatives were selected.
17 ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Shimei and 12 of his sons and relatives were selected.
18 ya kumi na moja ikamwangukia Azareli, // wanawe na jamaa zake, 12
Next, Azarel and 12 of his sons and relatives were selected.
19 ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Hashabiah and 12 of his sons and relatives were selected.
20 ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Shubael and 12 of his sons and relatives were selected.
21 ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Mattithiah and 12 of his sons and relatives were selected.
22 ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Jerimoth and 12 of his sons and relatives were selected.
23 Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Hananiah and 12 of his sons and relatives were selected.
24 ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Joshbekashah and 12 of his sons and relatives were selected.
25 ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Hanani and 12 of his sons and relatives were selected.
26 ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Mallothi and 12 of his sons and relatives were selected.
27 ya ishirini ikamwangukia Eliatha, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Eliathah and 12 of his sons and relatives were selected.
28 ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Hothir and 12 of his sons and relatives were selected.
29 ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Giddalti and 12 of his sons and relatives were selected.
30 ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 12
Next, Mahazioth and 12 of his sons and relatives were selected.
31 ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.
Next, Romamti-Ezer and 12 of his sons and relatives were selected.

< 1 Nyakati 25 >