< 1 Nyakati 24 >

1 Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.
Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwahiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.
3 Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
Daudi pamoja na Zadoki, uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, uzao wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi yao ya kazi kama makuhani.
4 Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.
Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.
5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.
Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.
6 Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
7 Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu, ya pili Yedaya,
Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
8 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu,
ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
9 ya tano Malkiya, ya sita Miyamini,
ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
10 ya saba Hakosi, ya nane Abiya,
ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
11 ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania,
ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
12 ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu,
ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
13 ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu,
ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
14 ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri,
ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
15 ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi,
ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
16 ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Yehezkeli,
ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
17 ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli,
ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
18 ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.
ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.
19 Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.
20 Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki: Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli; kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.
Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
21 Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe: Ishia alikuwa wa kwanza.
Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
22 Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi, kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.
Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
23 Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
24 Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika; kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.
Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
25 Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia; na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.
Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
26 Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.
Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
27 Wana wa Merari: kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.
Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
28 Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
29 Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi: alikuwa Yerameeli.
Wana wa Kishi: Yerameli
30 Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi. Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao.
wana wa Mushi: Mahli, Eda, na yerimothi. Walikuwa walawi, walio orodheshwa na familia zao.
31 Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.
Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa katika nyumba za baba zao na kila wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.

< 1 Nyakati 24 >