< 1 Nyakati 23 >
1 Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.
Daudi alipo kuwa mzee na kukaribia mwisho wa maisha yake, alimfanya Sulemani mwanae mfalme juu ya Israeli.
2 Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.
Aliwakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, na makuhani na Walawi.
3 Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000.
Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa. Idadi ya elfu thelathini na nane.
4 Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi,
Kwa hawa, elfu ishirini na nne walikuwa kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, na elfu sita walikuwa maaskari na waamuzi.
5 na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”
Elfu nne walikuwa walinzi wa lango, na elfu nne walikuwa wamsifu Yahweh na vyombo nilivyo vitengeneza vya kusifu.” Daudi akasema.
6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
Akawatenganisha kwenye vikundi kulingana na wana wa Levi: Gerishoni, Kohathi, na Merari.
7 Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
Kwa koo za uzao wa Gerishoni, kulilkuwa na Ladani na Shimei.
8 Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
Palikuwa na watatu wa wana wa Ladani: Yehieli kiongozi, Zethami, na Yoeli.
9 Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi, Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.
Palikuwa na watatu wa wana wa Shimei: Shelomothi, Hazieli, na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa koo ya Ladani.
10 Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.
Palikuwa na wanne wa wana wa Shimei: Yahathi, Ziza, Yeushi, na Beria.
11 Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.
Yahathi alikuwa mkubwa, Ziza wapili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi, hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja na kupangiwa kazi sawa.
12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi: Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
13 Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.
Hawa walikuwa wana wa Amramu: Aruni na Musa. Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.
14 Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.
Lakini kwa Musa mtu wa Mungu, wana wake walihesabiwa kuwa Walawi.
15 Wana wa Mose walikuwa: Gershomu na Eliezeri.
Wana wa Musa walikuwa Gerishomu na Eliezeri.
16 Wazao wa Gershomu: Shebueli alikuwa wa kwanza.
Uzao wa Gerishomu ulikuwa Shebueli mkubwa.
17 Wazao wa Eliezeri: Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
Uzao wa Eliezeri alikuwa Rehabia. Eliezeri hakuwa na wana wengine, lakini Rehabia alikuwa na uzao mkubwa.
18 Wana wa Ishari: Shelomithi alikuwa wa kwanza.
Mwana wa Izihari alikuwa Shelomithi kiongonzi.
19 Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.
Uzao wa Hebroni ulikuwa Yeria, mkubwa, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
20 Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili.
Wana wa Uzieli walikuwa Mika mkubwa, na Ishia wapili.
21 Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Wana wa Mahli walikuwa: Eleazari na Kishi.
Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Wana wa Mahili walikuwa Eleazari na Kishi.
22 Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
Eleazari alikufa bila mtoto wa kiume. Alikuwa na mabinti tu. Wana wa Kishi waliwaoa.
23 Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.
Wana wa Mushi watatu walikuwa Mahili, Ederi, na Yeremothi.
24 Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana.
Hawa walikuwa uzao wa Lawi kuligana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo zilizo fanya kazi katika nyumba ya Yahweh, kutoka miaka ishirini na zaidi.
25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele,
Kwa kuwa Daudi alisema, “Yahweh, Mungu wa Israeli, amewapa pumziko watu wake. Anafanya makao yake Yerusalemu milele.
26 Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.”
Walawi hawataitaji kubeba hema la kuabuadia na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake.”
27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.
Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa, miaka ishirini na kuendelea.
28 Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.
Wajibu wao ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh. Walikuwa washughulikie nyuani, vyumbani, utakasaji wa vitu vyote vya Yahweh, na kazi zingine katika utumishi wa nyumba ya Mungu.
29 Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa.
Pia walishughulikia mkate wa uwepo, unga safi wa mbegu za sadaka, maandazi ya siotiwa chachu, sadaka za ngano, sadaka ziliochanganywa na mafuta, na vipimo vyote vya idadi n a ukubwa wa vitu.
30 Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni
Pia walisimama kila asubui kumshukuru na kumsifu Yahweh. Pia walifanya hivi jioni
31 na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.
na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh, siku ya Sabato na sherehe za mwezi mpya na siku za maakuli. Idadi iliyo pangwa, iliyo tolewa kwa amri, ilipaswa kuwa mbele ya Yahweh.
32 Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.
Walikuwa viongozi wa hema la kukutania, patakatifu, na kuwasaidia ndugu zao wa uzao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh.