< 1 Nyakati 22 >
1 Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya Bwana Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”
Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.”
2 Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu.
Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.
3 Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika.
Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,
4 Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.
na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta mboa nyingi za mierezi kwa Daudi azihesabu.)
5 Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya Bwana inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.
Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.
6 Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana, Mungu wa Israeli.
Akaagiza Sulemani mwanae kuitwa na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.
7 Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu.
Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.
8 Lakini neno hili la Bwana likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu.
Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, 'Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hauta jenga nyumba kwa jina langu, kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.
9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake.
Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.
10 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’
Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli.
11 “Sasa, mwanangu, Bwana awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya Bwana Mungu wako, kama alivyosema utafanya.
Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.
12 Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako.
Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.
13 Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.
Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika.
14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.
Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100, 000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.
15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi
Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, maseremala, wanaume wenye ujuzi mbali mbali,
16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”
wenye uwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na nishati. Hivyo anza kufanya kazi, na Yahweh awe nawe.
17 Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe.
Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,
18 Akawaambia, “Je, Bwana Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya Bwana na watu wake.
“Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.
19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Bwana Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Bwana.”
Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.