< 1 Nyakati 20 >
1 Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.
Ikaja kuwa wakati wa mvua, kipindi wafalme uenda vitani, Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kusikitisha nchi ya Waamoni. Alienda na kuteka Raba. Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu alishambulia Raba na kuishinda.
2 Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu, nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo.
Daudi alichukuwa taji la mfalme wao kichwani mwake, na akagundua linauzito wa talanta moja ya dhahabu, na ndani yake kulikuwa na mawe ya thamani. Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi, na akaleta mali nyingi za mji.
3 Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.
Aliwaleta watu walio kuwa ndani ya mji na kuwalazimisha wafanye kazi kwa msumeno na jembe na shoka. Daudi aliwataka watu wote wa mji kufanya kazi hii. Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu.
4 Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai, nao Wafilisti wakashindwa.
Ilikuwa baada ya haya kukawa na pambano huko Gezeri na Wafilisti. Sibekai Mhushathi akamua Sipai, mmoja wa uzao wa Refaimu, na wa Filisti wakazidiwa.
5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.
Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.
6 Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.
Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu.
7 Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.
Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.
8 Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.
Hawa walikuwa uzao wa Refaimu wa Gathi, na waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa wanajeshi wake.