< 1 Nyakati 2 >
1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,
2 Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
3 Wana wa Yuda walikuwa: Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
4 Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
5 Wana wa Peresi walikuwa: Hesroni na Hamuli.
6 Wana wa Zera walikuwa: Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
7 Mwana wa Karmi alikuwa: Akari, ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
8 Mwana wa Ethani alikuwa: Azariya.
9 Wana wa Hesroni walikuwa: Yerameeli, Ramu na Kalebu.
10 Ramu alimzaa Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11 Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi,
12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
13 Yese akawazaa Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,
14 wa nne Nethaneli, wa tano Radai,
15 wa sita Osemu, na wa saba Daudi.
16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.
17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.
18 Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni.
19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri.
20 Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.
22 Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi.
23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
24 Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa: Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.
26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa: Maasi, Yamini na Ekeri.
28 Wana wa Onamu walikuwa: Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa: Nadabu na Abishuri.
29 Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.
30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31 Apaimu akamzaa: Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani. Sheshani akamzaa Alai.
32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa: Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33 Wana wa Yonathani walikuwa: Pelethi na Zaza. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.
34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu. Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha.
35 Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
36 Atai akamzaa Nathani, Nathani akamzaa Zabadi,
37 Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi,
38 Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria,
39 Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa,
40 Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu,
41 Shalumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elishama.
42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa: Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43 Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema.
44 Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.
45 Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
46 Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47 Wana wa Yadai walikuwa: Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48 Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana.
49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.
50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa: Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,
51 Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa: Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,
53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
54 Wazao wa Salma walikuwa: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori,
55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.