< 1 Nyakati 18 >
1 Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka utawala wa Wafilisti.
Baada ya haya Daudi akawashambulia Wafilisti na kuwashinda. Alichukuwa Gathi na vijiji vyake katika utawala wa Wafilisti.
2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.
Kisha akamshinda Moabu, na Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakamlipa ushuru maalumu.
3 Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati.
Daudi kisha akamshinda Hadadezeri, mfalme wa Zoba huko Hamathi, wakati Hadadezeri alipo kuwa akisafiri kuimarisha utawala wake kwa Mto wa Frati.
4 Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.
Daudi akateka magari ya farasi elfu, wanaume wa farasi elfu saba, na wanajeshi wa miguu elfu ishirini. Daudi aliwajeruhi farasi wote wagari, lakini akahifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.
5 Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao.
Waaramia wa Damasko walipo kuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Zoba, Daudi aliua wanaume elfu ishirini na mbili wa Kiaramia.
6 Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. Bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.
Kisha Daudi akaweka vikosi huko Aramu ya Damasko, na Waaramia wakawa watumishi wake na wakamletea ushuru maalaumu. Yahweh alimpatia Daudi ushindi popote alipoenda.
7 Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu.
Daudi alichukua ngao za dhahabu zilizo kuwa kwa watumishi wa Hadadezeri na kuleta Yerusalemu.
8 Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.
Kutoka Tibhathi na Kuni, miji ya Hadadezeri, Daudi alichukuwa shaba nyingi sana. Ilikuwa shaba hii ambayo baadae Sulemani alifanya saani ya shaba, nguzo, na vifaa vya shaba.
9 Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba,
Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, alipo sikia kuwa Daudi ameshinda majeshi yote ya Hadadezeri mfalme wa Zoba,
10 akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba.
Toi akamtuma Hadoramu mwanae kwa Mfalme Daudi kumsalimia na kumbariki, kwasababu Daudi amepigana na Hadadezeri na kumshinda, na kwasababu Hadadezeri alifanya vita na Toi. Hadoramu alipeleka vifaa vya fedha, dhahabu, na shaba.
11 Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki.
Mfalme Daudi alivitenga hivi vitu kwa ajili ya Yahweh, pamoja na fedha na dhahabu aliyo ibeba kutoka kwa mataifa yote: Edomu, Moabu, watu wa Amoni, Wafilisti, na Waamaleki.
12 Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.
Abishai mwana wa Zeruia akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.
13 Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.
Alieka vikosi huko Edomu, na Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi. Yahweh alimpa Daudi ushindi pote alipoenda.
14 Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote.
Daudi alitawala Israeli yote, na alitenda haki na utaua kwa watu wote.
15 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu;
Yoabu mwana wa Zeruia walikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mtunza kumbukumbu.
16 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Shausha alikuwa mwandishi;
Zadoki mwana wa Ahitubi na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Shavisha alikuwa mwandishi.
17 naye Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme.
Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwangalizi wa Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wakuu wa mfalme.