< 1 Nyakati 17 >
1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la Bwana liko ndani ya hema.”
Ikawa baada ya mfalme kuwa katika nyumba yake, akasema kwa Nathani yule nabii, “Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema.”
2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.”
Kisha Nathani akasema kwa Daudi, Nenda, fanya yalio moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yupo nawe.”
3 Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema:
Lakini usiku huo neno la Mungu lilimjia Nathani, nakusema,
4 “Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo.
“Nenda umwambie Daudi mtumishi wangu, 'Hivi ndivyo Yahweh asemavyo: Hautanijengea nyumba ya kuishi.
5 Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine.
Kwa kuwa sijaishi katika nyumba toka ile siku niliyo ileta Israeli hadi leo. Badala yake, nimeishi ndani ya hema, hema la kukusanyikia, sehemu mbali mbali.
6 Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’
Katika sehemu zote nilizo enda na Israeli, niliwai kusema lolote kwa viongozi wa Israeli niliyo wachagua kuwa chunga watu wangu, kwa kusema, “Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierezi?””
7 “Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli.
“Kisha sasa, mwambie mtumishi wangu Daudi, 'Hili ndilo Yahweh wa majeshi anasema: Nilikuchugua kutoka malishoni, kufuata kondoo, ilikwamba uwe mtawala wa watu wangu Waisraeli.
8 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.
Nimekuwa nawe pote ulipo enda na nimewakata maadui zako wote, na na nitakufanyia jina, kama jina la wakuu wa dunia.
9 Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni,
Nitachagua sehemu ya watu wangu Israeli na nitawapanda hapo, iliwaishi sehemu yao na wasisumbuke tena. Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya mwanzo,
10 na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. “‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba Bwana atakujengea nyumba:
kama walivyo kuwa wakifanya toka siku zile nilipo waamuru waamuzi kuwa juu ya watu wangu Waisraeli. Kisha nitawatiisha maadui zako wote. Zaidi sana nina kwambia kwamba mimi, Yahweh, nitakujengea nyumba.
11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake.
Itakuja kuwa hapo siku zako zitapo timia za wewe kwenda kwa baba zako, nitainua uzao wako baada yako, na mmoja wa uzao wako nitaimarisha ufalme wake.
12 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele.
Yeye atanijengea nyumba, na nitaimarisha kiti chake cha enzi milele.
13 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia.
Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana wangu. Sitaondoa uwaminifu wa Agano langu kwake, kama nilivyo ondoa kwa Sauli, aliye tawala kabla yako.
14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’”
Nitamweka juu ya nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.”
15 Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.
Nathani akanena haya kwa Daudi na kumtaarifu, na akamwambia kuhusu maono yote.
16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema: “Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?
Kisha Daudi mfalme akaenda ndani na kuketi mbele za Yahweh; akasema, “Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?
17 Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee Bwana Mungu.
Hili lilikuwa jambo dogo machoni pako, Mungu. Umezungumzia familia ya mtumishi wako kwa muda mrefu ujao, na umenionyesha vizazi vijavyo, Yahweh Mungu.
18 “Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako,
Nini zaidi mimi, Daudi, niseme? Umemheshimu mtumishi wako. Umemtambua kwa kipekee mtumishi wako.
19 Ee Bwana Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana.
Yahweh, kwa ajili ya mtumishi wako, na kutimiza kusudi lako, umefanya hili ilikudhihirisha matendo yako makuu.
20 “Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe.
Yahweh, hakuna aliye kama wewe, na hakuna Mungu zaidi yako, kama tulivyo sikia mara zote.
21 Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Ni taifa gani duniani kama watu wako Israeli, ambaye wewe, Mungu, uliwaokoa kutoka Misri iliwawe watu wako, kujifanyia jina lako kwa matendo makuu na yahajabu? Uliondoa mataifa mbele za watu wako, uliye waokoa kutoka Misri.
22 Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana Mungu, umekuwa Mungu wao.
Ulifanya Israeli watu wako milele, na wewe, Yahweh, ukawa Mungu wao.
23 “Sasa basi, Bwana ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi,
Hivyo sasa, Yahweh, ile ahadi uliyo iweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake itimizwe milele. Fanya kama ulivyo nena.
24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.
Jina lako na litukuzwe milele na kuwa kuu, ili watu waseme, 'Yahweh wa majeshi ni Mungu wa Israeli,' na nyumba yangu, mimi Daudi, mtumishi wako ikiwa imeimarishwa mbele zako.
25 “Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya.
Kwa kuwa wewe, Mungu wangu, umedhihirisha kwa mtumishi wako utamjengea nyumba. Hiyo ndio sababu, mimi mtumishi wako, nimepata ujasiri wa kuomba kwako.
26 Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri.
Sasa, Yahweh, wewe ni Mungu, na umefanya hii ahadi nzuri kwa mtumishi wako:
27 Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee Bwana, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.”
Sasa imekupendeza kubariki nyumba ya mtumishi wako, iliiendelee milele mbele zako. Wewe, Yahweh, umeibariki, na itabarikiwa milele.”