< 1 Nyakati 14 >

1 Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme.
Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.
2 Naye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.
Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli
3 Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi.
Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.
4 Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni,
Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, nathani, Solimoni,
5 Ibihari, Elishua, Elpeleti,
Ibhari, Elishama, Elpeleti,
6 Noga, Nefegi, Yafia,
Noga, Nefegi, Jafia,
7 Elishama, Beeliada na Elifeleti.
Elishama, Beliada, na Elifeleti.
8 Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.
Sasa tangu Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo nae akaenda nje kinyume nao.
9 Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai,
Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.
10 Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”
Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”
11 Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.
12 Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.
Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.
13 Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde;
Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.
14 hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi.
Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.
15 Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.”
Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”
16 Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.
Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.
17 Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.
Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.

< 1 Nyakati 14 >