< 1 Nyakati 14 >

1 Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme.
וישלח חירם (חורם) מלך צר מלאכים אל דויד ועצי ארזים וחרשי קיר וחרשי עצים--לבנות לו בית
2 Naye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.
וידע דויד כי הכינו יהוה למלך על ישראל כי נשאת למעלה מלכותו בעבור עמו ישראל
3 Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi.
ויקח דויד עוד נשים בירושלם ויולד דויד עוד בנים ובנות
4 Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni,
ואלה שמות הילודים אשר היו לו בירושלם שמוע ושובב נתן ושלמה
5 Ibihari, Elishua, Elpeleti,
ויבחר ואלישוע ואלפלט
6 Noga, Nefegi, Yafia,
ונגה ונפג ויפיע
7 Elishama, Beeliada na Elifeleti.
ואלישמע ובעלידע ואליפלט
8 Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.
וישמעו פלשתים כי נמשח דויד למלך על כל ישראל ויעלו כל פלשתים לבקש את דויד וישמע דויד ויצא לפניהם
9 Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai,
ופלשתים באו ויפשטו בעמק רפאים
10 Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”
וישאל דויד באלהים לאמר--האעלה על פלשתיים (פלשתים) ונתתם בידי ויאמר לו יהוה עלה ונתתים בידך
11 Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
ויעלו בבעל פרצים ויכם שם דויד ויאמר דויד פרץ האלהים את אויבי בידי כפרץ מים על כן קראו שם המקום ההוא--בעל פרצים
12 Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.
ויעזבו שם את אלהיהם ויאמר דויד וישרפו באש
13 Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde;
ויסיפו עוד פלשתים ויפשטו בעמק
14 hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi.
וישאל עוד דויד באלהים ויאמר לו האלהים לא תעלה אחריהם הסב מעליהם ובאת להם ממול הבכאים
15 Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.”
ויהי כשמעך את קול הצעדה בראשי הבכאים--אז תצא במלחמה כי יצא האלהים לפניך להכות את מחנה פלשתים
16 Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.
ויעש דויד כאשר צוהו האלהים ויכו את מחנה פלשתים מגבעון ועד גזרה
17 Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.
ויצא שם דויד בכל הארצות ויהוה נתן את פחדו על כל הגוים

< 1 Nyakati 14 >