< 1 Nyakati 12 >
1 Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani,
Now these [are] they that came to David to Ziklag, while he yet kept himself close because of Saul the son of Kish: and they [were] among the mighty men, helpers of the war.
2 walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):
[They were] armed with bows, and could use both the right hand and the left in [hurling] stones, and [shooting] arrows from a bow, [even] of Saul's brethren of Benjamin.
3 Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi,
The chief [was] Ahiezer, then Joash, the sons of Shemaah the Gibeathite; and Jeziel, and Pelet, the sons of Azmaveth; and Berachah, and Jehu the Antothite,
4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi,
And Ismaiah the Gibeonite, a mighty man among the thirty, and over the thirty; and Jeremiah, and Jahaziel, and Johanan, and Josabad the Gederathite,
5 Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi;
Eluzai, and Jerimoth, and Bealiah, and Shemariah, and Shephatiah the Haruphite,
6 Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora;
Elkanah, and Jesiah, and Azareel, and Joezer, and Jashobeam, the Korhites.
7 Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.
And Joelah, and Zebadiah, the sons of Jeroham of Gedor.
8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.
And of the Gadites there separated themselves to David in the hold in the wilderness men of might, [and] men of war [fit] for the battle, that could handle shield and buckler, whose faces [were like] the faces of lions, and [were] as swift as the roes upon the mountains;
9 Ezeri alikuwa mkuu wao, Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu,
Ezer the first, Obadiah the second, Eliab the third,
10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano,
Mishmannah the fourth, Jeremiah the fifth,
11 Atai wa sita, Elieli wa saba,
Attai the sixth, Eliel the seventh,
12 Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa,
Johanan the eighth, Elzabad the ninth,
13 Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja.
Jeremiah the tenth, Machbanai the eleventh.
14 Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000.
These [were] of the sons of Gad, captains of the host: one of the least [was] over a hundred, and the greatest over a thousand.
15 Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.
These [are] they that went over Jordan in the first month, when it had overflowed all its banks; and they put to flight all [them] of the valleys, [both] towards the east, and towards the west.
16 Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake.
And there came of the children of Benjamin and Judah to the hold to David.
17 Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.”
And David went out to meet them, and answered and said to them, If ye have come peaceably to me to help me, my heart shall be knit to you: but if [ye have come] to betray me to my enemies, seeing [there is] no wrong in my hands, the God of our fathers look [on it], and rebuke [it].
18 Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema: “Sisi tu watu wako, ee Daudi! Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese! Ushindi, naam, ushindi uwe kwako, pia ushindi kwa wale walio upande wako, kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.” Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.
Then the spirit came upon Amasai, [who was] chief of the captains, [and he said], Thine [are we], David, and on thy side, thou son of Jesse: peace, peace [be] to thee, and peace [be] to thy helpers; for thy God helpeth thee. Then David received them, and made them captains of the band.
19 Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”)
And there fell [some] of Manasseh to David, when he came with the Philistines against Saul to battle: but they helped them not: for the lords of the Philistines upon advisement sent him away, saying, He will fall to his master Saul to [the jeopardy of] our heads.
20 Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase.
And as he went to Ziklag, there fell to him of Manasseh, Adnah, and Jozabad, and Jediael, and Michael, and Jozabad, and Elihu, and Zilthai, captains of the thousands that [were] of Manasseh.
21 Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake.
And they helped David against the band [of the rovers]: for they [were] all mighty men of valor, and were captains in the host.
22 Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
For at [that] time day by day there came to David to help him, until [it was] a great host, like the host of God.
23 Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Bwana alivyokuwa amesema:
And these [are] the numbers of the bands [that were] ready armed to the war, [and] came to David to Hebron, to turn the kingdom of Saul to him, according to the word of the LORD.
24 watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.
The children of Judah that bore shield and spear [were] six thousand and eight hundred, ready armed for war.
25 Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.
Of the children of Simeon, mighty men of valor for war, seven thousand and one hundred.
26 Watu wa Lawi walikuwa 4,600,
Of the children of Levi four thousand and six hundred.
27 pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700,
And Jehoiada [was] the leader of the Aaronites, and with him [were] three thousand and seven hundred;
28 na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.
And Zadok, a young man mighty of valor, and of his father's house twenty and two captains.
29 Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo.
And of the children of Benjamin, the kindred of Saul, three thousand: for hitherto the greatest part of them had kept the ward of the house of Saul.
30 Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.
And of the children of Ephraim twenty thousand and eight hundred, mighty men of valor, famous throughout the house of their fathers.
31 Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.
And of the half tribe of Manasseh eighteen thousand, who were expressed by name, to come and make David king.
32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.
And of the children of Issachar, [who were men] that had understanding of the times, to know what Israel ought to do; the heads of them [were] two hundred; and all their brethren [were] at their command.
33 Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.
Of Zebulun, such as went forth to battle, expert in war, with all instruments of war, fifty thousand, who could keep rank: [they were] not of double heart.
34 Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki.
And of Naphtali a thousand captains, and with them with shield and spear thirty and seven thousand.
35 Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita.
And of the Danites expert in war twenty and eight thousand and six hundred.
36 Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita.
And of Asher, such as went forth to battle, expert in war, forty thousand.
37 Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000.
And on the other side of Jordan, of the Reubenites, and the Gadites, and of the half tribe of Manasseh, with all manner of instruments of war for the battle, a hundred and twenty thousand.
38 Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme.
All these men of war, that could keep rank, came with a perfect heart to Hebron, to make David king over all Israel: and all the rest also of Israel [were] of one heart to make David king.
39 Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao.
And there they were with David three days, eating and drinking: for their brethren had prepared for them.
40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.
Moreover, they that were nigh them, [even] to Issachar, and Zebulun, and Naphtali, brought bread on asses, and on camels, and on mules, and on oxen, [and] provision, meal, cakes of figs, and bunches of raisins, and wine, and oil, and oxen, and sheep abundantly: for [there was] joy in Israel.