< 1 Nyakati 11 >
1 Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako.
以色列众人聚集到希伯 见大卫,说:“我们原是你的骨肉。
2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’”
从前扫罗作王的时候,率领以色列人出入的是你;耶和华—你的 神也曾应许你说:‘你必牧养我的民以色列,作以色列的君。’”
3 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.
于是以色列的长老都来到希伯 见大卫王。大卫在希伯 耶和华面前与他们立约,他们就膏大卫作以色列的王,是照耶和华借撒母耳所说的话。
4 Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo
大卫和以色列众人到了耶路撒冷,就是耶布斯;那时耶布斯人住在那里。
5 wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.
耶布斯人对大卫说:“你决不能进这地方。”然而大卫攻取锡安的保障,就是大卫的城。
6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.
大卫说:“谁先攻打耶布斯人,必作首领元帅。”洗鲁雅的儿子约押先上去,就作了元帅。
7 Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi.
大卫住在保障里,所以那保障叫作大卫城。
8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.
大卫又从米罗起,四围建筑城墙,其余的是约押修理。
9 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.
大卫日见强盛,因为万军之耶和华与他同在。
10 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi.
以下记录跟随大卫勇士的首领,就是奋勇帮助他得国、照着耶和华吩咐以色列人的话、与以色列人一同立他作王的。
11 Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi: Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.
大卫勇士的数目记在下面:哈革摩尼的儿子雅朔班,他是军长的统领,一时举枪杀了三百人。
12 Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.
其次是亚合人朵多的儿子以利亚撒,他是三个勇士里的一个。
13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.
他从前与大卫在巴斯·达闵,非利士人聚集要打仗。那里有一块长满大麦的田,众民就在非利士人面前逃跑;
14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.
这勇士便站在那田间击杀非利士人,救护了那田。耶和华使以色列人大获全胜。
15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.
三十个勇士中的三个人下到磐石那里,进了亚杜兰洞见大卫;非利士的军队在利乏音谷安营。
16 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu.
那时大卫在山寨,非利士人的防营在伯利恒。
17 Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!”
大卫渴想,说:“甚愿有人将伯利恒城门旁井里的水打来给我喝!”
18 Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.
这三个勇士就闯过非利士人的营盘,从伯利恒城门旁的井里打水,拿来奉给大卫。他却不肯喝,将水奠在耶和华面前,
19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.
说:“我的 神啊,这三个人冒死去打水,这水好像他们的血一般,我断不敢喝!”如此,大卫不肯喝。这是三个勇士所做的事。
20 Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
约押的兄弟亚比筛是这三个勇士的首领;他举枪杀了三百人,就在三个勇士里得了名。
21 Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.
他在这三个勇士里是最尊贵的,所以作他们的首领;只是不及前三个勇士。
22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
有甲薛勇士耶何耶大的儿子比拿雅行过大能的事:他杀了摩押人亚利伊勒的两个儿子,又在下雪的时候下坑里去杀了一个狮子,
23 Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao.
又杀了一个埃及人。埃及人身高五肘,手里拿着枪,枪杆粗如织布的机轴;比拿雅只拿着棍子下去,从埃及人手里夺过枪来,用那枪将他刺死。
24 Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.
这是耶何耶大的儿子比拿雅所行的事,就在三个勇士里得了名。
25 Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.
他比那三十个勇士都尊贵,只是不及前三个勇士。大卫立他作护卫长。
26 Wale watu mashujaa walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
军中的勇士有约押的兄弟亚撒黑,伯利恒人朵多的儿子伊勒哈难,
27 Shamothi Mharori, Helesi Mpeloni,
哈律人沙玛,比伦人希利斯,
28 Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, Abiezeri kutoka Anathothi,
提哥亚人益吉的儿子以拉,亚拿突人亚比以谢,
29 Sibekai Mhushathi, Ilai Mwahohi,
户沙人西比该,亚合人以来,
30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,
尼陀法人玛哈莱,尼陀法人巴拿的儿子希立,
31 Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, Benaya Mpirathoni,
便雅悯族基比亚人利拜的儿子以太,比拉顿人比拿雅,
32 Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, Abieli Mwaribathi,
迦实溪人户莱,亚拉巴人亚比,
33 Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
巴路米人押斯玛弗,沙本人以利雅哈巴,
34 wana wa Hashemu Mgiloni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari,
基孙人哈深的众子,哈拉人沙基的儿子约拿单,
35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifale mwana wa Uru,
哈拉人沙甲的儿子亚希暗,吾珥的儿子以利法勒,
36 Heferi Mmekerathi, Ahiya Mpeloni,
米基拉人希弗,比伦人亚希雅,
37 Hezro Mkarmeli, Naarai mwana wa Ezbai,
迦密人希斯罗,伊斯拜的儿子拿莱,
38 Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri,
拿单的兄弟约珥,哈基利的儿子弥伯哈,
39 Seleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
亚扪人洗勒,比录人拿哈莱(拿哈莱是给洗鲁雅的儿子约押拿兵器的),
40 Ira Mwithiri, Garebu Mwithiri,
以帖人以拉,以帖人迦立,
41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai,
赫人乌利亚,亚莱的儿子撒拔,
42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,
吕便人示撒的儿子亚第拿(他是吕便支派中的一个族长,率领三十人),
43 Hanani mwana wa Maaka, Yoshafati Mmithni,
玛迦的儿子哈难,弥特尼人约沙法,
44 Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri,
亚施他拉人乌西亚,亚罗珥人何坦的儿子沙玛、耶利,
45 Yediaeli mwana wa Shimri, nduguye Yoha Mtizi,
提洗人申利的儿子耶叠和他的兄弟约哈,
46 Elieli Mmahawi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithma Mmoabu,
玛哈未人以利业,伊利拿安的儿子耶利拜、约沙未雅,摩押人伊特玛、
47 Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai.
以利业、俄备得,并米琐八人雅西业。