< 1 Nyakati 1 >

1 Adamu, Sethi, Enoshi,
Adam Seth Enos
2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
Cainan Malelehel Iared
3 Enoki, Methusela, Lameki, Noa.
Enoch Matusale Lamech
4 Wana wa Noa walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi.
Noe Sem Ham et Iafeth
5 Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
filii Iafeth Gomer Magog Madai et Iavan Thubal Mosoch Thiras
6 Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
porro filii Gomer Aschenez et Rifath et Thogorma
7 Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
filii autem Iavan Elisa et Tharsis Cetthim et Dodanim
8 Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.
filii Ham Chus et Mesraim Phut et Chanaan
9 Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.
filii autem Chus Saba et Evila Sabatha et Rechma et Sabathaca porro filii Rechma Saba et Dadan
10 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.
Chus autem genuit Nemrod iste coepit esse potens in terra
11 Misraimu akawazaa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
Mesraim vero genuit Ludim et Anamim et Laabim et Nepthuim
12 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
Phethrosim quoque et Chasluim de quibus egressi sunt Philisthim et Capthurim
13 Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,
Chanaan vero genuit Sidonem primogenitum et Heth
14 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,
Iebuseum quoque et Amorreum et Gergeseum
15 Wahivi, Waariki, Wasini,
Evheumque et Aruceum et Asineum
16 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Aradium quoque et Samareum et Ematheum
17 Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
filii Sem Aelam et Assur et Arfaxad et Lud et Aram et Us et Hul et Gothor et Mosoch
18 Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi.
Arfaxad autem genuit Sala qui et ipse genuit Heber
19 Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
porro Heber nati sunt duo filii nomen uni Phaleg quia in diebus eius divisa est terra et nomen fratris eius Iectan
20 Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
Iectan autem genuit Helmodad et Saleph et Asermoth et Iare
21 Hadoramu, Uzali, Dikla,
Aduram quoque et Uzal et Decla
22 Obali, Abimaeli, Sheba,
Ebal etiam et Abimahel et Saba necnon
23 Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.
et Ophir et Evila et Iobab omnes isti filii Iectan
24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
Sem Arfaxad Sale
25 Eberi, Pelegi, Reu,
Heber Phaleg Raau
26 Serugi, Nahori, Tera,
Serug Nahor Thare
27 Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).
Abram iste est Abraham
28 Abrahamu alikuwa na wana wawili: Isaki na Ishmaeli.
filii autem Abraham Isaac et Ismahel
29 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari: Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
et hae generationes eorum primogenitus Ismahelis Nabaioth et Cedar et Adbeel et Mabsam
30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
Masma et Duma Massa Adad et Thema
31 Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
Iathur Naphis Cedma hii sunt filii Ismahelis
32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani.
filii autem Cetthurae concubinae Abraham quos genuit Zamram Iecsan Madan Madian Iesboc Sue porro filii Iecsan Saba et Dadan
33 Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.
filii autem Madian Epha et Apher et Enoch et Abida et Eldaa omnes hii filii Cetthurae
34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaki. Wana wa Isaki walikuwa: Esau na Israeli.
generavit autem Abraham Isaac cuius fuerunt filii Esau et Israhel
35 Wana wa Esau walikuwa: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
filii Esau Eliphaz Rauhel Iaus Ialam Core
36 Wana wa Elifazi walikuwa: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
filii Eliphaz Theman Omer Sepphu Gethem Cenez Thamna Amalech
37 Wana wa Reueli walikuwa: Nahathi, Zera, Shama na Miza.
filii Rauhel Naath Zara Samma Maza
38 Wana wa Seiri walikuwa: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
filii Seir Lothan Sobal Sebeon Ana Dison Eser Disan
39 Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
filii Lothan Horri Humam soror autem Lothan fuit Thamna
40 Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana.
filii Sobal Alian et Manaath et Ebal et Sepphi et Onam filii Sebeon Aia et Ana filii Ana Dison
41 Mwana wa Ana alikuwa: Dishoni. Nao wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
filii Dison Amaran et Eseban et Iethran et Charan
42 Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani. Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.
filii Eser Balaan et Zaban et Iacan filii Dison Us et Aran
43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
isti sunt reges qui imperaverunt in terra Edom antequam esset rex super filios Israhel Bale filius Beor et nomen civitatis eius Denaba
44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
mortuus est autem Bale et regnavit pro eo Iobab filius Zare de Bosra
45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
cumque et Iobab fuisset mortuus regnavit pro eo Husam de terra Themanorum
46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
obiit quoque et Husam et regnavit pro eo Adad filius Badad qui percussit Madian in terra Moab et nomen civitatis eius Avith
47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
cumque et Adad fuisset mortuus regnavit pro eo Semla de Masreca
48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
sed et Semla mortuus est et regnavit pro eo Saul de Rooboth quae iuxta amnem sita est
49 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
mortuo quoque Saul regnavit pro eo Baalanan filius Achobor
50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
sed et hic mortuus est et regnavit pro eo Adad cuius urbis fuit nomen Phou et appellata est uxor eius Mehetabel filia Matred filiae Mezaab
51 Naye Hadadi pia akafa. Wakuu wa Edomu walikuwa: Timna, Alva, Yethethi,
Adad autem mortuo duces pro regibus in Edom esse coeperunt dux Thamna dux Alva dux Ietheth
52 Oholibama, Ela, Pinoni,
dux Oolibama dux Hela dux Phinon
53 Kenazi, Temani, Mibsari,
dux Cenez dux Theman dux Mabsar
54 Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.
dux Magdihel dux Iram hii duces Edom

< 1 Nyakati 1 >