< Éxodo 25 >

1 Y él Señor dijo a Moisés:
Yahweh akamwambia Musa,
2 Di a los hijos de Israel que me hagan ofrenda; de cada hombre, de acuerdo a la voluntad en su corazón, tómese una ofrenda.
“Waambie Waisraeli wanitolee sadaka kila mtu nawe utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Lazima upokee hizi sadaka kwa ajili yangu.
3 Y esta es la ofrenda que tomarás: oro, plata y bronce;
Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba,
4 Y tela azul, púrpura y rojo, y el mejor lino y pelo de cabra;
buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi;
5 Y pieles de oveja de color rojo, y cuero, y madera de acacia;
na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, miti ya mjohoro,
6 Aceite para la luz, especias para el aceite de la unción, perfumes dulces para incienso;
mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;
7 Piedras de ónice, piedras de valor para poner en el efod y en él pectoral.
mawe ya shohamu na mawe mengine ya kutiwa kwa ile naivera na kwa kile kifuko cha kifuani.
8 Y que me hagan un santuario, para que pueda estar siempre presente entre ellos.
Waache wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao.
9 Haz el santuario de acuerdo al diseño y todo lo que contiene el santuario de acuerdo a los diseños que te daré.
Lazima ufanye sawa na haya yote nikuoneshayo mfano wa maskani, na vifaa vyake, ndivyo utakavyovifanya.
10 Y harán un cofre de madera de acacia; dos y medio codos de largo, y un codo y medio de y alto.
Wana paswa wafanye sanduku la mti wa mjohoro. Urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu; na upana wake moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
11 Es para ser revestido por dentro y por fuera con el mejor oro, con un borde de oro a su alrededor.
Lazima ulifunike nadni kwa dhahabu safi, na utie na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
12 Y hazle cuatro anillos de oro, para fijar en sus cuatro patas, dos anillos en un lado y dos en el otro.
Nawe uta yayusha katika viduara vinne vya dhahabu, na kuviweka katika miguu yake minne; viduara viwili upande mmoja, na viduara viwili upande wake wa pili.
13 Y haz varillas del mismo palo, cubriéndolas de oro.
Nawe lazima ufanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.
14 Y pon las varas por los anillos a los lados del cofre, para levantarla.
Nawe lazima uweka hiyo miti katika vile viduara vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.
15 Las varillas se mantendrán en los anillos, y nunca se sacarán.
Hiyo miti itakaa katika vile viduara vya sanduku; haitaondolewa.
16 Dentro del cofre debes poner la ley que te daré.
Kisha weka ndani ya sanduku hizo amri nitakazokupa.
17 Y harás una cubierta del mejor oro, de dos codos y medio de largo y un codo y medio de ancho.
Nawe lazima utengeneze kifuniko cha dhahabu safi. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.
18 Y en los dos extremos de la cubierta, harás dos querubines de oro martillado,
Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu katika hiyo miisho miwili ya kiti cha rehema.
19 Uno en un extremo y uno en el otro; los querubines deben ser parte de la portada.
Weka kerubi moja mwisho mmoja wa kiti cha rehema, na kerubi la pili mwisho wa pili. Lazima hao makerubi wawe kitu kimoja na kiti cha rehema.
20 Y sus alas deben extenderse sobre la cubierta, y las alas deben estar opuestas entre sí, de cara a la cubierta.
Na hao makerubi watainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao. Nyuso zao makerubi zitaelekeana na zitaelekea kiti cha rehema.
21 Y pon la cubierta sobre el cofre del pacto, y en el cofre la ley que yo te daré.
Lazima uweke kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha uwe hizo amri nitakazokupa ndani ya sanduku.
22 Y allí, sobre el trono de la gracia entre los dos querubines que están sobre él cofre del pacto, vendré a ti, cara a cara, y te daré los mandamientos que tengo para darte para los hijos de Israel.
Nami nitaonana nawe hapo katika sanduku. Nitazungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema. Itakuwa katikati ya hao makerubi mawili waliyo juu ya sanduku la ushuhuda nitakapo zungumza na wewe katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
23 Y harás una mesa de madera de acacia, de dos codos de largo, un codo de ancho y un codo y medio de altura,
Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
24 Cubierto con el mejor oro, con un borde dorado a su alrededor;
Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.
25 Y haz un marco alrededor de él, tan ancho como la mano de un hombre, con un borde dorado en el marco.
Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote.
26 Y haz cuatro anillos de oro, y ponlos en los cuatro ángulos, sobre las cuatro patas de la mesa;
Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipo kuwa.
27 Los anillos deben fijarse debajo del marco para tomar las varillas con las que se levantará la mesa.
Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.
28 Haz varillas de la misma madera, chapadas con oro, para levantar la mesa.
Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.
29 Y haz los vasos de la mesa, las cucharas, las copas y los tazones para los líquidos, todo con el mejor oro.
Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi.
30 Y en la mesa en todo momento debes guardar mi pan santo.
Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.
31 Y debes hacer un candelabro, del mejor oro; su base y su columna deben ser de oro martillado; sus copas, sus flores deben estar hechos del mismo metal.
Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho.
32 Tiene seis ramas que salen de sus lados; tres ramas de un lado y tres del otro.
Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili.
33 Cada rama tiene tres copas hechas como flores de almendro, cada copa con un capullo y una flor, en todas las ramas.
Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara.
34 Y en el pilar, cuatro copas como flores de almendro, cada uno con su capullo y su flor:
Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake.
35 Y habrá una copa en las primeras dos ramas, y una copa en la segunda dos, rama y una copa en la tercera dos ramas cada uno de los tres pares de brazos que salen del candelabro tendrá un cáliz, para todas sus seis ramas.
Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.
36 Las copas y las ramas deben estar hechos del mismo metal de una sola pieza; todos juntos un trabajo completo de oro martillado.
Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.
37 Entonces debes hacer sus siete vasijas para las luces, poniéndolas en su lugar para que luzcan frente a ellas.
Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.
38 Y las despabiladeras, las bandejas para usar con él tienen que ser del mejor oro.
Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.
39 Se necesitará un talento de oro para ello, con todos estos vasos.
Tumia talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.
40 Ve y los haces conforme al diseño que viste en la montaña.
Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

< Éxodo 25 >