< 1 Crónicas 3 >
1 Estos eran los hijos de David, cuyo nacimiento tuvo lugar en Hebrón: el mayor, Amnón, de Ahinoam de Jezreel; el segundo Daniel, de Abigail la mujer de Carmel;
Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;
2 El tercer, Absalón, hijo de Maaca, hija de Talmai, rey de Gesur; el cuarto, Adonías, el hijo de Haguit;
watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;
3 El quinto, Sefatias, de Abital; el sexto, Itream, de Egla su esposa.
watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.
4 Tenía seis hijos en Hebrón; estuvo gobernando allí durante siete años y seis meses, y en Jerusalén durante treinta y tres años.
Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
5 Y en Jerusalén tuvo cuatro hijos, Simea y Sobab, y Natán y Salomón, de Bet-Sua, la hija de Amiel;
Hawa wana wa nne, kwa Bathshua binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Nathani, na Sulemani.
6 E Ibhar, Elisama, Elifelet.
Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
8 Y Elisama, Eliada y Elifelet, nueve.
Elishama, na Elifeleti.
9 Todos estos fueron hijos de David, además de los hijos de sus concubinas; y Tamar era hermana de ellos.
Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
10 Y el hijo de Salomón fue Roboam, Abías fue su hijo, Asa su hijo Josafat su hijo,
Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
11 Joram su hijo, Ocozías su hijo, Joás su hijo,
Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
12 Amasías su hijo, Azarías su hijo, Jotam su hijo,
Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
13 Acaz su hijo, Ezequías su hijo, Manasés su hijo,
Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
14 Amón su hijo, Josías su hijo.
Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
15 Y los hijos de Josías: el mayor Johanán; el segundo Joacim; el tercer Sedequías; el cuarto Salum.
Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
16 Y los hijos de Joacim: Jeconías su hijo, Sedequías su hijo.
Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
17 Y los hijos de Jeconías, que fue hecho prisionero: Salatiel su hijo y Asir.
Wana wa YehoYakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
18 Y Malquiram, Pedanías, Senazar, Jecamias, Hosama y Nedabias.
Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.
19 Y los hijos de Pedaías: Zorobabel y Simei; y los hijos de Zorobabel: Mesulam y Hananías; y Selomita era su hermana;
Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
20 Y Hasubá, Ohel, Berequías y Hasadías, Jusab-hesed, cinco.
Wanae watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
21 Y los hijos de Hananías: Pelatías y Jesaías; Los hijos de Refaias, los hijos de Arnan, los hijos de Abdias, los hijos de Secanías.
Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
22 Y los hijos de Secanías: Semaías; y los hijos de Semaías: Hatus e Igal, Barias, Nearias, y Safat, seis.
Mwana wa Shekania alikuwa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
23 Y los hijos de Nearías: Elioenai, Ezequías y Azricam, tres.
Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
24 Y los hijos de Elioenai: Hodavias, Eliasib, Pelaias, Acub, Johanan, Dalaias y Anani, siete.
Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.