< Romanos 11 >
1 Pregunto: ¿Dios desechó a su pueblo? ¡Claro que no! También yo soy israelita, de [la] descendencia de Abraham, de [la ]tribu de Benjamín.
Basi nasema, je, Mungu aliwakataa watu wake? Hata kidogo. Kwa kuwa mimi pia ni Mwiisraeli, wa ukoo wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.
2 Dios no desechó a su pueblo, al cual conoció con anticipación. ¿No supieron lo que dice la Escritura en cuanto a Elías, cómo invoca a Dios contra Israel?
Mungu hakuwakataa watu wake, aliowajua tangu mwanzo. Je hamjui andiko linasema nini kuhusu Eliya, jinsi alivyomsihi Mungu juu ya Israeli?
3 Señor, mataron a tus profetas y destruyeron tus altares. Yo quedé solo, y buscan mi vida.
“Bwana, wamewaua manabii wako, nao wamebomoa madhabahu zako. Mimi peke yangu nimesalia, nao wanatafuta uhai wangu.”
4 ¿Pero qué le dice la respuesta divina? Me reservé a 7.000 varones, quienes no doblaron rodilla ante baal.
Lakini jibu la Mungu lasema nini kwako? “Nimetunza kwa ajili yangu watu elfu saba ambao hawampigii magoti Baali.”
5 Así también en el tiempo presente quedó un remanente escogido por gracia.
Hata hivyo, wakati huu wa sasa pia kuna walio salia kwa sababu ya uchaguzi wa neema.
6 Si es por gracia, ya no es por obras. De otra manera, la gracia ya no es gracia.
Lakini ikiwa ni kwa neema, si tena kwa matendo. Vinginevyo neema haitakuwa tena neema.
7 Entonces ¿qué diremos? Lo que Israel buscaba no [lo] obtuvo, pero los elegidos [lo] obtuvieron y los demás fueron endurecidos.
Ni nini basi? Jambo ambalo Israeli alikuwa akitafuta, hakukipata, bali wateule walikipata, na wengine walitiwa uzito.
8 Como está escrito: Dios les dio espíritu de adormecimiento, ojos para no ver y oídos para no oír hasta el día de hoy.
Ni kama ilivyoandikwa: “Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie, mpaka leo hii.”
9 David dice: Que su banquete se convierta en engaño y en trampa, Y en piedra de tropiezo y en pago para ellos.
Naye Daudi anasema, “Acha meza zao na ziwe wavu, mtego, sehemu ya kujikwaa, na kulipiza kisasi dhidi yao.
10 Que se oscurezcan sus ojos para que no vean, Y doble la espalda de ellos para siempre.
Acha macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona. Ukawainamishe migongo yao daima.”
11 Pregunto: ¿Tropezaron para que cayeran? ¡Claro que no! Pero con su transgresión [vino] la salvación a los gentiles para provocarlos a celos.
Basi nasema, “Je, wamejikwaa hata kuanguka?” Isiwe hivyo kamwe. Badala yake, kwa kushindwa kwao, wokovu umefika kwa Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.
12 Si su transgresión es riqueza del mundo, y su derrota, riqueza de los gentiles, ¡cuánto más su plena restauración!
Sasa ikiwa kushindwa kwao ni utajiri wa ulimwengu, na kama hasara yao ni utajiri wa mataifa, ni kiasi gani zaidi itakuwa kukamilika kwao?
13 Pero hablo a ustedes los gentiles por cuanto yo soy apóstol de los gentiles. Honro mi ministerio para ver
Na sasa naongea nanyi watu wa Mataifa. Kwa kuwa nimekuwa mtume kwa watu wa Mataifa mengine, najivunia huduma yangu.
14 si de alguna manera provoco a celos a mis parientes y logro la salvación de algunos de ellos.
Labda nitawatia wivu walio mwili mmoja na mimi. Labda tutawaokoa baadhi yao.
15 Porque si la reprobación de ellos es reconciliación del mundo, ¿qué será su aceptación? Solo vida de entre [los] muertos.
Maana ikiwa kukataliwa kwao ni maridhiano ya dunia, kupokelewa kwao kutakuwaje ila uhai toka kwa wafu?
16 Si lo primero de la masa es santo, también la masa. Si la raíz es santa, también las ramas.
Kama matunda ya kwanza ni akiba, ndivyo ilivyo kwa donge la unga. Kama mzizi ni akiba, matawi nayo kadhalika.
17 Pero si algunas de las ramas fueron desgajadas, y tú, que eras un olivo silvestre, fuiste injertado entre ellas y participaste de la rica savia de la raíz del olivo,
Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, kama wewe, tawi pori la mzeituni, ulipandikizwa kati yao, na kama ulishiriki pamoja nao katika mizizi ya utajiri wa mzeituni,
18 no te enaltezcas contra las ramas. Si te enalteces, recuerda que no sustentas a la raíz, sino la raíz a ti.
usijisifu juu ya matawi. Lakini kama unajisifu, si wewe ambaye unaisaidia mizizi, bali mizizi inakusaidia wewe.
19 Entonces dirás: Unas ramas fueron desgajadas para que yo fuera injertado.
Basi utasema, “Matawi yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika shina.”
20 Tienes razón. Fueron desgajadas por incredulidad, y tú por la fe estás firme. No seas arrogante, sino teme.
Hiyo ni kweli. Kwa sababu ya kutoamini kwao walikatwa, lakini wewe ulisimama imara kwa sababu ya imani yako. Usijifikirie mwenyewe kwa hali ya juu sana, bali ogopa.
21 Porque si Dios no preservó las ramas naturales, tampoco te preservará.
Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, hatakuhurumia wewe pia.
22 Considera, pues, [la ]bondad y [la ]severidad de Dios para los que cayeron, pero bondad para ti, si permaneces en la bondad. De otra manera tú también serás cortado.
Angalia, basi, matendo mema na ukali wa Mungu. Kwa upande mmoja, ukali ulikuja juu ya Wayahudi ambao walianguka. Lakini kwa upande mwingine, wema wa Mungu huja juu yako, kama utadumu katika wema wake. Vinginevyo wewe pia utakatiliwa mbali.
23 Aun ellos, si dejan la incredulidad, serán injertados, porque Dios es poderoso para volverlos a injertar.
Na pia, kama hawataendelea katika kutoamini kwao, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
24 Porque si tú fuiste cortado de un olivo silvestre natural, y contra naturaleza fuiste injertado en un olivo cultivado, ¿cuánto más estas ramas naturales serán injertadas en el propio olivo?
Kwa maana ikiwa ninyi mlikatwa nje kwa ulio kwa asili mzeituni mwitu, na kinyume cha asili mlipandikizwa katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana hawa Wayahudi, ambao ni kama matawi ya asili kuweza kupandikizwa tena ndani ya mzeituni wao wenyewe?
25 Hermanos, para que no presuman de sabios, quiero que sepan este misterio: que a Israel en parte le ocurrió un endurecimiento hasta que entre la plenitud de los gentiles.
Kwa maana ndugu sitaki msijue, kuhusiana na siri hii, ili kwamba msiwe na hekima katika kufikiri kwenu wenyewe. Siri hii ni kwamba ugumu umetokea katika Israeli, hadi kukamilika kwa mataifa kutakapokuja.
26 Así todo Israel será rescatado, como está escrito: El Libertador vendrá de Sion, y quitará la impiedad de Jacob.
Hivyo Israeli wote wataokoka, kama ilivyoandikwa: “Kutoka Sayuni atakuja Mkombozi. Atauondoa uovu kutoka kwa Yakobo.
27 Y éste será mi Pacto con ellos cuando [les] quite sus pecados.
Na hili litakuwa agano langu pamoja nao, wakati nitakapoziondoa dhambi zao.”
28 Ciertamente, en cuanto a las Buenas Noticias, [los judíos] son enemigos por causa de ustedes, pero en cuanto a la elección, son muy amados por Dios por causa de los antepasados.
Kwa upande mmoja kuhusu injili, wanachukiwa kwa sababu yenu. Kwa upande mwingine kutokana na uchaguzi wa Mungu, wamependwa kwa sababu ya mababu.
29 Porque los dones y el llamamiento de Dios son irrevocables.
Kwa kuwa zawadi na wito wa Mungu haubadiliki.
30 Pues así como en otro tiempo ustedes fueron desobedientes a Dios, pero por la desobediencia de ellos, ahora se [les] concedió misericordia,
Kwa kuwa awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmeipokea rehema kwa sababu ya kuasi kwao.
31 así también ahora éstos fueron desobedientes, para que por la misericordia que ustedes recibieron, ellos también logren misericordia.
Kwa njia iyo hiyo, sasa hawa Wayahudi wameasi. Matokeo yake ni kwamba kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi wanaweza pia kupokea rehema.
32 Porque Dios encerró a todos en desobediencia para tener misericordia de todos. (eleēsē )
Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi, ili aweze kuwahurumia wote. (eleēsē )
33 ¡Oh profundidad de [la ]riqueza, de [la ]sabiduría y del conocimiento de Dios! ¡Cuán inalcanzables son sus juicios e inescrutables sus caminos!
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hazichunguziki hukumu zake, na njia zake hazigunduliki!
34 Porque ¿quién entendió [la] mente del Señor? ¿O quién fue su consejero?
“Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani amekuwa mshauri wake?
35 ¿O quién le dio por adelantado para que Él le devuelva?
Au ni nani kwanza aliyempa kitu Mungu, ili alipwe tena?”
36 Porque de Él, por medio de Él y en Él son todas las cosas. ¡A Él sea la gloria por los siglos! Amén. (aiōn )
Kwa maana kutoka kwake, na kwa njia yake na kwake, vitu vyote vipo. Kwake uwe utukufu milele. Amina. (aiōn )