< 2 Crónicas 23 >
1 El año séptimo Joiada se fortaleció. Hizo un pacto con los jefes de centenas: con Azarías, hijo de Jeroham, Ismael, hijo de Johanán, Azarías, hijo de Obed, Maasías, hijo de Adaía, y Elisafat, hijo de Zicri.
Katika mwaka wa sa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
2 Recorrieron Judá para convocar a los levitas de todas las ciudades de Judá y a los jefes de las casas paternas de Israel. Fueron a Jerusalén.
Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.
3 Entonces toda la congregación hizo un pacto con respecto al rey en la Casa de ʼElohim. Joiada les dijo: Aquí está el hijo del rey quien reinará, tal como Yavé habló acerca de los descendientes de David.
Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, “Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.
4 Esto es lo que harán: la tercera parte de ustedes, los sacerdotes y los levitas que entran el sábado, estarán de porteros en las puertas.
Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.
5 Otra tercera parte estará en el palacio real. Otra tercera parte, en la puerta del Fundamento. Todo el pueblo estará en los patios de la Casa de Yavé.
Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
6 Pero nadie entrará en la Casa de Yavé, excepto los sacerdotes y los levitas que ministran. Solo éstos podrán entrar, porque están consagrados. Y todo el pueblo guardará la ordenanza de Yavé.
Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaoatumika. Wao wanaweza kuingia kwa sababu inawahusu.
7 Los levitas rodearán al rey por todas partes, cada uno con sus armas en la mano, y cualquiera que entre en la Casa morirá. Estarán con el rey cuando entre y cuando salga.
Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje.”
8 Los levitas y todo Judá hicieron según todo lo que ordenó el sacerdote Joiada. Tomaron cada uno a sus hombres, a los que entrarían o saldrían el sábado, pues el sacerdote Joiada no dio licencia a los grupos.
Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana
9 Después el sacerdote Joiada entregó a los jefes de centenas las lanzas, los escudos pequeños y los escudos grandes del rey David que estaban en la Casa de ʼElohim.
Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.
10 Colocó a todo la gente en orden alrededor del rey, cada uno con su espada en la mano, desde el lado derecho de la Casa hasta el lado izquierdo, delante del altar y la Casa.
Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.
11 Luego sacaron al hijo del rey, lo coronaron, le dieron el Testimonio y lo proclamaron rey. Joiada y sus hijos lo ungieron y dijeron: ¡Viva el rey!
Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, “Aishi maisha marefu mfalme.”
12 Cuando Atalía oyó el ruido de la gente que corría y aclamaba al rey, se acercó al pueblo en la Casa de Yavé.
Athalia aliposikia kele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.
13 Miró, y ahí estaba el rey en pie en su tarima real en la entrada, y los jefes y trompetistas junto al rey. Todo el pueblo de la tierra estaba alborozado y tocaba las trompetas. Los cantores con los instrumentos musicales dirigían las aclamaciones. Entonces Atalía rasgó sus ropas y exclamó: ¡Conspiración! ¡Conspiración!
na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!”
14 Pero el sacerdote Joiada sacó a los jefes de centenas que comandaban la tropa y les dijo: ¡Déjenla pasar entre las filas, y cualquiera que la siga, que muera a espada! Pues el sacerdote advirtió: No la maten en la Casa de Yavé.
Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, “Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga.” kwa maana kuhani alikwishasema, “Msimuue katika nyumba ya Yahwe.”
15 Así que ellos le abrieron paso, y ella fue hacia la puerta de los Caballos en el palacio real. Allí la mataron.
Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.
16 Entonces Joiada hizo un pacto con el rey y todo el pueblo, según el cual serían el pueblo de Yavé.
kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.
17 Después todo el pueblo fue al templo de baal y lo destruyó, destrozó sus altares y sus imágenes. Mató a Matán, sacerdote de baal, delante de los altares.
Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.
18 Luego Joiada organizó los ministerios en la Casa de Yavé bajo la mano de los sacerdotes levitas, a quienes David distribuyó en la Casa de Yavé para ofrecer los holocaustos a Yavé con regocijo y cánticos, según lo escrito en la Ley de Moisés, como David ordenó.
Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.
19 También estableció porteros en las puertas de la Casa de Yavé, para que ningún impuro entrara por ningún motivo.
Yehoyada akaweka walinzi katika malango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.
20 Luego tomó a los jefes de centenas, los magistrados, los gobernadores del pueblo y todo el pueblo de la tierra y llevaron al rey desde la Casa de Yavé, pasaron por la puerta Superior al palacio real y sentaron al rey en el trono del reino.
Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme. (Baadhi ya maandiko ya ya kisasa yanasema, “wakamshusha chini mfalme”)
21 Todo el pueblo de la tierra se regocijó. La ciudad estaba tranquila, porque mataron a Atalía a filo de espada.
Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.