< 1 Corintios 6 >
1 Si alguno de ustedes tiene algo contra otro, ¿se atreve a denunciar el caso ante los injustos y no ante los santos?
Mmoja wenu anapokuwa na tatizo na mwenzake, anathubutu kwenda kwa mahakama ya wasio haki kuliko mbele ya waumini?
2 ¿No saben que los santos juzgarán al mundo? Si el mundo será juzgado por ustedes, ¿no son capaces de juzgar en casos insignificantes?
Hamjui kuwa waumini watauhukumu ulimwengu? Na kama mtauhukumu ulimwengu, hamuwezi kuamua mambo yasiyo muhimu?
3 ¿No saben que juzgaremos a [los] ángeles? ¡Cuánto más en asuntos de esta vida!
Hamjui kuwa tutawahukumu malaika? Kwa kiasi gani zaidi, tunaweza kuamua mambo ya maisha haya?
4 Cuando ustedes tienen juicios sobre cosas de esta vida, ¿designan como jueces a los de menor estima en la congregación?
Kama tunaweza kuhukumu mambo ya maisha haya, kwa nini mnathubutu kupeleka mashitaka mbele ya wasiosimama kanisani?
5 Digo esto para avergonzarlos. ¿No hay entre ustedes algún entendido que juzgue entre sus hermanos?
Nasema haya kwa aibu yenu. Hakuna mwenye busara miongoni mwenu wa kutosha kuweka mambo sawa kati ya ndugu na ndugu?
6 ¿Alguno denuncia a un hermano ante un tribunal porque peleó contra otro hermano, y esto ante los incrédulos?
Lakini kama ilivyo sasa, mwamini mmoja huenda mahakamani dhidi ya muumini mwingine, na mashitaka hayo huwekwa mbele ya hakimu asiyeamini!
7 Ya es una falta que entre ustedes tengan pleitos. ¿Por qué más bien no soportan la ofensa? ¿Por qué más bien no dejan que los defrauden?
Ukweli ni kwamba kuna matatizo katikati ya Wakristo yaliyoleta tayari usumbufu kwenu. Kwanini msiteseke kwa mabaya? Kwanini mnakubali kudanganywa?
8 Pero ustedes cometen injusticia y defraudan a hermanos.
Lakini mmetenda uovu na kudanganya wengine, na hao ni kaka na dada zenu!
9 ¿No saben que [los] injustos no heredarán [el] reino de Dios? No se engañen: Ni inmorales sexuales, ni idólatras, ni adúlteros, ni afeminados, ni homosexuales,
Hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msiamini uongo. Waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, wafiraji, walawiti,
10 ni ladrones, ni avaros, ni borrachos, ni difamadores, ni estafadores heredarán [el] reino de Dios.
wevi, wachoyo, walevi, wanyang'anyi, watukanaji-hakuna miongoni mwao atakayeurithi ufalme wa Mungu.
11 Esto eran algunos de ustedes. Pero fueron lavados, santificados y declarados justos en el Nombre del Señor Jesucristo y por el Espíritu de nuestro Dios.
Na hao walikuwa baadhi yao ni ninyi. Lakini mmekwisha kutakaswa, lakini mmekwisha kuoshwa, lakini mmekwisha kutengwa kwa Mungu, lakini mmefanywa haki mbele za Mungu katika jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.
12 Todas las cosas me son lícitas, pero no todas me son provechosas. Todas las cosas me son lícitas, pero no permitiré que alguna me domine.
“Vitu vyote ni halali kwangu”, lakini si kila kitu kina faida. “Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini sitatawaliwa na kimoja cha hivyo.
13 El alimento es para el estómago y el estómago para el alimento, pero Dios los inutilizará a ambos. El cuerpo no es para la inmoralidad sexual, sino para el Señor. Y el Señor para el cuerpo,
“Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu atavitowesha vyote. Mwili haujaumbwa kwa ajili ya ukahaba, badala yake, mwili ni kwa ajili ya Bwana, na Bwana atauhudumia mwili.
14 pues Dios, Quien resucitó al Señor, también nos resucitará por medio de su poder.
Mungu alimfufua Bwana na sisi pia atatufufua kwa nguvu zake.
15 ¿No saben que sus cuerpos son miembros de Cristo? ¿Tomaré los miembros de Cristo y los uniré a una prostituta? ¡Claro que no!
Hamjui kwamba miili yenu ina muunganiko na Kristo? Mwawezaje kuvitoa viungo vya Kristo na kwenda kuviunganisha na kahaba? Haiwezekani!
16 ¿No saben que el que se une a una prostituta es un cuerpo con ella? Porque la Escritura dice: Los dos serán un solo cuerpo.
Hamjui kwamba anayeungana na kahaba amekuwa mwili mmoja naye? Kama andiko lisemavyo, “Wawili watakuwa mwili mmoja.”
17 Pero el que se une al Señor es un espíritu con Él.
Lakini anayeungana na Bwana anakuwa roho moja pamoja naye.
18 ¡Huyan de la inmoralidad sexual! Todo pecado que cometa un hombre está fuera del cuerpo, pero el que practica inmoralidad sexual, peca contra su propio cuerpo.
Ikimbieni zinaa! “Kila dhambi aifanyayo mtu ni nje na mwili wake. Lakini zinaa, mtu hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
19 ¿No saben que su cuerpo es Santuario del Espíritu Santo, Quien está en ustedes, el cual recibieron de Dios? ¿[No saben que] ustedes no se pertenecen
Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe?
20 porque fueron comprados por precio? Por tanto enaltezcan a Dios con su cuerpo.
Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu.