< 1 Crónicas 9 >
1 Todo Israel fue registrado según sus genealogías, y están inscritos en el rollo de los reyes de Israel. Y [los] de Judá fueron llevados cautivos a Babilonia, por causa de su infidelidad.
Kwa hivyo watu wote wa Israeli walinakiliwa ki uzao. Walinakiliwa katika vitabu vya kifalme vya Israeli. Yuda, walipelekwa matekani Babylon kwasababu ya dhambi zao.
2 Los primeros que regresaron a sus posesiones en sus ciudades fueron los israelitas: sacerdotes, levitas y servidores del Templo.
Wakwanza kurudi kuishi katika miiji yao walikuwa Waisraeli, Makuhani, Walawi, na Watumishi wa hekalu.
3 En Jerusalén se establecieron algunos de los hijos de Judá, Benjamín, Efraín y Manasés:
Baadhi ya uzao wa Yuda, Benjamin, Efraimu, na Manase waliishi Yerusalemu.
4 Utai, hijo de Amiud, hijo de Omri, hijo de Imri, hijo de Bani, de los hijos de Fares, hijo de Judá.
Wahamiaji walijumusha Uthai mwana wa Ammihudi mwana wa Omri mwana wa Bani, moja ya uzao wa Perezi mwana wa Yuda.
5 De los silonitas, Asaías, el primogénito, y sus hijos.
Kati ya Mashilonite kulikuwa na Asaia mtoto wa kwanza na wana wake.
6 De los hijos de Zera, Jeuel y sus hermanos. Eran 690.
Kati ya uzao wa Zera alikuwa Yeuli. Uzao wao ulikuwa na namba 690.
7 De los hijos de Benjamín, Salú, hijo de Mesulam, hijo de Hodavías, hijo de Asenúa,
Katika uzao Benjamini walikuwa Salu mwana wa Meshulamu mwana wa hodavia mwana wa Hssenua.
8 Ibneías, hijo de Jeroham, Ela, hijo de Uzi, hijo de Micri, y Mesulam, hijo de Sefatías, hijo de Reuel, hijo de Ibnías.
Pia walikuwa Ibneia mwana wa Yerohamu; Ela mwana wa Uzzi mwana wa Mikri; na Meshullam mwana wa Shefatia mwana waReuli mwana wa Ibnija.
9 Sus hermanos según sus familias: 956. Todos estos hombres fueron jefes de familia en sus casas paternas.
Ndugu zao waliandika kwenye orodha ya namba 956 ya vizazi vyao. Wanaume wote hawa walikuwa viongozi wa koo za mababu zao.
10 De los sacerdotes: Jedaías, Joiarib, Jaquín,
Makuhani walikuwa Yedaia, Yehoiarib, na Yokini.
11 Azarías, hijo de Hilcías, hijo de Mesulam, hijo de Sadoc, hijo de Meraiot, hijo de Ahitob, jefe de la Casa de ʼElohim.
Walikuwa pia Azaria mwana wa Hilkia mwana wa Meshullamu mwana wa Zadoki mwana wa Meraioti mwana wa Ahitubi, aliyekuwa na mamlaka katika nyumba ya Mungu.
12 Adaía, hijo de Jeroham, hijo de Pasur, hijo de Malquías. Masai, hijo de Adiel, hijo de Jazera, hijo de Mesul, hijo de Mesilemit, hijo de Imer,
Kulikuwa na Adaia mwana wa Yerohamu mwana wa Pashuri mwana wa Malkija. Pia kulikuwa na Maasai mwanawa Adieli mwana wa Yazera mwana wa Meshulamu mwana wa Meshilemiti mwana wa Imma.
13 y sus hermanos, jefes de sus casas paternas, en número de 1.760, hombres valientes para la obra del servicio en la Casa de ʼElohim.
Ndugu zao, ambao walikuwa viongozi katika koo za mababu zao, idadi ya 1, 760. Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu.
14 De los levitas: Semaías, hijo de Hasub, hijo de Azricam, hijo de Hasabías, de los hijos de Merari,
Kati ya Walawii, kulikuwa na Shemaia mwana wa Hashubu mwana wa Azrikam mwana wa Hashabia, kati ya uzao wa Merari.
15 Bacbacar, Heres, Galal, Matanías, hijo de Micaía, hijo de Zicri, hijo de Asaf,
Walikuwako pia Bakbakari, Hereshi, Galali, na Mattania mwana wa Mika mwana wa Zikri mwana wa Asafu.
16 Obadías, hijo de Semaías, hijo de Galal, hijo de Jedutún. Y Berequías, hijo de Asa, hijo de Elcana, el cual vivió en las aldeas de los netofatitas.
Walikuwako pia Obadia mwana wa Shemaia mwana wa Galali mwana wa Yedutuni; na Berekia mwana wa Asa mwana wa Elkana, aliyeishikatika vijiji vya Netophathites.
17 Y los porteros: Salum, Acub, Talmón, Ahimán y los hermanos de ellos. Salum era el jefe.
Walinzi wa lango walikuwa Shalumu, Akubi, Talimoni, Ahimani, na uzao wao. Shalumu alikuwa kiongozi wao.
18 Hasta entonces estaban encargados de la puerta real, al oriente, y eran porteros de los hijos de Leví.
Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi.
19 Salum, hijo de Coré, hijo de Abiasaf, hijo de Coré, y sus hermanos los coreítas, por la casa de su padre, tuvieron a su cargo la obra del servicio, y cuidaban las puertas del Tabernáculo, como sus padres cuidaban las puertas del campamento de Yavé.
Shalumu mwana wa Kore mwana wa Ebiasafu, ambaye kama mwana wa Kora, na ndugu zake kutoka nyumba ya baba yake, Korahite, alikuwa na mamlaka kwa kazi ya huduma, Walilinda mlango wa hema, kama mababu zao walivyolinda kambi ya Yawehi, na pia walilinda lango la kuingilia.
20 En tiempo antiguo, Finees, hijo de Eleazar, fue jefe de ellos. Yavé estuvo con él.
Finehasi mwana wa Eleaza aliwaongoza kipindi cha nyuma, na Yahwehi alikuwa pamoja nae.
21 Zacarías, hijo de Meselemías, era portero en la entrada del Tabernáculo de Reunión.
Zekaria mwana wa Meshelemia alikua mlinzi katika mlango wa kuingilia hekalu, “eneo la kukutania.”
22 Todos estos, escogidos para vigilar las puertas, eran 212 cuando fueron contados según el orden de sus familias en sus aldeas, a quienes David y el vidente Samuel constituyeron en su oficio.
Hawa wote walichaguliwa kana walinzi wa mageti ya kuingilia kwa idadi ya 212. Majina yao yaliandikwa kwenye kumbukumbu za watu katika vijiji vyao. Mtabiri aliwaweka Daudi na Samueli katika nafasi ya uaminifu.
23 Así ellos y sus hijos eran porteros por turnos en la Casa de Yavé, es decir, la Casa del Tabernáculo.
Kwa hivyo wao na watotot wao walilinda mageti katika nyumba ya Yawehi, hema la kuabudia.
24 Estaban los porteros en los cuatro puntos: hacia el oriente, el occidente, el norte y el sur.
Walinzi wa mageti waliwekwa katika pande zote nne, upande wa mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini.
25 Sus hermanos que vivían en las aldeas llegaban cada siete días para estar con ellos según su turno,
Kaka zao, walioishi kwenye vijiji vyao, walikuja kuwasaidia baada ya mzunguko wa siku saba.
26 porque los cuatro porteros principales, que eran levitas, estaban en servicio permanente a cargo de las cámaras y de los tesoros de la Casa de ʼElohim.
Lakini viongozi wanne wa walinzi, ambao walikwa walawi, walipangiwa kulinda vyumba na vyumba vya kuhifadhi katika nyumba ya Mungu.
27 Pasaban la noche en los alrededores de la Casa de ʼElohim, pues ellos estaban encargados de la guardia y de abrirla cada mañana.
Walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu, kwao ilikuwa ni wajibu wao kulinda. Na walifungua geti kila asubuhi.
28 Algunos de éstos tenían a su cargo los utensilios para el ministerio, los cuales eran contados cuando los guardaban y cuando los sacaban.
Baadhi yao waliwajibika katika hekalu la vifaa; walihesabu makala zilizo ingizwa ndani na zilizo tolewa nje.
29 Otros tenían a su cargo el mobiliario y todos los utensilios del Santuario, la flor de harina, el vino, el aceite, el incienso y las especias;
Baadhi yao pia waliwekwa kutunza vitu vitakatifu, vifaa, na vitu, kujuisha unga safi, mvinyo, mafuta, manukato, na uvumba.
30 y otros, de los hijos de los sacerdotes, preparaban la mezcla de las especias aromáticas.
Baadhi ya wana wa makuhani walichanganya uvumba.
31 Matatías, uno de los levitas, primogénito de Salum coreíta, era responsable de las cosas que se preparaban en sartenes.
Matithia, mmoja wa walawi, ambaye alikuwa mtoto wa kwanza wa Shalumu wa Wakorahi, alikuwa na wajibu wa kuandaa mikate kwa ajili ya sadaka.
32 Algunos de los hijos de Coat y de sus hermanos tenían a su cargo el Pan de la Presencia, para prepararlo cada sábado.
Baadhi ya kaka zao, uzao wa kohathite, waliwajibika kwa mikate ya uwepo, kuandaa kila Sabatho.
33 También había cantores, jefes de casas paternas de los levitas, quienes vivían en las cámaras del Templo, libres de otro servicio, porque estaban en aquella obra día y noche.
Waimbaji na viongozi wa familia ya Walawi waliishi ndani ya vyumba katika mahali takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi, kwa sababu wapiswa kufanya kazi walio pangiwa usiku na mchana.
34 Éstos eran jefes de casas paternas de los levitas según sus familias, jefes que vivían en Jerusalén.
Hawa walikuwa viongozi wa familia miongoni mwa Walawi, kama ilivyo orodheshwa katika kumbukumbu za uzao wao. Waliishi Yerusalemu.
35 En Gabaón vivía Jehiel, padre de Gabaón. El nombre de la esposa de él era Maaca,
Baba wa Gibeoni, Yeiel, ambaye mkewe aliitwa Maaka, aliishi Gibeoni.
36 y Abdón, su hijo primogénito, luego Zur, Cis, Baal, Ner, Nadab,
Mtoto wake wa kwanza alikuwa Abdoni, alafu wana wake Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
37 Gedor, Ahío, Zacarías y Miclot.
Gedori, Ahio, Zekaria, na Mikloti.
38 Miclot engendró a Simeam. Éstos vivían también en Jerusalén enfrente de sus hermanos.
Mikloti alikuwa baba wa Shimeamu. Pia waliishi karibu na kaka yao huko Yerusalemu.
39 Ner engendró a Cis, Cis a Saúl, y Saúl a Jonatán, Malquisúa, Abinadab y Es-baal.
Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. sauli alikuwa baba wa Yonathani, malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
40 Hijo de Jonatán fue Merib-baal, y Merib-baal engendró a Micaía.
Mwana wa Jonathani alikuwa Merib baali. Merib baali alikuwa baba wa Mika.
41 Los hijos de Micaía fueron Pitón, Melec, Tarea y Acaz.
Mwana wa Mika walikuwa pithoni, Meleki, Tahrea, na ahazi.
42 Acaz engendró a Jara, y Jara a Alemet, Azmavet y Zimri, y Zimri a Mosa,
Ahazi alikuwa baba wa Jara. Jara alikuwa baba wa Alemeti, Azmaveti, na zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
43 Mosa a Bina, cuyo hijo fue Refaías, del cual fue hijo Elasa, del cual Azel fue hijo.
Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Refaia. Refaia alikuwa baba wa Eleas. eleasa alikuwa baba wa Azeli.
44 Azel tuvo seis hijos, cuyos nombres son: Azricam, Bocru, Ismael, Searías, Obadías y Hanán.
Wana sita wa Azeli walikuwa Azrikamu, Bochera, Ishmaeli, shearia, Obdia, na Hanani. hawa walikuwa wana wa Azeli