< Isaías 52 >
1 ¡Despierta, despierta, Sión! ¡Sé fuerte! Ponte tus mejores galas, Jerusalén, la ciudad santa. Los extranjeros paganos no volverán a entrar en ti.
Amka, amka, vaa nguvu zako, Sayuni; vaa vazi lako zuri, mji mtakatifu; maana hakuna tena kutotahiriwa wala wasio safi kuingia kwako.
2 Sacúdete del polvo y levántate. Siéntate en tu trono, Jerusalén. Lanza las cadenas de tu cuello, hija cautiva de Sión.
Jikung'ute mwenyewe kutoka mavumbini; nyanyuka na ukae, ewe Yerusalemu; ondoa shanga katika shingo yako, wafungwa, binti ya Sayuni.
3 Esto es lo que dice el Señor: Fuiste vendida por nada, y serás comprada de nuevo sin dinero.
Maana Yahwe asema hivi, umeuzwa bure, na utakombolewa pasipo pesa.''
4 Esto es lo que dice el Señor: En primer lugar, mi pueblo fue a vivir a Egipto, luego Asiria lo conquistó sin razón.
Maana Bwana Yahwe asema hivi, ''Hapo mwanzo watu wangu walishuka chini Misri kuishi kwa muda mfupi; Waasiria waliwanyanyasa wao hivi karibuni.
5 ¿Qué tengo que hacer ahora? pregunta el Señor. Mi pueblo ha sido llevado al cautiverio sin razón alguna. Los que los gobiernan se burlan de ellos, y a mí me tratan con desprecio todo ese tiempo, dice el Señor.
Sasa ni kitu gani nilicho nacho hapa- Hili ni tamko Yahwe- aonae kwamba watu wake wanachukuliwa bure tu? Wale wanowaongoza wao wanafanya mzaha-Hili ni tamko la Yahwe- jina langu linakashifiwa mchan kutwa.
6 Así que voy a hacer que mi pueblo me conozca; en ese momento sabrán que soy yo quien habla en serio. ¡Sí, soy yo!
Hivyo basi watu wangu watalijua jina langu; watajua kwamba siku hiyo kwamba mimi ndiye ninayesema ''Ndiyo, Ni Mimi!''
7 ¡Qué espectáculo tan maravilloso en las montañas es el que corre a traer buenas noticias, anunciando la paz y la buena nueva, anunciando la salvación, diciendo a Sión: “Tu Dios reina!”
Ni kwa uzuri gani juu miliima ni miguu ya mjumbe aliyeleta habari njema, atangazae amani, aliyebeba uzuri wa ukuu, aliyetangaza wokovu, anayesema kwa Sayuni, ''Mungu wako anatawala!''
8 Los vigilantes de la ciudad gritan con fuerza y cantan juntos de alegría; todos ven que el Señor vuelve a Jerusalén.
Sikiliza enyi walinzi nyanyueni sauti zenu, kwa pamoja pigeni kelele kwa furaha, maana mtamuona, kwa kila jicho lenu, kurejea kwa Yahwe Sayuni.
9 Que las ruinas de Jerusalén canten todas de alegría porque el Señor ha venido a cuidar a su pueblo; ha liberado a Jerusalén.
Pazeni sauti kwa kuimba kwa furaha, enyi mateka wa Yerusalemu; maana Yahwe amefariji watu wake; ameikomboa Yerusalemu.
10 El Señor ha demostrado su santo poder a todas las naciones; el mundo entero verá la salvación de nuestro Dios.
Yahwe amewaonyesha kwamba mkono wake mtakatifu katika macho ya mataifa yote; nchi yote itauona wokovu wa Mungu wetu.
11 ¡Salgan, salgan, salgan de ahí! No traigan nada pagano; salgan y dejen todo atrás. Los que llevan los objetos sagrados del Señor deben purificarse.
Ondokeni, ondokeni, enendeni mbali na hapa; msiguse kitu chochote ambacho ni najisi; au kuishi katikati yake; jitakase mwenyewe, enyi mliobeba vyombo vya Yahwe.
12 Pero no salgan con prisa, no se apresuren como si huyeran, porque el Señor irá delante de ustedes, y también protegerá a los de atrás.
Maana hautakwenda nje kwa kukimbia, wala hautaondoka kwa hofu; Maana Yahwe atakuwa mbele yako; na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wako nyuma.
13 Mira: mi siervo actuará con sabiduría; será muy alabado, será elevado en su posición y visto como alguien a quien la gente admira.
Tazameni, mtumishi wangu atafanya hekima; atakuwa juu na atanyanyuliwa juu, na atapandishwa juu.
14 Pero muchos se horrorizaron de él, tan desfigurado en apariencia, que ya no parece un hombre, tan distinto a cualquier ser humano.
Na wengi watamstajabia yeye- muonekano wake umekunjamana nje ya muonekano wa mwanadamu, hivyo basi upande wake ulikuwa mbali na kitu chochote ambacho ni binadamu-
15 Sorprenderá a muchas naciones, y los reyes callarán a causa de él, porque verán lo que no se les ha dicho, y entenderán lo que no habían oído.
Na hivyo, mtumishi wangu atanyunyizia mataifa mengi na wafme watafunga midomo yao kwa sababu yake. Kana kwamba hawajawahi kuambiwa, wataona, kana kwamba hawakusikia, wataelewa.