< San Mateo 16 >
1 Acercáronse los fariseos y saduceos y, para ponerlo a prueba le pidieron que les hiciese ver alguna señal del cielo.
Mafarisayo na Masadukayo walimjia na kumjaribu Yesu awaonyeshe ishara inayotoka angani.
2 Mas Él les respondió y dijo: “Cuando ha llegado la tarde, decís: Buen tiempo, porque el cielo está rojo”,
Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kuwa “Ikiwa ni jioni mnasema kuwa hali ya hewa ni nzuri, kwa kuwa anga ni jekundu.
3 y a la mañana: “Hoy habrá tormenta, porque el cielo tiene un rojo sombrío”. Sabéis discernir el aspecto del cielo, pero no las señales de los tiempos.
Na asubuhi mnasema 'Hali ya hewa leo si nzuri kwa kuwa anga ni jekundu na mawingu yameifunika anga lote.' Mnajua kufasiri mwonekano wa anga, lakini hamwezi kufasiri ishara za nyakati.
4 Una generación mala y adúltera requiere una señal: no le será dada otra que la del profeta Jonás”. Y dejándolos, se fue.
Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakuna ishara yoyote kitakachopewa, isipokuwa ile ya Yona. Kisha Yesu akawaacha na akaenda zake.
5 Los discípulos, al ir a la otra orilla, habían olvidado de llevar panes.
Wanafunzi wakaja upande wa pili, lakini walikuwa wamesahau kuchukua mikate.
6 Y Jesús les dijo: “Mirad y guardaos de la levadura de los fariseos y de los saduceos”.
Yesu akawaambia “Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”
7 Ellos dentro de sí discurrían diciendo: “Es que no hemos traído panes”.
Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. “Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.”
8 Mas Jesús lo conoció y dijo: “Hombres de poca fe; ¿qué andáis discurriendo dentro de vosotros mismos que no tenéis panes?
Yesu alitambua hilo na kusema, “Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate?
9 ¿No entendéis todavía, ni recordáis los cinco panes de los cinco mil, y cuántos canastos recogisteis?
Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya?
10 ¿Ni los siete panes de los cuatro mil, y cuántos canastos recogisteis?
Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlikuchukua?
11 ¿Cómo no entendéis que no de los panes os quería hablar al deciros: “Guardaos de la levadura de los fariseos y de los saduceos?”
Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”
12 Entonces, comprendieron que no había querido decir que se guardasen de la levadura de los panes, sino de la doctrina de los fariseos y saduceos.
Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
13 Y llegado Jesús a la región de Cesarea de Filipo, propuso esta cuestión a sus discípulos: “¿Quién dicen los hombres que es el Hijo del hombre?”
Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, “Watu wanasema kuwa Mwana wa Mtu ni nani?”
14 Respondieron: “Unos dicen que es Juan el Bautista, otros Elías, otros Jeremías o algún otro de los profetas”.
Wakasema,” Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii.
15 Díjoles: “Y según vosotros, ¿quién soy Yo?”
Akawaambia, ninyi mwasema mimi ni nani?
16 Respondiole Simón Pedro y dijo: “Tú eres el Cristo, el Hijo del Dios vivo”.
Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai”
17 Entonces Jesús le dijo: “Bienaventurado eres, Simón Bar-Yoná, porque carne y sangre no te lo reveló, sino mi Padre celestial.
Yesu akamjibu na kumwambia, “Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Y Yo, te digo que tú eres Pedro, y sobre esta piedra edificaré mi Iglesia, y las puertas del abismo no prevalecerán contra ella. (Hadēs )
Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda. (Hadēs )
19 A ti te daré las llaves del reino de los cielos: lo que atares sobre la tierra, estará atado en los cielos, lo que desatares sobre la tierra, estará desatado en los cielos”.
Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni.”
20 Entonces mandó a sus discípulos que no dijesen a nadie que Él era el Cristo.
Kisha Yesu akawaamuru wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye alikuwa ni Kristo.
21 Desde entonces comenzó Jesús a declarar a sus discípulos que Él debía ir a Jerusalén y sufrir mucho de parte de los ancianos, de los sumos sacerdotes y de los escribas, y ser condenado a muerte y, resucitar al tercer día.
Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.
22 Mas Pedro, tomándolo aparte, se puso a reconvenirle, diciendo: “¡Lejos de Ti, Señor! Esto no te sucederá por cierto”.
Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, kwa kusema, “Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako.
23 Pero Él volviéndose, dijo a Pedro: “¡Quítateme de delante, Satanás! ¡Un tropiezo eres para Mí, porque no sientes las cosas de Dios, sino las de los hombres!”.
Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu.”
24 Entonces, dijo a sus discípulos: “Si alguno quiere seguirme, renúnciese a sí mismo, y lleve su cruz y siga tras de Mí.
Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kama mtu yeyote akitaka kunifuata mimi, ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.
25 Porque el que quisiere salvar su alma, la perderá; y quien pierda su alma por mi causa, la hallará.
Kwa kuwa anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na kwa yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
26 Porque ¿de qué sirve al hombre, si gana el mundo entero, mas pierde su alma? ¿O qué podrá dar el hombre a cambio de su alma?
Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?
27 Porque el Hijo del hombre ha de venir, en la gloria de su Padre, con sus ángeles, y entonces dará a cada uno según sus obras.
Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika wake. Naye atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.
28 En verdad, os digo, algunos de los que están aquí no gustarán la muerte sin que hayan visto al Hijo del hombre viniendo en su Reino”.
Kweli nawaambieni kuna baadhi yenu mliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.