< Псалтирь 147 >
1 Хвалите Господа, яко благ псалом: Богови нашему да усладится хваление.
Msifuni Yahwe, kwa maana ni vyema kumwimbia sifa Mungu wetu, ni kuzuri, kusifu kwa faa sana.
2 Зиждай Иерусалима Господь: разсеяния Израилева соберет:
Yahwe huijenga tena Yerusalemu, huwakusanya pamoja watu wa Israeli waliotawanyika.
3 изцеляяй сокрушенныя сердцем и обязуяй сокрушения их:
Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
4 изчитаяй множество звезд, и всем им имена нарицаяй.
Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote.
5 Велий Господь наш, и велия крепость Его, и разума Его несть числа.
Ukuu ni wa Bwana wetu na nguvu zake ni za kutisha, ufahamu wake hauwezi kupimika.
6 Приемляй кроткия Господь, смиряяй же грешники до земли.
Yahwe huwainua wanyonge, huwashusha chini wenye jeuri.
7 Начните Господеви во исповедании, пойте Богови нашему в гуслех:
Mwimbieni Yahwe kwa shukurani, mwimbieni sifa Mungu wetu kwa kinubi.
8 одевающему небо облаки, уготовляющему земли дождь: прозябающему на горах траву и злак на службу человеком:
Huzifunika mbingu kwa mawingu na huiandaa mvua kwa ajili ya nchi, akizifanya nyasi kukua juu ya milima.
9 дающему скотом пищу их, и птенцем врановым призывающым Его.
Huwapa wanyama chakula na wana kunguru waliapo.
10 Не в силе констей восхощет, ниже в лыстех мужеских благоволит:
Hapati furaha katika nguvu ya farasi, wala haridhii miguu imara ya mwanadamu.
11 благоволит Господь в боящихся Его и во уповающих на милость Его.
Yahwe huridhia katika wale wanao muheshimu yeye, watumainio katika uaminifu wa agano lake.
12 Похвали, Иерусалиме, Господа, хвали Бога твоего, Сионе:
Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni.
13 яко укрепи вереи врат твоих, благослови сыны твоя в тебе.
Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
14 Полагаяй пределы твоя мир, и тука пшенична насыщаяй тя:
Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
15 посылаяй слово Свое земли, до скорости течет слово Его,
Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.
16 дающаго снег свой яко волну, мглу яко пепел посыпающаго,
Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
17 метающаго голоть Свой яко хлебы: противу лица мраза Его кто постоит?
Hutupa mvua ya mawe kama makombo, ni nani awezaye kuhimili baridi aitumayo?
18 Послет слово Свое, и истает я: дхнет дух Его, и потекут воды.
Hutuma amri zake na kuziyeyusha, huvumisha upepo wake na hutiririsha maji.
19 Возвещаяй слово Свое Иакову, оправдания и судбы Своя Израилеви:
Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 не сотвори тако всякому языку, и судбы Своя не яви им.
Hajafanya hivyo kwa taifa linginelo lolote, na kama ilivyo amri zake, hawazijui. Msifuni Yahwe.