< Книга пророка Иеремии 10 >
1 Слышите слово Господне, еже глагола Господь на вас, доме Израилев.
“Sikilizeni neno ambalo BWANA anawaambieni, enyi nyumba ya Israeli.
2 Сия глаголет Господь: по путем языков не учитеся и от знамений небесных не страшитеся, яко их боятся языцы.
BWANA asema hivi, 'msijifunze njia za mataifa, na msishangazwe na ishara za mbinguni, kwa kuwa mataifa hushangazwa na haya.
3 Понеже законы языков суетни суть: древо есть от леса изсеченое, дело тектонское и слияние:
Kwa kuwa desturi za watu ni ubatili. Kwa kuwa mtu mmoja hukata mti msituni; kazi ya mikono ya mtu na shoka.
4 сребром и златом украшена суть, и млатами и гвоздьми утвердиша я, да не движутся:
Kisha huzipamba kwa fedha na dhahabu. Huikaza kwa misumari na nyundo ili isitikisike.
5 сребро изваяно есть, не глаголют, носими носятся, понеже ходити не возмогут: не убойтеся их, яко не сотворят зла, и блага несть в них.
Sanamu hizi ni mfano wa sanamu za kutishia ndege katika shamba la matango, kwa kuwa haziwezi kusema chochote. Hubebwa, kwa kuwa haziwezi hata kusogea hatua moja. Usiwaogope, Kwani hawawezi kutenda maovu wala mema.”
6 Несть подобен Тебе, Господи: велик еси Ты и велико имя Твое в крепости.
Hakuna aliye kama wewe, BWANA. Wewe ni mkuu, na jina lako lina nguvu.
7 Кто не убоится Тебе, о, Царю языков! Твоя бо честь между всеми премудрыми языков, и во всех царствах их ни един есть подобен Тебе.
Ni nani asiyekuwa na hofu juu yako, wafalme wa mataifa? Kwa kuwa hiki ndicho unachostahili, kwa kuwa hakuna wa kuwa kama wewe kati ya wote wenye hekima katika mataifa yote au katika hali yao ya enzi.
8 Купно буии и безумнии суть, учение суетных их древо есть:
Wote wako sawa, ni kama wanyama na wapumbavu, wanafunzi wa samamu ambazo si chochote isipokuwa miti tu.
9 сребро извито от Фарсиса приходит, злато от Офаза, и рука златарей, дела вся художников: в синету и багряницу одеют их, дела умоделников вся сия.
Wanaleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi iliyotengenezwa na sonara, ni kazi ya ustadi. Mavazi yao ni ya rangi ya samawi na urujuani. Watu wao stadi waliyafanya haya yote.
10 Господь же Бог истинен есть, Той Бог живый и Царь вечный, от гнева Его подвигнется земля, и не стерпят языцы прещения Его.
Lakini BWANA ni Mungu wa kweli. Yeye ni Mungu aliye hai na mfalme wa milele. Matetemeko yako katika hasira yake, na mataifa hayawezi kuvumilia hasira yake.
11 Тако рцыте им: бози, иже небесе и земли не сотвориша, да погибнут от земли и от сих, иже под небесем суть.
Utawaambia hivi, “Miungu ambayo haikuumba mbingu na nchi itaangamia katika dunia hii na chini ya mbingu.”
12 Господь сотворивый землю во крепости Своей, устроивый вселенную в премудрости Своей, и разумом Своим простре небо.
Aliyeiumba dunia kwa nguvu zake aliumba nchi kavu kwa hekima zake na kuzitandaza mbingu kwa fahamu zake.
13 Ко гласу Своему дает множество вод на небеси: и возведе облаки от последних земли, блистания в дождь сотвори и изведе ветр от сокровищ Своих.
Sauti yake ndiyo itengenezayo muungurumo wa maji mbinguni, naye huzileta mbingu katika mwisho wa dunia. Hutengeneza radi kwa ajili ya mvua na kutuma upepo kutoka katika hazina yake.
14 Буй сотворися всяк человек от ума (своего), постыдеся всяк златоделник во изваяниих своих, яко ложная слия, несть духа в них:
Kila mtu amekuwa mjinga, hawana maarifa. Kila mfua chuma ameaibishwa kwa sanamu zake. Maana sanamu yake ya kuyeyushwa ni uongo; hakuna pumzi ndani yake.
15 суетна суть дела, смеху достойна, во время посещения своего погибнут.
Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu; zitapotea wakati wa hukumu.
16 Несть сицевая часть Иакову, яко Создавый вся Той есть, и Израиль жезл достояния Его, Господь Сил имя Ему.
Lakini Mungu ni fungu la Yakobo, si kama hawa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; BWANA wa majeshi ndiye jina lake.
17 Собра отвне имение, обитающее во избранных,
Kusanya vitu vyako na uiache nchi, wewe ambaye umekuwa ukiishi katika mazingiwa haya.
18 понеже тако глаголет Господь: се, Аз отвергу обитатели земли сея в скорби и смущу их, яко да обрящется язва твоя.
Kwa kuwa BWANA asema hivi, “Tazama, Ni tayari kuwatupa wakazi wa nchi nje wakati huu. Nitawasababishia huzuni, na itakuwa hivyo.”
19 Горе во сокрушении твоем, болезненна язва твоя: аз же рех: воистинну сия болезнь моя (есть) и объят мя, жилище мое опусте, погибе:
Ole wangu! Kwa sababu ya mifupa yangu iliyovunjika, Jeraha zangu zimeumia. Kwa hiyo nilisema. “Hakika haya ni maumivu, lakini lazima nivumilie.”
20 скиния моя опусте, погибе, и вся кожи моя растерзашася: сынов моих и овец моих несть, несть ктому места скинии моей, места кожам моим:
Hema yangu imeharibiwa, na kamba za hema yangu zote zimekatwa. Wamewachukua watoto wangu wote, Kwa hiyo hawaishi tena. Hakuna tena mtu wa kuitandaza hema yangu au wa kuziinua pazia za hema yangu.
21 понеже обуяша пастырие и Господа не взыскаша, сего ради не уразуме все стадо и расточено бысть.
Kwa kuwa wachungaji wamekuwa wapumbavu. Hawamtafuti BWANA. Kwa hiyo hawana mafanikio; Kondoo wao wote wamesambaa.
22 Глас слышания, се, грядет и трус велий от земли северныя, да положит грады Иудины в запустение и во обитание змием.
Taarifa imewadia, “Tazama! inakuja, tetemeko kubwa linakuja kutoka katika nchi ya kaskazini kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, na maficho ya mbweha.
23 Вем, Господи, яко несть человеку путь его, ниже муж пойдет и исправит шествие свое.
Ninajua, BWANA, kwamba njia ya mtu haiji kutoka kwake. Wala hakuna mtu atembeaye anayeongoza hatua zake mwenyewe.
24 Накажи нас, Господи, обаче в суде, а не в ярости, да не умаленых нас сотвориши.
Ee BWANA, unirudi, kwa hukumu za haki, si kwa hasira zako vinginevyo utaniangamiza.
25 Излий гнев Твой на языки не знающыя Тя и на племена, яже имене Твоего не призваша, яко поядоша Иакова и потребиша его и пажить его опустошиша.
Mwaga hasira zako kwa mataifa ambao hawakujui na katika familia ambazo hawakuiti kwa jina lako. Kwa kuwa wamemla Yakobo na kumwangamiza kabisa na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.