< Книга пророка Исаии 66 >
1 Тако глаголет Господь: небо престол Мой, земля же подножие ногу Моею: кий дом созиждете Ми, и кое место покоища Моего?
Yahwe asema hivi, ''Mbinguni ni makao yangu, na nchi ni miguu yangu. Iko wapi nyumba uliyonitengenezea mimi? iko wapi sehemu amabayo ninaweza kupumzika?
2 Вся бо сия сотвори рука Моя, и сия суть вся Моя, глаголет Господь. И на кого воззрю, токмо на кроткаго и молчаливаго и трепещущаго словес Моих?
Mkono wangu umeyafanya haya yote; hivi ndovyo jinsi ambavyo vitu vitatokeavyo—hili ndilo tamko la Yahwe. Mtu niliyempitisha, mwenye roho iliyopondeka na mwenye kujutia roho, na atetemekaye kwa ajili ya neno langu.
3 Беззаконник же жряй ми телца, яко убиваяй пса: и приносяй семидал, яко кровь свиную: даяй ливан в память, аки хулник. И тии избраша пути своя, и мерзости их, яже душа их изволи.
Yeyote achinjae ng'ombe humuua mtu pia; yeye anayetoa sadaka ya kondoo huvunja shingo ya mbwa pia; yeye anayetoa sadaka ya mavuno anatoa sadaka ya damu yangurue; yeye anayetoa kumbukumbuvumba huwabariki wakosaji pia. Wamechagua njia zao wenyewe wanachukua radhi kwa uchafu wao wenyewe.
4 И Аз изберу поругания их и грехи их воздам им: яко звах их, и не послушаша Мене, глаголах, и преслушаша и сотвориша злое предо Мною, и яже не хотех избраша.
Katika njia hiyo hiyo nitachagua adhabu yao wenyewe; Nitaleta juu yao kitu wanachokiogopa, maana niilpowaita, hakuna aliyeitika; nilipozungumza aliyenisikiliza mimi. Walifanya yaliyo maovu mbele yangu, na kuchagua yasiyo nipenindeza mimi.''
5 Услышите глаголгол Господень, трепещущии словесе Его: рцыте, братия, ненавидящым вас и гнушающымся, да имя Господне прославится и явится во веселии их, и они посрамятся.
Sikiliza neno la Yahwe, ewe utemekae kwa neno lake, ''Kaka zako wanaonichukia na kukutenga wewe kwa ajili ya jina langu walisema, 'Na atukuzwe Yahwe, halafu tutaiona furaha yenu; lakini mtatiwa katika aibu.
6 Глас вопля от града, глас от храма, глас Господа воздающаго воздаяние сопротивящымся.
Sauti ya vita vya ghasi vinakuja katika mji, sauti kutoka hekaluni, sauti ya Yahwe anawarudia maadui zake.
7 Прежде неже чревоболети ей, роди, прежде неже приити труду чревоболения, избеже и породи мужеск пол.
Kabla ajaenda katika chumba, hujifungua; kabla ya uchungu kumtoka hujifungua mtoto wa kiume.
8 Кто слыша сицевое, и кто виде сице? Аще родила земля с болезнию во един день? Или и родися язык весь купно, яко поболе и роди Сион дети своя?
Ni nani asikiaye mambo haya? Ni nani aonae mambo haya? Je taifa linaweza kuanzishwa kwa wakati mmoja? lakini kwa haraka Sayuni inapokwenda katika chumba, hujifungua watoto wake.
9 Аз же дах чаяние сие, и не помянул еси Мене, рече Господь. Не се ли, Аз родящую и неплодную сотворих? Рече Бог твой.
Ninawezaje kumleta mtoto azaliwe na nisimruhusu mtoto azaliwe? Yahwe auliza? — au Je ninamleta mtoto wakati tu wa kujifungua na halafu nimshikilie tena - anauliza Yahwe.''
10 Веселися, Иерусалиме, и торжествуйте в нем, вси любящии его и живущии в нем: радуйтеся вкупе с ним радостию, вси елицы плакасте о нем,
Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake!
11 да ссете и насытитеся от сосца утешения его, да ссавше насладитеся от входа славы его.
Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake.
12 Яко сия глаголет Господь: се, Аз укланяю на ня аки реку мира, и аки поток наводняемый славу языков: дети их на рамена взяты будут и на колену утешатся.
Yahwe asema hivi, ''Ni nanakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake.
13 Якоже аще кого мати утешает, тако и Аз утешу вы, и во Иерусалиме утешитеся
Kama vile mama anavyomfariji mtoto wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.''
14 и узрите, и возрадуется сердце ваше, и кости вашя яко трава прозябнут: и познается рука Господня боящымся Его, и запретит непокаряющымся.
Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahweitajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake.
15 Се бо, Господь яко огнь приидет, и яко буря колесницы Его, воздати яростию отмщение Свое и прещение во пламени огненне:
Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao.
16 огнем бо Господним судитися будет вся земля, и мечем Его всяка плоть: мнози язвени будут от Господа.
Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi.
17 Очищающиися и освящающиися во вертоградех и в преддвериих ядущии мясо свиное и мерзости и мышы вкупе погибнут, рече Господь.
Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. ''Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe.
18 И Аз дела их и помышление их вем, и гряду собрати вся народы и языки, и приидут и узрят славу Мою:
Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakatiutafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu.
19 и оставлю на них знамение, и послю от них спасеных во языки, во Фарсис и в Фуд, и в Луд и в Мосох, и в Фовель и во Елладу, и во островы дальния, иже не слышаша имене Моего, ниже видеша славу Мою: и возвестят славу Мою во языцех,
Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.
20 и приведут братию вашу от всех язык дар Господеви, с коньми и колесницами и с носилами мсков, под сеньми во святый град Иерусалим, рече Господь, аки бы принесли сынове Израилевы жертвы своя Мне со псалмы в дом Господень:
Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe.
21 и от тех поиму себе жерцы и левиты, рече Господь.
Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi — asema Yahwe.
22 Якоже бо небо ново и земля нова, яже Аз творю, пребывают предо Мною, глаголет Господь, тако станет семя ваше и имя ваше:
Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu— Hili ndilo tamko la Yahwe— Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki.
23 и будет месяц от месяца, и суббота от субботы, приидет всяка плоть поклонитися предо Мною во Иерусалим, рече Господь:
Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini— asema Yahwe.
24 и изыдут и узрят трупы человеков преступивших Мне: червь бо их не скончается, и огнь их не угаснет, и будут в позор всяцей плоти.
Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hatakufa, na moto huwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.''