< Psalmi 88 >
1 Gospode Bože, spasitelju moj, danju vièem i noæu pred tobom.
Yahwe, Mungu wa wokovu wangu, ninalia mchana na usiku mbele zako.
2 Nek izaðe preda te molitva moja, prigni uho svoje k jauku mojemu;
Sikiliza maombi yangu; utazame kulia kwangu.
3 Jer je duša moja puna jada, i život se moj primaèe paklu. (Sheol )
Maana nimejawa taabu, na uhai wangu umefika kuzimuni. (Sheol )
4 Izjednaèih se s onima koji u grob odlaze, postadoh kao èovjek bez sile,
Watu hunichukulia kama wale waendao chini shimoni; mimi ni mtu asiye na nguvu.
5 Kao meðu mrtve baèen, kao ubijeni, koji leže u grobu, kojih se više ne sjeæaš, i koji su od ruke tvoje daleko.
Nimetelekezwa miongoni mwa wafu; niko kama mfu alalaye katika kaburi, wao ambao wewe huwajari tena kwa sababu wametengwa mbali na nguvu zako.
6 Metnuo si me u jamu najdonju, u tamu, u bezdanu.
Wewe umeniweka katika sehemu ya chini kabisa ya shimo, sehemu yenye giza na kilindini.
7 Oteža mi gnjev tvoj, i svima valima svojim udaraš me.
Gadhabu yako yanielemea, na mawimbi yako yote yanatua juu yangu. (Selah)
8 Udaljio si od mene poznanike moje, njima si me omrazio; zatvoren sam, i ne mogu izaæi.
Kwa sababu yako, wale wanijuao wote hunikwepa. Umenifanya wakutisha machoni pao. Nimefungwa na siwezi kutoroka.
9 Oko moje usahnu od jada, vièem te, Gospode, vas dan, pružam k tebi ruke svoje.
Macho yangu yamefifia kutokana na shida; kila siku nakuita wewe, Yahwe; ninakunyoshea wewe mikono yangu.
10 Eda li æeš na mrtvima èiniti èudesa? ili æe mrtvi ustati i tebe slaviti?
Je! utafanya miujiza kwa ajili ya wafu? Wale waliokufa watafufuka na kukusifu wewe? (Selah)
11 Eda li æe se u grobu pripovijedati milost tvoja, i istina tvoja u truhljenju?
Uaminifu wa agano lako utatangazwa kaburini? au uaminifu wako mahali pa wafu?
12 Eda li æe u tami poznati èudesa tvoja, i pravdu tvoju gdje se sve zaboravlja?
Matendo yako ya ajabu yatajulikana gizani? au haki yako katika mahali pa usahaulifu?
13 Ali ja, Gospode, k tebi vièem, i jutrom molitva moja sreta te.
Lakini ninakulilia wewe, Yahwe; wakati wa asubuhi maombi yangu huja kwako.
14 Zašto, Gospode, odbacuješ dušu moju, i odvraæaš lice svoje od mene?
Yahwe, kwa nini unanikataa? Kwa nini unauficha uso wako mbali nami?
15 Muèim se i izdišem od udaraca, podnosim strahote tvoje, bez nadanja sam.
Nimekuwa nikiteswa kila siku na hatihati ya kifo tangu ujana wangu. Nimeteseka dhidi ya hofu yako kuu; ninakata tamaa.
16 Gnjev tvoj stiže me, strahote tvoje razdiru me.
Matendo yako ya hasira yamepita juu yangu, na matendo yako ya kutisha yameniangamiza.
17 Optjeèu me svaki dan kao voda, stežu me otsvuda.
Siku zote yananizingira mimi kama maji; yote yamenizunguka mimi.
18 Udaljio si od mene druga i prijatelja; poznanici moji sakrili su se u mrak.
Wewe umemuondoa kwangu kila rafiki na anijuaye. Na sasa anijuaye pekee ni giza.