< 1 Abhakorintho 7 >

1 Ahusu amambo ngamsimbiye: Huli isala aje shinza unume asahag'one nushe wakwe.
Kuhusu mambo mliyoniandikia: Kuna wakati ambapo ni vizuri mwanaume asilale na mke wake.
2 Walakini eshi injelo nyinchi iya zinaa shila ashe awe nu nume wakwe, na shila ashe awe nu nume wakwe.
Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe.
3 Unume ahwanziwa apele ushi ihaki yakwe iiyahwengama, shishila ushi nape hwanume.
Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe.
4 Saga yushi yatawala ubele gwakwe, nume. Na shishila unume nape sagatawala ubele gwake ila ushialinao.
Si mke aliye na mamlaka juu ya mwili wake, ni mme. Na vile vile, mme naye hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke anayo.
5 Mngaje ahwimane lwamgona peka, maana mwentehene masala gengo. Muwombaje shesho nkamzahugaje amasala gapute. Epo mzawezye awelelano nantele peka, aje usietono asahahwezye huwapele ingelo nkhasanga muwe ni kiasi.
Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi.
6 Walakini iyanga ega amambo ninene sagaje malajizyo.
Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri.
7 Inyonywa aje shila muntu angahali nazine shindeho. Eshi shila weka alinishipaji shakwe afume hwa Ngolobhe. Ono alinishipaji eshi, ola alinishipaji eshi.
Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile.
8 Hwawasaga wengwilwe na awafyelwe inyanga aje shinza aje wasangale bila ahwengwe, nanzi sindehone.
Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi.
9 Walakini nkasangawawajie huizijile wahuanziwa ahwengwe. Aje aheri ahwengwe kuliko anyonywe.
Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa heri kwao kuolewa kuliko kuwaka tamaa.
10 Eshi hwawala wa wegwilwe ihimbapela indajizyo, saga nene ila yu Bwana. “Ushi asahalehane nu nume wakwe.”
Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. “Mke asitengane na mme wake.”
11 Eshi nkanza alehane afume hwa nuwene asangale shesho asahahwenge, au nkasangashesho akondane nunumeo na unume asahapele.”
Lakini kama akijitenga kutoka kwa mmewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mmewe. Na “Mme asimpe talaka mke wake.”
12 Walakini wawasangee iyanga- ane, saga yu Bwana- aje nkaholo wowonti ali nushi yasanga aputa ayetesha akhale nao, sagahwaziwa huneshe.
Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
13 Nkashee alinunume yasagaputa na ahwenteha ahale nao asahaneshe.
Kama mwanamke ana mme asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.
14 Hwa nume yasanga aputa ahoziwa nola yalinu lweteho ushi wakwe. Na ushi yasanga aputa ahoziwa nola unume yalinulweteho. Nkasanga sishesho awana wwenyu indisaga wazelu, walakini ulioli wozilwe.
Kwa mme asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mmewe aaminiye. Vinginevyo watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.
15 Umpenzi yasagaputa nkasongola asongalaje. Hunamna eyo, usahala nendu sagawapinywa ni ndopo yao. Ungolobhe atikwizizye akhale huamani.
Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka na aende. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani.
16 Umenye wele aje ushi angakombola unumeo? Au umenye wele aje unume angakombola ushi wakwe?
Unajuaje kama mwanamke, huenda utamwokoa mmeo? Au unajuaje kama mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?
17 Shila weka ahale amaisha hwa Bwana shawagawiye, shila wweka nanzi Ungolobhe shakwizizye awene. Owu longozi wane huviwanza vyonti.
Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote.
18 Aleho yahaleho atahiliwe ahakwizi welwe akombolewe? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Sanga ahwaziwa atahiliwe.
Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa.
19 Hueli indola atahiliwa au sanga atahiliwe nagamo amatatizo. Shashili na matatizo hu tii iagizo lya Ngolobhe.
Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.
20 Shila weka asagale shakwizizye Ungolobhe na hukombole.
Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini.
21 Uhali muwomba mbombo amasala Ungolobhe lwahakwizizye? Usahasaje ahusu elyo. Nkashele uwajie awe huru wombanga shesho.
Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hiyo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo.
22 Hwa weka yahakwiziwilwe nu Bwana aje muomba mbombo uyo umntu huru hwa Bwana. Nazi shila weka yali huru lwahakwiziwilwe akombolewe awe muomba mbombo wa Kristi.
Kwa mmoja aliyeitwa na Bwana kama mtumwa ni mtu huru katika Bwana. Kama vile, mmoja aliye huru alipoitwa kuamini ni mtumwa wa Kristo.
23 Amwe mkalililwe hu hung'alama hije msahawe waomba mbombo hwa wantu.
Mmekwisha nunuliwa kwa thamani, hivyo msiwe watumwa wa wanadamu.
24 Wasahala na walendu wane, humaisha gonti shila weka ahakwiziwilwe akombolewe tusagale shishesho
Kaka na dada zangu, katika maisha yoyote kila mmoja wetu tulipoitwa kuamini, tubaki kama vile.
25 Eshi wala wonti wagawejile kamwe sanga indi ni ndajizyo afume hwa Bwana. Ila ihumbapela iseo zyane nazi shindeho. Husanjilo zya Bwana, zizihuaminiha
Sasa, wale wote ambao hawajaoa kamwe, sina amri kutoka kwa Bwana. Lakini nawapa maoni yangu kama nilivyo. Kwa huruma za Bwana, zinazo aminika
26 Kwa hiyo, isewa eshohunongwa ya malawa, shinza unume asagale nazi shaleho.
Kwa hiyo, ninafikiri hivyo kwa sababu ya usumbufu, ni vyema mwanaume abaki kama alivyo.
27 Upinyilwe nushi nishiapo sha hwengane? Usahahanze uuhuru afume hwelyo. Uli nu huru wafume hwashe au saganyegwilwe? Usahahanze ushi.
Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke.
28 Walakini nku yenje sanga uwombile imbiwi. Wasele wala wawahwengana wahugaga amalawa gagali mbalimbali nane ihwanza aje embepuzye ego.
Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.
29 Eshi iyanga ishi awasahala na walendu wane amasala mafupi. Ahwande eshi nahuendelele, walaw wawali na hawashe wakhale aje sagawali na washe.
Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana.
30 Wonti wawazungumie wawenje saga wazungumie na wonti wawashiye wahalije sagawashinye, na wonti wawakala ivintu vyovyonti waweje sanga watawala shoshonti.
Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote.
31 Na wonti wawawomba imbombo zya munsi waweje sanga washunghuliha liohonti. Yaani amatindo ga munsi idujile humalishilo wakwe.
Na wote wanaoshughulika na ulimwengu, wawe kama hawakushughulika nao. Kwa kuwa mitindo ya dunia inafikia mwisho wake.
32 Ihwanza unume yalihura humalawa gonti. Unume yasaga ayejile ahwihusisha ni vintu vivihumsu uBwana, isha hupendezye umwene.
Ninataka muwe huru kwa masumbufu yote. Mwanaume asiyeoa anajihusisha na vitu vinavyo mhusu Bwana, namna ya kumpendeza yeye.
33 Lakini unume ya yejile ahuihusisha na mambo ya dunia, namna ya hupendezye ushi wakwe,
Lakini mwanaume aliyeoa hujihusisha na mambo ya dunia, namna ya kumpendeza mkewe,
34 abaguhene ushi yasagaayegwilwe au unende ahuihusisha ni vintu kuhusu Bwana, inamna ya huibagula hu bele na mpepo. Lakini ushi yayengwilwe ahuihusisha ahusu ivintu vya munsi namna ya hufulaisye unume wakwe.
amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.
35 Iyanga ishi hufaida yenyu, mwemwe na sanga imbeha umtengo humwenyu. Iyanga eshi nalioli aje muwajie huiweshe tayari hwa Bwana bila azigwe nashashonti.
Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.
36 Lakini umntu nkasewa apotilwe humuombele ishishi umwanamwali wakwe, huu seo zwake zili ni ngovu hani leha wegane nao nanzishahwanzya. Sanga mbiwi.
Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi.
37 Lakini awombile shahuanza saga ahwenga nemo ihaja ya ulazima, nkawajiye atawale ihamu yakwe anzawombe shinza nkasanga ahwenga.
Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa.
38 Oyo yahumwenga umwana mwali wakwe awombe shinza, wowonti ola yasaluye sagaahwenga anza wombe shinza hani.
Hivyo, anayemwoa mwanamwali wake afanya vyema, na yeyote ambaye anachagua kutooa atafanya vyema zaidi.
39 Ushi apinyilwe nu nume wakwe uwakati wa ali momi. Lakini nkuleshe unume afyiye ali huru ahwengwe na wowonti yagene, lakini katika Bwana tu.
Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu.
40 Bado katika ahwamle hwane anza songwe hani nkahale nazi shaleho. Na isewa aje nane pia indi nu Mpepo ufinjile.
Bado katika maamuzi yangu, atakuwa na furaha zaidi kama akiishi kama alivyo. Na ninafikiri kuwa nami pia nina Roho wa Mungu.

< 1 Abhakorintho 7 >