< I Koryntian 1 >

1 Paweł, powołany apostoł Jezusa Chrystusa z woli Boga, i Sostenes, brat;
Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,
2 Do kościoła Bożego w Koryncie, do uświęconych w Chrystusie Jezusie, powołanych świętych, ze wszystkimi, którzy w każdym miejscu wzywają imienia naszego Pana Jezusa Chrystusa, ich i naszego [Pana].
tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia.
3 Łaska wam i pokój od Boga, naszego Ojca, i Pana Jezusa Chrystusa.
Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
4 Zawsze dziękuję mojemu Bogu za was, za łaskę Bożą, która została wam dana w Chrystusie Jezusie.
Ninamshukuru Mungu wangu daima kwa ajili yenu kwa sababu amewatunukia ninyi neema yake kwa njia ya Kristo Yesu.
5 We wszystko bowiem jesteście wzbogaceni w nim, we wszelkie słowo i wszelkie poznanie;
Maana, kwa kuungana na Kristo mmetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwa elimu yote na uwezo wote wa kuhubiri,
6 Gdyż świadectwo Chrystusa jest utwierdzone w was;
kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwa ndani yenu,
7 Tak że żadnego daru nie brakuje wam, którzy oczekujecie objawienia naszego Pana Jezusa Chrystusa.
hata hampungukiwi kipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
8 On też utwierdzi was aż do końca, abyście byli nienaganni w dniu naszego Pana Jezusa Chrystusa.
Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia Siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Wierny [jest] Bóg, przez którego zostaliście powołani do społeczności jego Syna, Jezusa Chrystusa, naszego Pana.
Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae Yesu Kristo Bwana wetu.
10 Proszę więc was, bracia, przez imię naszego Pana Jezusa Chrystusa, żebyście wszyscy to samo mówili i żeby nie było wśród was rozłamów, ale abyście byli zespoleni jednakowym umysłem i jednakowym zdaniem.
Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na fikira moja na nia moja.
11 Doniesiono mi bowiem o was, moi bracia, przez [domowników] Chloe, że są wśród was spory.
Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
12 Mówię to dlatego, że każdy z was twierdzi: Ja jestem Pawła, ja Apollosa, ja Kefasa, a ja Chrystusa.
Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,” mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo,”.
13 Czy Chrystus jest podzielony? Czy Paweł został za was ukrzyżowany? Czy w imię Pawła zostaliście ochrzczeni?
Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?
14 Dziękuję Bogu, że oprócz Kryspusa i Gajusa nikogo z was nie ochrzciłem;
Namshukuru Mungu kwamba sikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa tu Krispo na Gayo.
15 Aby nikt nie powiedział, że chrzciłem w swoje imię.
Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jina langu.
16 Ochrzciłem też dom Stefanasa. Poza tym nie wiem, czy ochrzciłem jeszcze kogoś.
(Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
17 Bo Chrystus nie posłał mnie, abym chrzcił, ale abym głosił ewangelię, [i to] nie w mądrości słowa, aby nie zniweczyć krzyża Chrystusa.
Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
18 Mowa o krzyżu bowiem jest głupstwem dla tych, którzy giną, ale dla nas, którzy jesteśmy zbawieni, jest mocą Boga.
Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.
19 Bo jest napisane: Wytracę mądrość mądrych, a rozum rozumnych obrócę wniwecz.
Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na elimu ya wataalamu nitaitupilia mbali.”
20 Gdzie [jest] mądry? Gdzie uczony w Piśmie? Gdzie badacz tego świata? Czyż Bóg nie obrócił w głupstwo mądrości tego świata? (aiōn g165)
Yu wapi basi, mwenye hekima? Yu wapi basi, mwalimu wa Sheria? Naye bingwa wa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanya hekima ya ulimwengu kuwa upumbavu. (aiōn g165)
21 Skoro bowiem w mądrości Bożej świat nie poznał Boga przez mądrość, upodobało się Bogu przez głupstwo głoszenia zbawić tych, którzy wierzą.
Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.
22 Gdyż Żydzi domagają się znaków, a Grecy szukają mądrości.
Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima;
23 My zaś głosimy Chrystusa ukrzyżowanego, [który] dla Żydów wprawdzie [jest] zgorszeniem, a dla Greków głupstwem;
lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;
24 Lecz dla tych, którzy są powołani, zarówno dla Żydów, jak i Greków, [głosimy] Chrystusa – moc Bożą i mądrość Bożą.
lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu.
25 Głupstwo Boże bowiem jest mądrzejsze niż ludzie, a słabość Boża jest mocniejsza niż ludzie.
Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.
26 Przypatrzcie się bowiem, bracia, waszemu powołaniu, że niewielu [jest] mądrych według ciała, niewielu możnych, niewielu szlachetnie urodzonych.
Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu wa tabaka ya juu.
27 Ale Bóg wybrał to, co głupie u świata, aby zawstydzić mądrych, wybrał to, co słabe u świata, aby zawstydzić mocnych.
Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
28 I [to, co] nieszlachetne u świata i wzgardzone, wybrał Bóg, a nawet to, co nie jest, aby to, co jest, obrócić wniwecz;
Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.
29 Aby nie chlubiło się przed nim żadne ciało.
Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu.
30 Lecz wy z niego jesteście w Chrystusie Jezusie, który stał się dla nas mądrością od Boga i sprawiedliwością, i uświęceniem, i odkupieniem;
Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
31 Aby, jak to jest napisane: Ten, kto się chlubi, [niech się] chlubi w Panu.
Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenye kutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana.”

< I Koryntian 1 >