< Markuj 12 >

1 A AP kotin tapiada padaki irail ni karajeraj akan: Aramaj amen me padukedi mat en krep eu o kele pena, ap weirada deun wunit krep eu, o kauada im en jilajil eu, ap mueidalan jaumat akai, ap momaitelan nan wai.
Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
2 Kadekadeo anjaun rak, a ap kadaralan jaumat oko ladu amen, pwen ale ren jaumat oko kijan wan matuel o.
Wakati wa mavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima akamletee sehemu ya mazao ya shamba lake.
3 Re ap jaikidi, kame o ari, kadarala kaip.
Wale wakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
4 A ap pil kadaralan irail amen ladu, re ap kate, pwalan on mona, ap kadarala i kajaroela.
Akatuma tena mtumishi mwingine; huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.
5 A ap pil kadarala amen; re ap kamela; pil me toto re woki akai, a re kamela akai.
Mwenye shamba akatuma mtumishi mwingine tena, na huyo wakamuua. Wengine wengi waliotumwa, baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa.
6 Ari, na ieroj eu, me a pokepoke, i me a kadarala ikmuri, a majani: Re pan wauneki nai ol.
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishowe akamtuma huyo akisema, Watamheshimu mwanangu.
7 A jaumat pukat inda pena nan pun arail: Jeri en jojo met; na, kitail en kamela! Ari, kitail ap pan id aneki jojo o;
Lakini hao wakulima wakaambiana, Huyu ndiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu!
8 Re ap ale, kamela, kajewei jan nan mat en krep.
Kwa hiyo wakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu.
9 Ari, da me jaumaj en mat o pan wia? A pan kodo, kamela jaumat oko; a ap pan mueid on akai matuel o.
“Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na kulikodisha hilo shamba la mizabibu kwa watu wengine.
10 Komail jota wadoker kijin Iikau et: Takai, me jauje kan kajapokelar ap id wialar takai en pukakaim?
Je, hamjasoma Maandiko haya? Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.
11 Mepukat wiauier ren Kaun o, men kapuriamui patail.
Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu.”
12 Irail ari jojon pwen jaikidi i, a re majak aramaj akan, pwe re aja, me a karajeraje kin irail. Irail ari kokola jan re a.
Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walifahamu ya kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtia nguvuni, lakini waliogopa umati wa watu. Basi, wakamwacha wakaenda zao.
13 Irail ap kadaralan re a Parijar o ian en Erodej akai, pwen kajapune i jan ni a majan.
Basi, baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake.
14 Ari, ni ar kodo, re potoan on i: Jaunpadak, je aja, me komui me melel o jota injenoki meamen. Pwe komui jota lipilipil maj en aramaj, a kom kaukawewe al en Kot ni me pun. Me pun, en nopweiki moni on nanmarki de jo? Je en kida, de je ender kida?
Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
15 A a kotin mani ar malaun majani on irail: Menda komail jonejon ia? Wa don ia eu denar en, pwe I en kilan.
Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionyesheni sarafu.”
16 Irail ap wado. A ap kotin majani on irail: Mom o intin en ij met akan? Irail potoan on i: En nanmarki.
Wakamwonyesha. Naye akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”
17 lejuj ap kotin japen, majani on irail: Ari, komail ki on nanmarki me nain nanmarki, o on Kot me japwilim en Kot. Re ap puriamui kila i.
Basi, Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yake Mungu.” Wakashangazwa sana naye.
18 Jadujar akai ap ko don re a, me kin inda me dene jota me pan maureda jan mela. Re ap peidok re a indada:
Masadukayo wasemao kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza,
19 Jaunpadak, Mojej intine don kit er, ma ri en ol amen mela, kidi a paud, jota na jeri ko, a ri a ol ap pan id ale a paud, pwen wiada kadaudok a on ri a ol o.
“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane amzalie watoto ndugu yake marehemu.
20 Ari pirien, ol ijimen mia. Men maj re’rail paude kida li amen ap melar, jota kadaudok a.
Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
21 Men muri ap id ale, ap melar, pil jota kadaudok a. A kajilimen pil dueta.
Ndugu wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu hali kadhalika.
22 A irail ijimen oko paude kida i, jota kadaudok a. Ari, murin karoj li o ari pil melar.
Wote saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa.
23 Ran en iajada ni ar pan maureda, ij me pan paudeki i re’rail, pwe irail ijimen oko paude kier i?
Basi, siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.”
24 lejuj ap kotin japen, majani on irail: Omail jota lelapokki kijin likau kan o rojon en Kot, kaidik iei me kareda omail jaj kida?
Yesu akawaambia, “Ninyi mmekosea sana, kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu.
25 Pwe irail pan lao maureda jan ren me melar akan, re jola pan papaud de kapapaud. A re pan duela tounlan kan me mimi nanlan.
Maana wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni.
26 Ari, duen me melar akan ar pan maureda, komail jota wadoker nan puk en Mojej, duen Kot a kotin majani on i nan wel en tuka o: Nai Kot en Apraain, o Kot en Ijaak, o Kot en Iakop!
Lakini kuhusu kufufuliwa kwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemu inayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto? Mungu alimwambia Mose, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.
27 Kaidin i Kot en me melar akan, pwe Kot en memaureta! Iei, me komail jaj kida kaualap.
Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Ninyi mmekosea sana!”
28 Ari, amen ren jaunkawewe kan ap potodo, me roner duen ar kapakaparok pena, ap kajauiada, me a pajapen me inen, ap idok re a: Ia mo en kujoned karoj?
Mmojawapo wa walimu wa Sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?”
29 lejuj ari majani on i: Iet mo en kujoned akan: Ron Ijrael! Kaun patail Kot me Kaun me ta men.
Yesu akamjibu, “Ya kwanza ndiyo hii: Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake Bwana.
30 Ari, koe en poke ki on Kaun, om Kot, monion om unjok, o nen om unjok, o om lamelam unjok, o om kel unjok! lei met me mo en kujoned akan.
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.
31 A kariau me dueta. let et: Koe en pok on men imp om due pein koe! Jota eu kujoned me lapajan mepukat.
Na ya pili ndiyo hii: Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
32 Jaunkawewe ap potoan on i: Me mau Jaunpadak! Melel me kom majani en! Pwe i me ta men, a jota pil amen, pwe i ota!
Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
33 O poke ki on i monion unjok, o lamelam unjok, o nen unjok, o kel unjok, o pok, on men impa due pein i, mau jan mairon ijij o mairon tei kan.
Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko dhabihu na sadaka zote za kuteketezwa.”
34 Ni en Iejuj a kotin majani a pajapen a inen, a ap majani on i: Kom jota doo jan wein Kot. Ari, ap jolar, me men pil idok re a meakot.
Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwa ujasiri, akamwambia, “Wewe huko mbali na Ufalme wa Mungu.” Baada ya hayo, hakuna mtu aliyethubutu tena kumwuliza kitu.
35 Iejuj ap pil kotin japen majani ni a kotin kaukawewe nan im en kaudok o: Da me jaunkawewe kan indaki, me Krijtuj nain Dawid?
Wakati Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa Sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
36 Pwe pein Dawid majaniki ren Nen jaraui: Kaun o kotin majani on ai Kaun: Kom kotidi on pali maun i, I lao wia kida wutipan aluwilu omui om imwintiti kan!
Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”
37 Ari, Dawid pein kaadaneki I Kaun; a daduen a wia na? Aramaj akan ap mauki a padak.
“Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
38 A ap kotin majani on irail ni a padak: Kalaka jaunkawewe kan, me mauki mi nan likau reirei o men, re en ranmaui ir nan wajan net.
Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
39 O men mod leppantam nan jinakoke kan o kamadip.
na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
40 O noper jan li odi im ar, ap liliajoj kapakap reirei. Irail pan lodi on kadeik lapalap.
Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!”
41 Iejuj ap kotikot jal on deun moni en mairon, ap mamajani, en aramaj ar kajedi on moni nan deu o. A me toto, me kapwapwa, kajedi on me toto.
Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina ya Hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi.
42 Li odi jamama ap kodo o kajedi on kijin moni riakij, me wiada kwadranj eu.
Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha.
43 A ap kotin molipedo japwilim a tounpadak kan, majani on ir: Melel I indai on komail, me liodi jamama men et kajedi on me laude jan irail karoj, me pil kajedi on nan deun moni o.
Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Kweli nawaambieni, huyu mama mjane maskini ametoa zaidi kuliko wengine wote waliotia fedha katika sanduku la hazina.
44 Pwe karoj kajedi on jan ni ar pai. A i me kajedi on jan ni a jamama, karoj me a, i eta a mana.
Maana wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”

< Markuj 12 >