< یوشع 23 >
سالها گذشت و خداوند بنیاسرائیل را از دست دشمنانش راحتی بخشید. در این هنگام یوشع پیر و سالخورده شده بود. | 1 |
Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka,
او تمام بنیاسرائیل را فرا خواند و به بزرگان و رهبران و داوران و مقامات قوم اسرائیل گفت: «من دیگر پیر و سالخورده شدهام. | 2 |
Joshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, “Mimi nimezeeka sana.
شما آنچه را که خداوند، خدایتان به خاطر شما انجام داده است دیدهاید. او خودش با دشمنانتان جنگید. | 3 |
Mmeshaona kila kitu ambacho Yahweh Mungu wenu ameshafanya kwa mataifa haya yote kwa ajili yenu, kwa kuwa ni Yahweh Mungu wenu ambaye amewapigania ninyi.
من زمینهایی را که به تصرف خود درآوردهاید و حتی آنهایی را که هنوز تصرف نکردهاید، بین شما تقسیم نمودهام. تمام این سرزمین، از رود اردن گرفته تا دریای مدیترانه از آن شما خواهد بود؛ زیرا چنانکه خداوند وعده داده است، خود او قبیلههایی را که هنوز میان شما باقی ماندهاند از این سرزمین بیرون خواهد راند تا در آن ساکن شوید. | 4 |
Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi.
Yahweh Mungu wenu atayaondoa. Atayafukuzia mbali kutoka kwenu. Ataiteka nchi yao, nanyi mtaimiliki nchi yao, kama vile Yahweh Mungu wenu alivyowaahidi ninyi.
«اما شما قوی باشید و به دقت دستورهایی را که در تورات موسی نوشته شده است اطاعت کنید و تمام جزئیات آن را نگاه دارید و از آن منحرف نشوید. | 6 |
Hivyo, iweni jasiri, ili kwamba mtunze na kuyafanya yale yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa, msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto,
مواظب باشید با قومهایی که هنوز در میان شما باقی ماندهاند معاشرت نکنید. نام خدایان آنها را هرگز به زبان نیاورید و به نام آنها قسم نخورید، آنها را عبادت نکنید و جلوی آنها زانو نزنید. | 7 |
basi msichanganyikane na mataifa haya ambayo yamesalia miongoni mwenu, wala msiyataje majina ya miungu yao, wala msiape kwayo, wala msiiabudu, wala msiipigie magoti.
بلکه به یهوه، خدای خود بچسبید، همانطور که تا حالا کردهاید. | 8 |
Badala yake, mnatakiwa kumshika sana Yahweh Mungu wenu kama vile mlivyofanya siku hii ya leo.
خداوند، قومهای بزرگ و نیرومند را از پیش روی شما بیرون رانده و تاکنون کسی نتوانسته است در برابر شما بایستد. | 9 |
Kwa kuwa Yahweh ameyafukuzia mbali mbele yenu mataifa makubwa yenye nguvu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama mbele yenu hata siku hii ya leo.
هر یک از شما به تنهایی قادر هستید با یک هزار سرباز دشمن بجنگید و آنها را شکست دهید، زیرا خداوند، خدای شما مطابق قولی که داده است به جای شما میجنگد. | 10 |
Mtu yeyote mmoja wa kwenu atawafanya watu elfu wakimbie mbali, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ndiye anayepigania ninyi, kama vile alivyowaahidi.
پس مواظب باشید که همیشه خداوند، خدای خود را دوست بدارید. | 11 |
Zingatieni kwa uangalifu ili mmpende Yahweh Mungu wenu.
«ولی اگر از خدا روگردان شده، با افراد این قومها که هنوز در میان شما هستند دوست شوید و از آنها زن بگیرید و به آنها زن بدهید، | 12 |
Lakini kama mkiegeuka na kushikamana na watu walioalia wa mataifa haya waliobaki miongoni mwenu, au kuoana nao, au kama mkishirikiana pamoja nao, na wao pamoja nanyi,
مطمئن باشید که خدا این قومها را از سرزمینتان بیرون نخواهد راند، بلکه آنها دامی برای پاهای شما، تازیانهای برای پشت شما، و خاری در چشم شما خواهند بود و شما عاقبت در زمین نیکویی که خداوند، خدایتان به شما داده است هلاک خواهید شد. | 13 |
jueni kwa hakika kwamba Yahweh Mungu wenu hatayafukuzia mbali mataifa haya yatoke kati yenu. Badala yake, watakuwa kitanzi na mtego kwenu, viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu, mpaka pale mtakapoangamia katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
«پایان عمر من فرا رسیده است و همهٔ شما شاهد هستید که هر چه خداوند، خدایتان به شما وعده فرموده بود، یک به یک انجام شده است. | 14 |
Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana.
ولی بدانید همانطور که خداوند نعمتها به شما داده است، بر سر شما بلا نیز نازل خواهد کرد اگر از دستورهای او سرپیچی کنید و خدایان دیگر را پرستش و سجده نمایید. بله، آتش خشم او بر شما افروخته خواهد شد و شما را از روی زمین نیکویی که به شما بخشیده است به کلی نابود خواهد کرد.» | 15 |
Lakini kama kila neno ambalo Yahweh Mungu wenu alilowaahidi limekwisha kutimia, hivyo Yahweh atawaletea juu yenu mabaya yote mpaka pale atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
Atafanya hivi kama mtalivunja agano la Yahweh Mungu wenu, ambalo aliwaagizeni kulitunza. Kama mtaenda na kuiabudu miungu mingine na kuiinamia, ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi, na ninyi mtaangamia upesi katika nchi nzuri ambayo amekwisha kuwapeni ninyi.”