< Tito 2 >
1 Lakini wenga ukoye galyo galongwana bwiso, mundu akuyowe.
Lakini wewe yaseme yale yanayoendana na maelekezo ya kuaminika.
2 Apendo babe ni kiasi, malango, batolii, bannyogope Nnongo, babe na moyo bwiso, kana babe na masaka lii.
Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu.
3 Alwana apendo baibonekiya bene kana bana ndimi ibele, kana babe amanda baugembe.
Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe.
4 Kasi yabe kuayegana aenza galyo gota gonogike ili batame bwiso ni asengo babe, ni bhana babe.
Wanapaswa kufundisha yaliyo mazuri ili kuwaandaa wasichana kwa busara kuwapenda waume zao na watoto wao.
5 Bwisho kuayegana kubhaa atwaanzi baapekanye asengo babe ili kna bhankupulu Nnongo.
Wanapaswa kuwafundisha kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na watii kwa waume zao wenyewe. Inawalazimu kufanya mambo haya ili kwamba neno la Mungu lisitukanwe.
6 kati iyeya alogolyae amisembe kana babe ni batolii.
katika namna iyo hiyo, watieni moyo vijana wa kiume wawe na busara.
7 Kwa ndila yeyote ibekaye kulongele bandu bababone, kwa kasi ntei, mana kamuayagana piyaye, miyegeyo bwiso bababone bhandu bema.
Katika njia zote jiwekeni wenyewe kuwa mfano katika kazi nzuri; na mfundishapo, onesheni uadilifu na heshima.
8 Mulongele ikowe ya ukoto nayangali kasolo, ili lelo wyowyote wyakana aibone oni kwa mwanja n'topu libaya kwitu.
Ongeeni ujumbe wenye afya na usio na dosari, ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe kwa sababu hana baya la kusema juu yetu.
9 Atumwa ban'yuwe angwana babe kwa kila kikowe. pabalikwa kwa y'hegana kwenda taukana nabo.
Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu. Wanapaswa kuwafurahisha na sio kubishana nao.
10 Kana bajibe pale pake bapalikwa bala yee imani hinanoga ili lelo katiwa ndela yoti baganogeye mapundiso gitu gagamusu Nnungu mwokozi witu.
Hawapaswi kuiba. Badala yake, wanapaswa kuonesha imani yote nzuri ili kwamba katika njia zote wayapambe mafundisho yetu kumhusu Mungu mwokozi wetu.
11 Kwa mwanja neema ya Nnungu indabonekana kwa bhandu boti.
Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa watu wote.
12 Itupundisa kana-makowe gangali ki'Nnungu na taman'iya kulunia. Itupundisa tama kwa lunda na haki na katika ndela Nnungu mula wono. (aiōn )
Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia. Inatufundisha kuishi kwa busara, kwa haki, na katika njia za kimungu kwa wakati huu. (aiōn )
13 Wakati watulenda pokya watu ubilia litu lene baraka ubonekane utukupu wa Nnungu witu mkholho na mwokosi witu Yesu kirisitu.
Wakati tunatarajia kupokea tumaini letu lenye baraka, mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
14 Yesu atekwipia mwene kwitu twenga kutulopwa boka kuasi kutupanga pelete, kwa nia yake. Bandu babasahaulilwe babile na kilolo cha panga kasi inanoga.
Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili kutukomboa kutoka katika uasi na kutufanya wasafi, kwa ajili yake, watu maalumu walio na hamu ya kufanya kazi nzuri.
15 Ugalongele na ugakong'ondi makowe haga, ukalipi kwa amuli yoti. kana un'yeketi mundu whowhti akusalawe.
Yaseme na kuyasisitiza mambo haya. Kemea kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.