< Luka 23 >

1 Kipenga soti sayemi, kabampeleka Yesu nnongi ya Pilato.
Mkutano wote wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.
2 Kabatumbwa kunshutumu, kababaya, “Twankutike mundu yolo atilipotosha taifa litu, kwa kuabakiya bandu baneke kutoa kodi kwa kaisari, no baya kuwa ywembe mwene nga Kristo, Mpwalume.”
Wakaanza kumshutumu, wakisema, “Tumemkuta mtu huyu akipotosha taifa letu, kwa kukataza tusitoe kodi kwa Kaisari, na akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, Mfalme.”
3 Pilato kannaluya, no baya, “Je wenga nga mpwalume ba Ayahudi? Ni Yesu kanyangwa no baya, “Wenga wabaya nyoo.”
Pilato akamuuliza, akisema, “Je wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Na Yesu akamjibu akisema, “Wewe wasema hivyo”.
4 Pilato kammakiya kuhani nkolo ni kipenga sa bandu.”Nibona kwaa likosa lya mundu yolo.”
Pilato akamuambia kuhani mkuu na makutano, “Sioni kosa kwa mtu huyu”.
5 Lakini balo batikunsisitiza, kababaya, “Abile akiachochea bandu, atikwapundisha mu'Uyahudi woti, boka Galilaya ni saa yeno abile pano.”
Lakini wao wakasisitiza, wakisema, “Amekuwa akiwachochea watu, akifundisha katika Uyahudi yote, kuanzia Galilaya na sasa yuko hapa.”
6 Pilato ayowine ago, kayangwa kati mundu ywoo ni a'Galilaya?
Pilato aliposikia haya, akaulizia kama mtu huyo ni wa Galilaya?
7 Pabaatangite kuwa abile pae ya utawala wa Herode, atikumpeleka Yesu kwa Herode, ywabile niywembe ywabile Yerusalemu kwa masoba ago.
Alipotambua kuwa alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka Yesu kwa Herode, ambaye naye alikuwa Yerusalemu kwa siku hizo.
8 Herode paamweni Yesu, atipulaika muno kwamana apalike kumwona kwa masoba ganansima. Ayowine habari za ywembe, ni atamaniye kubona yumo ywamuujiza wapangilwe ni ywembe.
Herode alipomuona Yesu, alifurahi sana kwasababu alitaka kumuona kwa siku nyingi. Alisikia habari zake na alitamani kuona moja ya miujiza ikifanywa na yeye.
9 Herode kannaluya Yesu kwa maneno ganansima, lakini Yesu kannyangwa kwaa chochote.
Herode alimhoji Yesu kwa maneno mengi, lakini Yesu hakumjibu chochote.
10 Makuhani akolo pamope ni baandishi bayemi kwa ukali kabanshitaki.
Makuhani wakuu pamoja na waandishi walisimama kwa ukali wakimshitaki.
11 Herode pamope nia askari bake, kabantukana ni kun'geya, ni kummwika ngobo nzuri, boka po atikunrudisha Yesu kwa Pilato.
Herode pamoja na maaskari wake, walimtukana na kumdhihaki, na kumvika mavazi mazuri, kisha akamrudisha Yesu kwa Pilato.
12 Herode ni Pilato babile mbwiga boka lisoba lelo, (kabla ya ago babile maadui)
Herode na Pilato wakawa marafiki kuanzia siku hiyo, (kabla ya hapo walikuwa maadui).
13 Pilato kabakema pamope makuhani akolo ni atawala ni kipenga sa bandu,
Pilato akawaita pomoja makuhani wakuu na watawala na umati wa watu,
14 Kabaakokeya, “Mwaniletii mundu yoo kati mundu ywaongoza bandu bapange abaya, no linga, baada ya kuba ninnaluye nnonge yinu, nibona kwaa likosa kwa mundu yoo husu makowe gote ambago mwenga mwamshitaki ywembe.
Akawaambia, “Mmeniletea mtu huyu kama mtu anaye waongoza watu wafanye mabaya, na tazama, baada ya kuwa nimemhoji mbele yenu, sikuona kosa kwa mtu huyu kuhusu mambo yote ambayo ninyi mnamshitaki yeye.
15 Hapana, Herode kwaa, mana ambuyanganiye kwitu, ni linga ntopo chochote chaakipangite chaastahili adhabu ya waa.
Hapana, wala Herode, kwa maana amemrudisha kwetu, na tazama hakuna chochote alichokifanya kinachostahili adhabu ya kifo.
16 Kwa eyo npala kumwadhibu ni kunneka.
Kwahiyo basi nitamuadhibu na kumuachilia.
17 (Pilato atiwajibika kunneka mfungwa yuno kwa Ayahudi wakati wa sikukuu)
(Sasa, Pilato anawajibika kumuachilia mfungwa mmoja kwa wayahudi wakati wa sikukuu).
18 Lakini bote bakombwi lilobe lyampamo, bakibaya, “Mmulage yoo, ni kunneka Baraba!”
Lakini wote wakapiga kelele pamoja, wakisema, “Mwondoe huyo, na tufungulie Baraba!”
19 Baraba abile mundu ywatabilwe mu'ligereza kwa sababu ya ubou pulani nkati ya ijiji na kubulaga.
Baraba alikuwa ni mtu ambaye amewekwa gerezani kwa sababu ya uasi fulani katika jiji na kwa kuua.
20 Pilato kaabakiya kae, atamaniye kunneka Yesu.
Pilato akawaambia tena, akitamani kumwachilia Yesu.
21 Lakini bembe bakombwi lilobe, babaya, “Mmulage, mmulage.”
Lakini wao wakapiga kelele, wakisema, “Msulibishe, msulibishe.”
22 Kabanaluya kwa mara ye itatu, “mwanja namani, mundu yoo, apangite baya lya namani? mbatike kwaa likosa lyastahili adhabu yo kiwo kwa ywembe. Kwa eyo mana niyomwile kumwadhibu nalowa kunneka.”
Akawauliza kwa mara ya tatu, “kwa nini, huyu mtu amefanya maovu gani? Sikupata kosa linalostahili adhabu ya kifo kwake. Kwahiyo nitakapo maliza kumuadhibu nitamuachilia.”
23 Lakini kabasisitiza kwa lilobe lya kunani, baloba asulubilwe. Ni lilobe lyao lyatikunshawishi Pilato.
Lakini wakasisitiza kwa sauti ya juu, wakitaka asulubiwe. Na sauti zao zikamshawishi Pilato.
24 Nga nyo Pilato atiamua kuwapeya kati kabapala.
Hivyo Pilato akaamua kuwapatia matakwa yao.
25 Kanneka yolo ywampala ywabile atabilwe kwa kupanga ghasia ni kubulaga. Lakini atikuntoa Yesu kati kabapala bembe.
Akamuachilia yule waliyemtaka ambaye alifungwa kwa kusababisha ghasia na kuua. Lakini akamtoa Yesu kwa matakwa yao.
26 Pabannyongoli no yendya, bakwembine ni mundu yumo ywakemilwe Simoni ba Ukirene, kaboka mu'kilambo, kabampeya msalaba apotwi, kunkengama Yesu.
Walipokuwa wakimpeleka, walimkamata mtu mmoja aitwaye Simoni wa Ukirene, akitokea katika nchi, wakamtwika msalaba ili abebe, akimfuata Yesu.
27 Kipenga kikolo sa bandu, ni annwawa babile batihuzunika no kwomboleza kwaajili ya ywembe, babile batikunkengama.
umati mkubwa wa watu, na wanawake ambao walihuzunika na kuomboleza kwa ajili yake, walikuwa wakimfuata.
28 Lakini atikubakelebukia, Yesu no kuabakiya,'Mwannwawa ba Yerusalemu, kana mulele kwaajili yango, ila mulele kwaajili yinu bene ni kwaajili ya bana binu.
Lakini akawageukia, Yesu akawaambia, 'Mabinti wa Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe na kwa ya ajili watoto wenu.
29 Linga, masoba gaisa ambazo balowa baya, “Watibarikilwa balyo agumba ni ndumbo yange beleka, ni mabele yangenyonyesha.
Tazama, siku zinakuja ambazo watasema, “Wamebarikiwa walio tasa na matumbo yasiyozaa, na matiti ambayo hayakunyonyesha.
30 Nga kabatumbwa kuikokeya itombe, “Mututombokii,'na itombe,'Itufunike.'
Ndipo watakapo anza kuiambia milima, 'Tuangukieni,' na vilima, 'Mtufunike.'
31 Mana kati bapangite makowe aga kwa nkongo mbichi, ipalika kwaa wo'ubile nkavu?”
Maana kama wakifanya mambo haya ikiwa mti mbichi, itakuwaje ukiwa mkavu?”
32 Analome wenge, aharibifu abele, batipelekwa pamope ni ywembe ili kababulagilwe.
wanaume wengine, wahalifu wawili, walipelekwa pamoja naye ili wauwawe.
33 Pabaikite mahali pakemelwage Livufu lya ntwe, nga kabansulubisha pamope ni balo aharibifu, yumo upande wa kummalyo ni ywenge upande wenge.
Walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo wakamsulubisha pamoja na wale wahalifu, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu kabaya, “Tate, ubasamei, kwa mana payowa kwaa bapanga namani.”Bembe bapiyite kura, kutaikulya nganju yake.
Yesu alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. “Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.
35 Bandu babile bayemi kabalola ni atawala kaban'geya, kababaya, “Uwalopolile benge. Nga ujilopwe wa mwene, kati wenga wa Kristo wa Nnongo, uchaulilwe.”
Watu walikuwa wamesimama wakiangalia huku watawala wakimdhihaki, wakisema, “Aliwaokoa wengine. Sasa ajiokoe mwenyewe, kama yeye ni Kristo wa Mungu, mteule”.
36 Ni akari kabandharau, kabankaribia ywembe ni kumpea siki,
Askari pia walimdharau, walimkaribia yeye na wakumpa siki,
37 kababaya, “Kati wenga wa Mpwalume ba Ayahudi jilopwe wa mwene.”
wakisema, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi jiokoe mwenyewe”
38 Pabile ni alama nnani yake yaiyandikilwe, “AYOO NGA MPWALUME AYAHUDI.”
Kulikuwa pia na alama juu yake iliyoandikwa “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.”
39 Yumo nkati ya baarifu balo basulubilwe atikuntukana kabaya, “Wenga wa Kristo kwaa? jilopwe wa mwene ni twenga”
Mmoja wa wahalifu aliyesulubishwa alimtukana akisema, “Wewe si Kristo? jiokoe mwenyewe na sisi”
40 Lakini yolo ywenge kayan'yangwa, atikunkemya no baya, “Je wenga wamwishimu kwaa Nnongo, ni ywembe ubile mu'hukumu yeyelo?
Lakini yule mwingine akajibu, akimkemea na akisema, “Je wewe humuogopi Mungu, nawe uko katika hukumu hiyo hiyo?
41 Twenga twabile pano kwa haki, kwa mana twenga twapoki chelo twastahili kwaajili ya makowe yitu. Lakini mundu yoo apangite kwaa chochote kibaya.”
Sisi tupo hapa kwa haki, kwa maana sisi tunapokea kile tunachostahili kwa matendo yetu. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”
42 Atiyongeyekeya, “Yesu nikumbuke nenga mana uyingii mu'upwalume wako.”
Na aliongeza, “Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”
43 Yesu kaankokeya, “Amini nendakumakiya, leno walowa tama pamope ni nenga mu'Paradiso.”
Yesu akamwambia, “Amini nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”
44 Muda woo yabile karibu lisaa lya sita, libendo lyaisa nnani ya nchi yote mpaka saa yo tisa,
Hapo ilikuwa karibu saa ya sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa ya tisa,
45 Bwee wa liumu wateyima. Boka po pazia lya mu'hekalu latipapwanika nkati boka kunani.
Mwanga wa jua ulizimika. Kisha pazia la hekalu likagawanyika katikati kuanzia juu.
46 Kalela kwa lilobe likolo, “Tate umaboko gako nibeka roho yango,” baada yabaya nyoo, awile.
Akilia kwa sauti kuu, Yesu alisema, “Baba mikononi mwako naiweka roho yangu,” baada ya kusema haya, akafa.
47 Muda woo akida abweni galo gatendike atikuntukuza Nnongo kabaya, “Hakika ayoo abile mundu mwene haki.”
Wakati Akida alipoona yaliyotendeka alimtukuza Mungu akisema, “Hakika huyu alikuwa mtu mwenye haki.”
48 Wakati woo kipenga sa bandu balo bayei mpamo shuhudia makowe gapangilwe, babuyangine kabakombwa ifua yabe.
Wakati umati wa watu waliokuja pamoja kushuhudia walipoona mambo yaliyofanyika, walirudi huku wakipiga vifua vyao.
49 Lakini mbwiga bake, ni alwawa balo bankengame boka Galilaya, bayemite kwa mbale kabalola makowe ago.
Lakini marafiki zake, na wanawake waliomfuata toka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiangalia hayo mambo.
50 Linga pabile ni mundu ywakemelwa Ysufu, ywabile yumo wa baraza, mundu nzuri ni mwene haki,
Tazama, palikuwepo na mtu aitwaye Yusufu, ambaye ni mmoja wa baraza, mtu mzuri na mwenye haki,
51 (abile akubaliana kwaa ni maamuzi au makowe ago), boka Armathaya, ijiji sa Uyahudi, wabile utisubiri upwalume wa Nnongo.
(alikuwa hajakubaliana na maamuzi au matendo yao), kutoka Armathaya, mji wa Kiyahudi, ambao ulikua ukisubiria ufalme wa Mungu.
52 Mundu yoo, akwembine ni Pilato, kaloba atole bwega wa Yesu.
Mtu huyu, alimkaribia Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
53 Kantombwa, ni kumwalisha sanda, ni kam'beka mu, likaburi lyabile lyatichongwa mu'liwe, lyabile ntopo mundu asikilwe nkati yake.
Alimshusha, na akauzungushia sanda, na akaumweka katika kaburi lililokuwa limechongwa katika jiwe, ambalo hakuna aliyewahi kuzikwa.
54 Lyabile lisiku lya maandalizi, ni sabato yabile karibu.
Ilikuwa ni siku ya maandalizi, na Sabato inakaribia.
55 Alwawa, baisile nakwe boka Galilaya, batikunkengama, ni babweni likaburi ni mwanja bwega wake waugonjike.
Wanawake, waliokuja nao kutoka Galilaya, walimfuata, na wakaona kaburi na jinsi mwili wake ulivyolazwa.
56 Kababuyangana ni tumbwa andaa manukato ni marashi. Boka po lisiku lya sabato kabapunzika lingana na saliya.
Walirudi na kuanza kuandaa manukato na marashi. Kisha siku ya sabato walipumzika kwa mujibu wa sheria.

< Luka 23 >